Turudi katika perspective ya religion scriptures.
"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na ardhi."
At the same time, vitabu vinadai Mungu ni wa milele yani yupo siku zote hata kabla ya huo uumbaji.
Lakini Vitabu havijaeleza Mungu alikuwa eneo lipi wakati akifanya huo uumbaji.
Na hilo eneo liliumbwa na nani?
Na kama hilo eneo liliumbwa, je ni sahihi kusema mbingu na ardhi ndio uumbaji wa mwanzo?
Unaweza kutusaidia majibu ya hayo maswali?
Ndugu, unapaswa kuelewa maana ya maneno yaliyotumiwa kwenye Biblia. Mfano neno "Mbingu" kwenye Biblia lina maana zaidi ya moja na hiyo ni kutokana na tafsiri iliyofanyika kutoka original manuscripts za Agano la kale zilizoandikwa kwa Kiebrania kwenda lugha ya Kiyunani na lugha zingine.
Mbingu inamaanisha;
- anga (atmosphere)
- Mfumo wa jua (solar system)
- ulimwengu (the universe)
- Mbinguni makao ya MUNGU ( Heaven)
"Hapo mwanzo MUNGU aliumba mbingu na nchi". Sentensi hii haizungumzii "mwanzo wa MUNGU", bali inazungumzia "mwanzo wa uumbaji" wa ulimwengu.
Neno mbingu katika hiyo sentensi linamaanisha anga (atmosphere) na nchi ni dunia. Biblia katika kitabu cha Mwanzo inazungumzia mwanzo wa uumbwaji wa ulimwengu (the universe including our solar system).
Biblia haizungumzii uumbwaji wa makao ya MUNGU ambayo ni "Mbinguni" (Heaven).
Unapaswa kufahamu kuwa Mbinguni (heaven) sio sehemu ya Ulimwengu (the universe). The heaven is not part of the universe. Mbinguni ni nje ya Ulimwengu, Yes, this will suprise you, lakini ukisoma Biblia utaona kuna mahali imeandikwa; 2 Wakorintho 12:2-4
2" Namfahamu mtu aliyekuwa ndani ya Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alijikuta katika
mbingu ya tatu. Kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. 3 Na ninafahamu ya kuwa huyu mtu alijikuta yuko Paradiso, kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. 4 Naye alisikia mambo ambayo hayawezi kusimuliwa, ambayo mtu hawezi kuyatamka."
Mbingu ya tatu ni ipi?
Kama kuna "mbingu ya Tatu" basi ni dhahiri kuwa ipo mbingu ya kwanza na ya pili.
Mbingu ya kwanza ni "anga" au atmosphere.
Mbingu ya pili ni "ulimwengu" au the universe with all its galaxies, planets, stars, comets, asteroids, moons etc.
Mbingu ya tatu ndio "Mbinguni" makao ya MUNGU au heaven.
Mbingu ya tatu iko mbali sana na mbingu ya kwanza na ya pili. Kwa kifupi "Mbingu ya tatu" sio sehemu ya ulimwengu huu (the universe).
Biblia haisemi Mbingu ya tatu iliumbwa lini. Biblia inatuambia kuna mambo ni siri, siri hiyo anaijua MUNGU mwenyewe na kuna mambo ameyafanya kuwa siri mpaka atakapoamua kuyaweka hadharani Yeye mwenyewe.
Soma Kumbukumbu la Torati 29:29
"Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii".
"Yaliyofunuliwa" ndiyo hayo yote yaliyoandikwa kwenye vitabu vya Biblia. Ambayo hayajaandikwa kama ni lini "Mbingu ya tatu" iliumbwa au MUNGU alikuwa anaishi wapi kabla ya kuumba makao yake, hayo yote ni SIRI.
Na MUNGU amefanya kuwa siri sababu hata kama angetufunulia bado yasingetusaidia lolote.
Yale yenyewe ambayo MUNGU aliona yanafaa tuyajue ili yatusaidie KUMTII na kuishi kama apendavyo, ametufunulia, yameandikwa, ametufundisha, lakini tumeshindwa kuyashika. Tunahangaika kutafuta yale yasiyokuwa na faida kwetu.
Tumeshindwa kuzishika Amri za MUNGU, tunahangaika kutafuta SIRI za MUNGU.
Mafarisayo walipomuuliza BWANA YESU KRISTO awaonyeshe ishara itokayo Mbinguni, alisema hivi;
"Kizazi
kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.