Mume wa Maunda Zoro ni mfano wa Wanaume wa hovyo wa Dar es Salaam

Mume wa Maunda Zoro ni mfano wa Wanaume wa hovyo wa Dar es Salaam

Msijitie ujuaji wa kijinga humu Jf, mumewe hakuwa karibu na tukio la ajali.

Psychologiacally unapopokea habari za tukio kama hilo na unaona hakuna uwezekano wa wewe kufika kwenye tukio haraka ni lazima ujaribu kupiga kwa kila aliyepo karibu ili kuwastress wafike kwenye tukio.

Mlitaka apae au?
Hapana aruke kama chura
 
Maunda alitoka msibani..

Lakini baadae akapitia sehemu, umeiona ile video ya alivyovaa huko alipopitia.? Kavaa kigauni kifupi kapiga make up huku kakumbatiana na mwanaume anaimba na anaonekana alilewa..

Ukiiona hiyo video utapata majibu mengi sana..

Maana yake alibadilisha nguo alibadilishia wapi.??? Alipakia make up wapi.?

Unaniacha nyumbani na watoto unaaga unaenda msibani, unapitia sehemu kulewa ukiwa na mwanaume, unarudi saa4 ..

Wanaumr tunapitia mengi sana..
Maunda kuna kipindi si alikuwa drugs addict pamoja na Hawa wa nitarejea wa Platnumz
 
Nyie si mnaangalia hela jamaa hela anazo kama alimwambia aache kuimba akakubali basi jua huyo mume wake sio kapuku halafu ukiangalia mda aliopata ajali unagundua kuna kitu hakipo sawa mke wa mtu saa nne hujarudi nyumbani upo bar kweli inamaana hawakuwa na mawasiliano mazuri
Endeleeni kuangalia wenye pesa matokeo yake ndio hayo.
Endelea kujidanganya hivyo hivyo usitafute hela,endelea kujifariji
 
Mwanamke malaya ukimpenda mkaoana na akazaa kumuacha inakuwa kazi .ila kila anavyocheat hadharan watu tunashindwa hata kukaa baa unawaza hawa wote washanipigia ,watu wanajiua wanapata pressure unafikia mahali unamuona kama mwendazake kuwa kumuua dhambi ila wajuu akifanya saaafi
Hiki ndicho ninachokiona..unawezakuta hapo ni kama jamaa kautua mzingo mzito mabegani.
 
Nimesikitishwa sana na Kifo cha Maunda Zoro, vibao vyake ni vya enzi zangu nilivipenda sana. Nakumbuka mchumba wangu wa enzi hizo akiniimbia Nataka niwe wako.

Ila nimesikitika zaidi kwa kuwa alikua akiishi na mtu wa hovyo sana. Ambaye mbali na kukaa nae miaka yote akimzalisha watoto watatu bila kufunga ndoa, pia hakuwahi kumjali.

Ukimsikiliza akihojiwa anasema alipigiwa simu mkewe kapata ajali, akaendelea kukaa Nyumbani huku akiwasiliana na watu. Anasema "MAMA akaniambia usitoke nikampigia RTO akasema ndio wanajaribu kumtoa, nampigia mdogo wangu aendee akafika baada ya kama dakika kumi akaniambia kafika ila bado wanahangaika kumtoa. Hatimaye wamemtoa kafariki."

Mwisho anasema kama angepatiwa huduma ya kwanza mapema angepona kwasababu kama kwa kuchelewa kupata Msaada. Wakati yeye alibaki Nyumbani akichat.
Msiendeshe vyombo vya moto mkiwa "mmelewa",hii itasaidia kuondoa lawama kama hizi,ajali ndogo ndogo na vifo visivyo na lazima..... TAFADHALI UKIJIONA UMELEWA USIENDESHE GARI/PIKIPIKI.
 
Hata mimi nimeshangaa, ukifuatilia hiki kisa youtube unaweza kulia, mapaka sasa najiuliza kwa nini mke hakuondoka, hivo ana kipaji angeweza kuanza upya na kutengeneza pesa ambayo ingemsaidia kuishi na watoto wake
Dini na hadhi ndo zimesababisha haya
 
Watu tumekuwa wepesi sana wa kuhukumu haraka haraka tukisikia uongo wowote unao anzishwa mitandaoni

Tatizo ni kwamba akifariki mtu tena akiwa maarufu kitu cha kwanza kabisa huwa kinakuwa ni kumtafuta wa kumbebesha lawama kwa hicho kifo, so kwa sababu tu jamaa hakufika eneo la ajali basi sababu imepatikana

Watu hawajui tu jinsi jamaa alivyopata tabu na Marehemu amemvumilia mengi sana sababu anampenda na kumjali

Kasumba ya marehemu asemwi vibaya ndio inayoficha ukweli hadi jamaa anaonekana mbaya

Ukweli ni kwamba Maunda alikua mrahibu wa madawa ya kulevya na wenzake kadhaa pale THT aikiwemo Hawa wa aliyeimba na Domo
Lakini pia Maunda ni mlevi wa kupindukia, yaani mlevi kweli kweli amempiga jamaa matukio mengi sana
Hadi anafariki kwenye drugs alikua ana in and out lakini pombe hakuwahi kuacha, hata sababu ya ajali haitajwi kabisa lakini ukweli ni kwamba alikua tila lila kwa pombe
Mind you aliaga anakwenda msibani lakini kaisha kulewa

Jamaa alimvumilia wakati wote akijitahidi kuhakikisha Marehemu anakua safi lakini watu hawajui haya yote wanaishia kumlaumu

Kifo ni kifo wala jamaa hajasababisha kwa namna yoyote ile
Jamaa hakika ni mtu mvumilivu sana na anayejali kwa jinsi alivyo mvumilia marehemu na kasoro zake za mihadarati na pombe

Imekua sasa ni kama fasheni akifa mtu maarufu basi ni lazima kuna uzembe......, sasa mnataka tufe makabwela tu ndio ionekane sahihi ebooo
 
Mbona sijakutukana nimekupa cheo chako, Mtu asiye na akili si mbumbumbu au tutusa? Maanake nyie hata kutawaza ni mpaka muambiwe na mama
 
Back
Top Bottom