Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Kama kitu sidai kipo ila wewe ndiye unayedai kipo, Uta takaje mimi ni kuthibitishie madai yako?

Ukisema kitu kipo unatakiwa wewe ndio uthibitishe kipo, Kama huwezi kuthibitisha kipo ni kwamba kitu hicho hakipo.
Na wewe ukishindwa thibitisha hakipo maana yake kipo
 
Unajuaje mawazo yanaendesha dunia? Mawazo ya nani?

Dunia inavyozunguka jua mawazo ndiyo yanaifanya izunguke jua?
Nimegundua uelewa wako ni mdogo sana. Unapenda kubishana bila kujua unataka nini
 
Vizuri,..Kwahiyo kwa kutumia time na space kama ulivyosema,..Je, Dunia ilikuepo milele?
Ndio ilikuwepo milele.
Na,Je kwa wakati uliopita wakipima watagundua Infropreneur ulikuepo milele au kuna wakati hukuwepo?
Kwa wakati uliopita Sikuwepo ndani ya Dunia ambayo yenyewe ipo milele ndani ya time na space.

Maana bila dunia yenye time na space huwezi fanya vipimo vya kitu chochote kile kujua kama kilikuwepo au hakikuwepo.

Yaani wewe ulikuepo milele au kuna wakati hukuepo?
Mimi Sikuwepo.

Ila time na space ambavyo vipo ndani ya dunia vilikuwepo milele.
 
Ni uelewa mdogo tulionao, Mungu yupo na ni muweza wa kila kitu, Mungu sio fundi, ni Muumba.
Je, jiulize una akili, na ipo wapi ipoje nainawezeje kufanya majambo?! Kama ipo, hujaiona basi Mungu yupo. Kama hakuna basi Mungu Hayupo.

Kuna watu tunawaita wavumbuzi(innovator) au fathers of, hawa wamepata wapi hayo yasiyokuwepo na ramani yake. Mungu anaumba sio anatengeneza.

Kuumba kitu ni hakipo hata mali ghafi zake,Mungu anaziumba na kuumba hicho kiiumbe au umbo, mfano mwanadamu, miti nk.. Fundi au Wabunifu huwa malighafi zipo mfano leo wataalam hasa wa afya duniani wameshindwa kuunda cells km vile seli nyekundu au nyeupe, mpaka wawachangishe watu kwa ajili ya kupata damu, si hivyo tu vipo vingi wameshindwa zaidi ya elfu.

Nina mengi ila nachoka kuandika kaka.

 
 
Post majina ya members wa JF kama sipo itaonekana
Upo JF ndio maana una uthibitisho kwamba upo na unaweza kujitetea mwenyewe upo

Sasa wewe unahangaika kumuongelea Mungu ambaye hawezi na hajawahi kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Huoni kwamba una mtetea na kumuongelea Mungu Mdhaifu ambaye hayupo na Kashindwa kuja kujiongelea mwenyewe na kujitetea?
 
Hebu niletee Nijifunze Kitu Kipya Boss
Surah Al-Baqarah (2:117):

"The Originator of the heavens and the earth. When He decrees a matter, He only says to it, 'Be,' and it is."


Surah Az-Zumar (39:62):

"Allah is the Creator of all things, and He is, over all things, Disposer of affairs".


So., hapo unaona wazi kwamba sio tu dunia, bali Mungu ndiye Originator wa kila kitu yaani Dunia na Ulimwengu kwa ujumla.

Ahsante na karibu kwa mtazamo tofauti.
 
Dunia haina umri.

Dunia ipo milele.

Umri ni kwa vitu vilivyo ndani ya dunia.
Sawa vizuri,..Kwahiyo kuna wakati ndani ya Dunia kulikua hakuna kitu kabisa?

Maana umesema vitu vilivyo ndani ya dunia ndiyo vina umri.
 
Sasa huu ni uthibitisho au maandiko uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule?

Mtu akitaka kuhakikisha haya maandiko ya Quran uliyo andika hapa ni ukweli ata hakikishaje?

Mnahangaika sana kumuongelea huyo Allah kwa kutumia maandiko uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule.

Huyo Allah aje hapa mwenyewe ajiongelee yeye kama yeye kwamba ndio originator wa huu ulimwengu.

Mbona huyo Allah hajawahi kujiongelea mwenyewe wala kujidhihirisha mwenyewe kwamba yeye ndiye originator wa ulimwengu?

Huoni kwamba unafosi mawazo yenu na maandiko yenu uchwara kutaka kumuongelea Allah ambaye Kashindwa na hawezi kujiongelea mwenyewe?
 
Hakuna ajuaye.

Kila mtu kazaliwa ndani ya dunia kwa wakati wake.

Ndio kila kilichowahi kuishi duniani kina umri wake.
Kama hujui kwanini ulisema Dunia haina umri ila vilivyopo ndani yake ndiyo vina umri?

Ukishasema vitu vilivyopo ndani ya dunia vina umri fulani maana yake kuna starting point ya umri husika.. kwa maana kwamba kuna wakati havikuepo.... umeelewa?
 
Sasa nani kakuambia huo ni uthibitisho?

Niliyemjibu alisema kwenye scriptures hakuna sehemu inayoonyesha Mungu kaumba Ulimwengu kwa ujumla,.. Mimi ndiyo nikaweka hapo kumuonyesha kwamba Scriptures zimeonyesha jambo hilo,....sasa wewe ume panic bila kujua kwanini nimeweka hizo verses hapo,..

Relax mzee 🤝🏼
 
Kama hujui kwanini ulisema Dunia haina umri ila vilivyopo ndani yake ndiyo vina umri?
Hakuna uthibitisho wowote ule unao thibitisha umri wa Dunia.

Hivyo kusema dunia ina umri ni madai tu yasiyo na uthibitisho.
Ukishasema vitu vilivyopo ndani ya dunia vina umri fulani maana yake kuna starting point ya umri husika.. kwa maana kwamba kuna wakati havikuepo.... umeelewa?
Kama kila kitu lazima kiwe na starting point mbona huyo Mungu mna mu exclude kuwa na starting point?

Kama Mungu hahitaji kuwa na starting point, kwa nini unalazimisha dunia iwe na starting point?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…