Wadau Muna ni Binadamu si malaika,yeyote hasio na dhambi awe wa kwanza kumtupia MUNA mawe,Tumpe faraja kwa maneno mazuri,bado hajakaa sawa,amepitia mitihani mikubwa sana,tumpe moyo tusimdhihaki,kama binaadamu yeyote ana mapungufu yake lakini isiwe kigezo cha kuzidi kumtia machungu.
Ndio amepitia stage za kidunia huko nyuma ila kwa sasa ,she is born again(Kaokoka),tumpe support katika kipindi hiki kigumu,hata haya anayoongea bado akili haijakaa sawa,anahitaji faraja asahau machungu,tunapozidi kumtupia mawe tunamuongezea machungu.
Mwache atoe ya moyoni ili awe free,huenda kuna vitu vilikuwa vinamyong'onyeza labda baada ya kutoa ya moyoni kwake ni relief,tusimbeze,hata angefanya press baada ya 40,tungesema hata mwaka haujapita? Kwa yeye wiki mbili ameona sawa kutoa ya moyoni.
Ni Hayo tu.