Wanazo pesa zao, lakini wengi wamefeli sana kufanya unachowashauri, na waliothubutu kufanya wanatamani kurudisha siku nyuma wabadili maamuzi yao!
Mfano mzuri, nina shemeji yangu anafanya kazi nzuri tu,(shirika la kimataifa), miaka kadhaa nyuma bro ali-cheat na demu wake wa zamani huko, akapata mtoto wa nje ya ndoa! (Shem aligeuka mbogo), bro alijitahidi kumuomba radhi lakini wapi, shem alikaza kwa madai kwamba hawezi kuendelea kuishi na mume msaliti...akabeba watoto wake 2, akasepaaaa!
Kimbembe kikawa, bro anawataka watoto mke hataki kumpa kwa madai kwamba ANA UWEZO WA KUWATUNZA hivyo hahitaji chochote kutoka kwa bro.
Maisha yakasogea, bro akaanza kuishi kibachela, huko bond na watoto wake ikiendelea kudhoofika, (maana bibie alikuwa hataki kumpa ushirikiano wowote bro)
Mwaka mmoja baadaye, shemeji akaingia kwenye mahusiano na jamaa mmoja alimwambia anafanya kazi usalama wa taifa, shem ikawa full kujitanua (japo pesa ya matanuzi inaonekana shem ndo alikuwa anaitoa), mara paaaap kajamaa kake kakaenda kuoa mwanamke mwingine, shem akachanganyikiwa, anaomba kurudi kwa bro walee watoto, bro kakaza, hataki kusikia kitu inaitwa kumrudia mkewe!
Home wamemshauri mno amsamehe mkewe, jamaa alivyoona anasumbuliwa habari ya kumrudia mama watoto wake, ameenda kuoa mdada wa ki- Iraq (wambulu) mzuri kinoma, ni nesi tu, bro anaendelea kupata heshima ya "mume wangu" huku shem akiendelea na mapambano kwamba Hatambui mwanamke yeyote kuishi na mumewe,na ameshaanza kumuwinda huyo mke mwenza wake...
Sijui hatma itakuwaje, ngoja tusubiri tuone...