Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Hujawahi kuwa mwanamke unajuaje hitaji lao?
Ndoa ni huko zamani sio sasa hivi majanga matupu.
Mimi ni mwanamke naona ndoa ni upuuzi sasa unasemaje ni hitaji la kila mwanamke?
Kwamba siku hizi ndoa sio hitaji la Mwanamke tena, you are wrong my dear.

Ungejua Waganga wa kienyeji na hao manabii uchwara wanavyowalia hela Wanawake wenzio kisa kupata ndoa hata usingesema hivyo.

Hitaji bado ni kubwa mno huko kwa ground
 
Wewe jamaa Mbona huwa hunamsimamo unachokisimamia juu ya hawa wanawake.

Au ndiyo ukijua kuandika imeisha hivyo?
 
Emu wajengee dunia yao watoto wako waishi huko na wayafanye haya Ila kwa dunia hiibhawana nafasi kabisa na utawafanya wawe watu wachini kuwahi kutokea,

Hili huwafundishi tu watoto wako Ila na mkeo, atatoka kwenye kukuheshim na ataishi kibabe kwako, huenda Hana kipato Cha kumpa uhuru na kibri kama ulivosema Ila atamtafuta sponsor wakumfanya awe hivo.

Maneno yanaumba ndugu yangu jiandae kwa haya maombi uliyotuma kwa mungu wako

Katika maisha unamfaninishaje au unamwekaje mwanamke au mwanaume kwenye nafasi moja na mzazi??

Ngoja mkeo asome andiko hili alafu yakukute urudi hapa utupe upande wa pili wa fikra zako.

Yaan mpaka Leo humjui mwanamke kaka, unafikri vitabu vitakatifu vimekosea kutuambia tuishi nao kwa akili,
 
Kwamba siku hizi ndoa sio hitaji la Mwanamke tena, you are wrong my dear.

Ungejua Waganga wa kienyeji na hao manabii uchwara wanavyowalia hela Wanawake wenzio kisa kupata ndoa hata usingesema hivyo.

Hitaji bado ni kubwa mno huko kwa ground
Ambao wapo desparate na ndoa maisha yamewapiga, hawana namna zaidi ya kuolewa ili wasitirike. Ipo hivyo kaka.
Ndo maana wanawake wengi wakiachika wanafubaa maana wao wenyewe hawana uwezo wa kujitunza.

Pia jamii imewaaminisha kwamba kuolewa ni lazima, ni mentality imejengeka akilini mwao kama ambavyo wewe imekukaa akilini mwako.

Ndoa ni hitaji la wanawake wengi lakini sio wanawake wote.
 
Mmeanzaaa!!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ww hata ukipewa hela na mwanaume hatushangai maana tunajua unaenda mpa nn hata tukuone saloon .sasa dume kabisa linalia kuwa sawa na wanawake tukimshika tako atatulia
 
Umesema sahihi, ila baada ya miaka 50 ijayo Kuoa/Kuolewa inaweza isiwe kipaumbele tena cha Vijana na likawa jambo la kawaida.
 
Kakah! andika Uzi utaolezea hii falsafa ya utibeli vizuri(Chanzo,mwanzilishi,je mtu Huwa anazaliwa nayo tu ama? Na watu wake Huwa wa aina Gani )

Japo Kuna vitu nishaviona kwenye nyuzi zako unapogusia hii falsafa ila nataka kuviona ukivichambua zaidi vikiwa katika Uzi wake maalumu.
 
Wanazo pesa zao, lakini wengi wamefeli sana kufanya unachowashauri, na waliothubutu kufanya wanatamani kurudisha siku nyuma wabadili maamuzi yao!

Mfano mzuri, nina shemeji yangu anafanya kazi nzuri tu,(shirika la kimataifa), miaka kadhaa nyuma bro ali-cheat na demu wake wa zamani huko, akapata mtoto wa nje ya ndoa! (Shem aligeuka mbogo), bro alijitahidi kumuomba radhi lakini wapi, shem alikaza kwa madai kwamba hawezi kuendelea kuishi na mume msaliti...akabeba watoto wake 2, akasepaaaa!

Kimbembe kikawa, bro anawataka watoto mke hataki kumpa kwa madai kwamba ANA UWEZO WA KUWATUNZA hivyo hahitaji chochote kutoka kwa bro.

Maisha yakasogea, bro akaanza kuishi kibachela, huko bond na watoto wake ikiendelea kudhoofika, (maana bibie alikuwa hataki kumpa ushirikiano wowote bro)

Mwaka mmoja baadaye, shemeji akaingia kwenye mahusiano na jamaa mmoja alimwambia anafanya kazi usalama wa taifa, shem ikawa full kujitanua (japo pesa ya matanuzi inaonekana shem ndo alikuwa anaitoa), mara paaaap kajamaa kake kakaenda kuoa mwanamke mwingine, shem akachanganyikiwa, anaomba kurudi kwa bro walee watoto, bro kakaza, hataki kusikia kitu inaitwa kumrudia mkewe!

Home wamemshauri mno amsamehe mkewe, jamaa alivyoona anasumbuliwa habari ya kumrudia mama watoto wake, ameenda kuoa mdada wa ki- Iraq (wambulu) mzuri kinoma, ni nesi tu, bro anaendelea kupata heshima ya "mume wangu" huku shem akiendelea na mapambano kwamba Hatambui mwanamke yeyote kuishi na mumewe,na ameshaanza kumuwinda huyo mke mwenza wake...

Sijui hatma itakuwaje, ngoja tusubiri tuone...
 
Mtibeli mpaka umuelewe lazima uwe Mtibeli. Vinginevyo leo utasema hivi kesho utasema vile.
Akiandika kinachonivutia utamsifia. Akiandika kinachokuumiza utamponda.
Wakati Watibeli huangalia jambo katika uhalisia wake(ukweli), Haki, upendo na Maarifa.
Usisahau pia kuwaambia, wake wa kiislamu, waume zao wakioa 4, na wao waolewe na wanaume 4, jino kwa jino, alaaaa!
 
Aka mkatie RB...police
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…