Mungu aliamua Magufuli afe ili Tanzania ipone

ni kweli mungu aliamua makufuli afe ili tuwe na shida za maisha. maji tabu, umeme taabu, upigaji pesa za serikali wamekuwa wengi, wauza dawa za kulevya wameongezeka, vyakula bei juu, vituo feki vya mafuta vipo vingi, wafanya biashara wezi wameongezeka, kweli
mungu alitaka makufuli afe ili tupewe adhabu isiokuwa na mwisho na bado tutarudi enzi za nyerere kula unga wa njano mchungu kama shubiri
 
Hivi mawazo wakati anauawa rais alikuwa nani?

Vipi mwangosi nae yuko wapi?
Ulimboka je?
Dr. Mvungi unamjua alipo?
Vipi wale watu 6 waliouawa kwa kutupiwa bomu kwenye mkutano wa machadema pale soweto arusha alikuwa jiwe yule?

Hizi mimba alizowaachia Magu mtajifungua lini?
 
Lissu ndo kaketa mgao wa umeme na maji? Inatusaidia kwamba acheni kuua watu wenye mawazo mbadala

Kwa hiyo Maalim Seif aliuliwa na Magufuli?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Vidonda vya huyo mtakatifu wako mbona harudishi maji na umeme.
Mbona vinakata maji Dar bila huruma?
 
Nchi yenyewe badala ya kupona imeishia kupata ombwe la uongozi, watu wapo wapo kama masanamu, fedha za umma zinatumiwa hovyo hovyo utafikiri hakuna wenye jukumu la kusimamia matumzi ya hizo pesa, hovyo kabisaaaaa.
 
Endeleeni kupambana na Magufuli mitandaoni. Bahati yako tu Wanaojua umuhimu wake hawana smartphone
Watanzania jamani tumrudie Mungu. Shida na taabu zilizopo nchini sasa hivi zinaashiria adhabu kutoka kwa Mungu aliyekasirika. Ninahisi hizi hasira zinatokana na kufa kwa Magufuli. Ndio mawazo yangu na nina haki ya kuwa na hayo mawazo. Sina hakika kama kuna mtanzania aliyehusika na kifo chake ila ni kwa nini Mungu atuadhibu hivi? Ukame wa kutisha, shida ya maji, ajali mfululizo, mauaji ya kiajabuajabu, ajali ya ndege hivi kweli hamuoni watu wa Mungu? Na hata haya mashambulizi kwa Magufuli aliyezikwa kitambo yana uhusiano na watu wanaoficha uovu wao ili wasikumbuke makubwa mno sana aliyoyafanya Magufuli. Ila legacy haibomolewi kwa kampeni za.....
 
Ni kweli.. Maana ndio njia yake ya uponyaji hata Yesu ilibidi afe ili ulimwengu upone
 
ndo mkome,Mungu hataniwi
 
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana !
 
Sijawahi Cheka sio mazuri ni mabaya kifo Cha mtu ila wewe Mungu anakuona Mungu anakuona Tena huyo alikuwa mume wa mama janeth , huyo alikuwa baba na Babu wa wajukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…