Mume anataka kumuacha mke kisa kumpeleka mtoto shule na ex wake

Mkiachana mkiwa mmeshazaa inakuwaga kama kuna ka laana kanawaganda hamtapumzika mpaka mmoja wenu afe
Hakuna chochote ni umalaya wake unamsumbua,

Ndio maana ata uyo x wake alimuacha aliona kabisa sio wife material
 
Well; haibadirishi maana hata ukinibadirisha jinsia; level ya kuchukia vitu vidogo kama hivo niliisha vuka siku nyingi sana
Sawa bibie maana uliniita dogo bila kujua umri wangu nikadhani ni mama yangu
 
wadau huyu Dada tumshauri nn?
Mume wangu anataka kuniacha kwa kumpeleka Mtoto shule Mimi na X ambaye tulizaa kabla ya ndoa!

Mimi ni mama wa watoto 3. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa kwenye mahusiano lakini alikuja kuoa mwanamke mwingine. Mwanzo mimi na yeye hatukuwa tunaongea kabisa kwani aliniacha vibaya, baadaye nilikutana na huyu mume wangu wa sasa. Katika mahusiano alikuwa ni mwanaume mzuri mpaka nikasahau kama nilishawahi kuumizwa.

Mpaka tunafunga ndoa, nilikuwa sifikirii kabisa kuhusu baba wa mtoto wangu, kwani huyu mume wangu alikuwa ananihudumia mimi na mwanangu kwa kila kitu. Kuna kipindi baba wa mtoto alirudi na kuomba msamaha, akasema anataka kuwa sehemu ya maisha ya mtoto na kulipa ada na mambo mengine.

Nilimkubalia na kwa kuwa ni mtoto wangu sikuona haja ya kuomba ruhusa kutoka kwa mume wangu, hivyo akaanza kulipa ada. Baadaye nililazimika kumwambia mume wangu kuwa ada inalipwa na baba yake mtoto, kwani kuna kipindi walilipa ada mara mbili shuleni.

Mume wangu alilipa ada ya mtoto bila kuniambia, wakati huo baba yake alikuwa tayari ameshalipa. Alikasirika kwa nini sikumwambia, lakini nilimwambia ni mwanangu na yule ni baba yake, hivyo ana haki zote. Tuliongea, yakasahaulika kwani watu waliniambia hata kama yeye si baba wa mtoto, kwa heshima nilitakiwa kumwambia kwani alibeba majukumu wakati baba wa mtoto kanitelekeza. Niliomba msamaha, yakamalizika, tukarudi kwenye hali nzuri.

Mtoto wangu amemaliza darasa la saba mwaka huu, na kuna shule mimi na baba yake tulipanga kumpeleka ili afanye usaili, ambayo ipo mkoani. Nilipoongea na mume wangu kumwambia kuwa tunataka kumpeleka mtoto, aliniambia hapendi hicho kitu, kwamba kama ni kumpeleka, nimpeleke mimi mwenyewe au baba yake ampeleke mwenyewe lakini si kuongozana kwenye gari moja mpaka mkoani, alikataa kabisa.

Nilijaribu kumuelewesha kuwa yule tumeshatengana naye, ni mzazi mwenza wangu tu, lakini hata hakujali. Aliniambia, "kama vipi nitakupeleka mimi, ila siwezi kukuruhusu kupanda gari moja na X wako." Nilimwambia hapana, yule ni baba yake mtoto na ana haki hivyo huwezi kunipangia. Aliniambia, "kama ukienda, ukirudi rudi huko huko." Mimi namjua mume wangu, ni mtu wa kunitishia-tishia kwani anahisi hajiamini, kwa kuwa huyo baba wa mtoto ana pesa zaidi, anaona kama ana hofu. Hivyo nilimwambia hapana.

Tulipanga na baba wa mtoto tukampeleka mtoto huko mkoani, nilimuaga lakini hakunijibu chochote. Nilienda na sikufanya chochote, hata usiku nilimpigia video call ili aone kuwa sipo chumba kimoja na huyo mwanaume, lakini hakupokea. Baada ya interview, nilirudi nyumbani ila kufika niliambiwa kuwa baba ameondoka. Nilimpigia simu kumtafuta, akaniambia "nimekuachia nyumba utakaa na watoto, mimi sidhani kama naweza kuendelea kuwa mume wako tena."

Sikufanya chochote, nilikaa kimya nikijua kuwa hasira zikiisha atarudi, lakini juzi nimepewa wito wa kuitwa Baraza la usuluhishi kwani mume wangu amefungua madai ya talaka. Kaka, sijui nifanye nini. Ndoa yangu bado naipenda, sina mahusiano na baba wa mtoto; nilimpeleka tu mtoto, nashindwa kuelewa kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la. Sikulala na X wangu na nimemwambia aongee naye, lakini hataki kabisa. Naomba ushauri wako, kaka, sijui nifanye nini?

HUPANGIWI JIPANGIE MWENYEWE SASA

Ukioa mwanamke aliye na mtoto ni sawa na kununua kiwanja chenye mgogoro.
Msije mka sema sija sema.
😛
 
Pumbavu kabisaa, ushakatazwa bado unaleta kiburi na ndoa bado unaitaka, yaan mnapanga mipango ya mtoto asome wapi na mwanaume mwingine huku uko kwa mwanaume mwingine hiyo si dharau??? na tulishasema single mother waoane na Singo father, huyu akijadili na mwenzake kuhusu mtoto na wewe unajadili huku, alipasha kiporo na wewe unapasha ukianza ndoa 1-0 ni tatizo
 
Kweli umekosea sana.Na kauli zako za awali zilikera pia: eti huyu ni baba wa mtoto wangu ana haki zote!! Ukasahau huyu uliyenaye alikustiri yule baba mtoto alipokutekekeza,ulitakiwa kumheshimu mumeo kwa ama kwenda naye kumpekeka mtoto shule na sio kwenda na X jamani yaani mkawa mume na mke mnampeleka mtoto wenu shule!Kweli umekosea sijui itakuwaje!!
wadau huyu Dada tumshauri nn?
Mume wangu anataka kuniacha kwa kumpeleka Mtoto shule Mimi na X ambaye tulizaa kabla ya ndoa!

Mimi ni mama wa watoto 3. Mtoto wangu wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa kwenye mahusiano lakini alikuja kuoa mwanamke mwingine. Mwanzo mimi na yeye hatukuwa tunaongea kabisa kwani aliniacha vibaya, baadaye nilikutana na huyu mume wangu wa sasa. Katika mahusiano alikuwa ni mwanaume mzuri mpaka nikasahau kama nilishawahi kuumizwa.

Mpaka tunafunga ndoa, nilikuwa sifikirii kabisa kuhusu baba wa mtoto wangu, kwani huyu mume wangu alikuwa ananihudumia mimi na mwanangu kwa kila kitu. Kuna kipindi baba wa mtoto alirudi na kuomba msamaha, akasema anataka kuwa sehemu ya maisha ya mtoto na kulipa ada na mambo mengine.

Nilimkubalia na kwa kuwa ni mtoto wangu sikuona haja ya kuomba ruhusa kutoka kwa mume wangu, hivyo akaanza kulipa ada. Baadaye nililazimika kumwambia mume wangu kuwa ada inalipwa na baba yake mtoto, kwani kuna kipindi walilipa ada mara mbili shuleni.

Mume wangu alilipa ada ya mtoto bila kuniambia, wakati huo baba yake alikuwa tayari ameshalipa. Alikasirika kwa nini sikumwambia, lakini nilimwambia ni mwanangu na yule ni baba yake, hivyo ana haki zote. Tuliongea, yakasahaulika kwani watu waliniambia hata kama yeye si baba wa mtoto, kwa heshima nilitakiwa kumwambia kwani alibeba majukumu wakati baba wa mtoto kanitelekeza. Niliomba msamaha, yakamalizika, tukarudi kwenye hali nzuri.

Mtoto wangu amemaliza darasa la saba mwaka huu, na kuna shule mimi na baba yake tulipanga kumpeleka ili afanye usaili, ambayo ipo mkoani. Nilipoongea na mume wangu kumwambia kuwa tunataka kumpeleka mtoto, aliniambia hapendi hicho kitu, kwamba kama ni kumpeleka, nimpeleke mimi mwenyewe au baba yake ampeleke mwenyewe lakini si kuongozana kwenye gari moja mpaka mkoani, alikataa kabisa.

Nilijaribu kumuelewesha kuwa yule tumeshatengana naye, ni mzazi mwenza wangu tu, lakini hata hakujali. Aliniambia, "kama vipi nitakupeleka mimi, ila siwezi kukuruhusu kupanda gari moja na X wako." Nilimwambia hapana, yule ni baba yake mtoto na ana haki hivyo huwezi kunipangia. Aliniambia, "kama ukienda, ukirudi rudi huko huko." Mimi namjua mume wangu, ni mtu wa kunitishia-tishia kwani anahisi hajiamini, kwa kuwa huyo baba wa mtoto ana pesa zaidi, anaona kama ana hofu. Hivyo nilimwambia hapana.

Tulipanga na baba wa mtoto tukampeleka mtoto huko mkoani, nilimuaga lakini hakunijibu chochote. Nilienda na sikufanya chochote, hata usiku nilimpigia video call ili aone kuwa sipo chumba kimoja na huyo mwanaume, lakini hakupokea. Baada ya interview, nilirudi nyumbani ila kufika niliambiwa kuwa baba ameondoka. Nilimpigia simu kumtafuta, akaniambia "nimekuachia nyumba utakaa na watoto, mimi sidhani kama naweza kuendelea kuwa mume wako tena."

Sikufanya chochote, nilikaa kimya nikijua kuwa hasira zikiisha atarudi, lakini juzi nimepewa wito wa kuitwa Baraza la usuluhishi kwani mume wangu amefungua madai ya talaka. Kaka, sijui nifanye nini. Ndoa yangu bado naipenda, sina mahusiano na baba wa mtoto; nilimpeleka tu mtoto, nashindwa kuelewa kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la. Sikulala na X wangu na nimemwambia aongee naye, lakini hataki kabisa. Naomba ushauri wako, kaka, sijui nifanye nini?

HUPANGIWI JIPANGIE MWENYEWE SASA
 
Siyo kweli!
Li mwanamke lile ndilo takataka. Namsubiri huyu wa kwangu afungue kopo lake kusema eti baba wa mtoto anataka one, two three! Hakuna rangi ataacha kuona siku hiyo! Yaani nimekosana na ndugu zangu shauri ya kumlelea mtoto wake halafu aje atoe ushuzi wake hapa? Ole wakeeee! In short hilo dada linalotaka ushauri ni takataka!
Kumbe umeona single maza
Mwenzako aliingia uwanjani na handicap ya 1-0
Komaa mzee usisahau aliyetoa bikra yake naye lazima ale mzigo
Hivi unaoaje mke wa mtu?
 
Nimeshangaa simps na wanaume wapumbavu wanasema eti mpaka ulione kaburi la baba wa mtoto ndio ufanye maisha na single mom

Wajinga wakubwa nyie awe baba wa mtoto amekufa au yuko hai mwanaume anayejielewa haoi single mom hata siku moja
Unaoaje mke wa mtu mzee
Utakuwa looser
 
Hii inaweza kuwa hadithi ya kutunga. Lakini inaakisi ukweli wa akili za wanawake wetu!
Huyu mwanamke ni mtaka yote ! Na alikuwa anampanda kichwani mumewe!
Hawa wakijeruhiwa wanamlaumu shetani!
 
Kiislam hairuhusiwi kutoka na yeyote ambae siyo mumeo na anaeweza kukuowa, iwe umeolewa au hujaolewa. Na hata ukipewa rukhsa na mumeo bado hairuhusiwi Kiislam.

Sijuwi kwa imani zingine.

Kama wote hao hamjawahi kuowana kwa ndoa na mlizaa tu, hakuna mwanamme mwenye mtoto hapo, wote ni wa mama.
Noma sana!
 
Kwanza kusema TU "Mumeo hajiamini kwa sababu x wako anahela kuliko yeye" hapo umeonyesha ilivyo na dharau kwake na kujipendekeza kwa x maana anahela kuliko Mumeo.

Pili kuruhusu mtoto wako kulelewa na Mumeo "masikini" wakati baba yake yupo na "ni tajiri" ilikua ni upendo mkubwa sana kwa Huyo baba lakini umeuharibu. Ni ngumu sana kukurudia Tena kwa upendo.

Dharau kubwa zaidi ni kuondoka bila ruhusa ya mmeo umejiona wewe unamaamuzi kuliko Mumeo, unamjali X wako alichokuambia kuliko anachosema mmeo.

Jilaumu kwa hayo na ndio maana Huyo uliyezaa nae MWANZO hakukuoa
 
Back
Top Bottom