Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

okay vizuri,..mwanzo ulisema Dunia haina umri ila vilivyopo ndani ya dunia ndiyo vina umri.........Sasa nina swali 'Umethibitisha vipi kama Vililivyopo ndani ya Dunia sasa hivi kuna wakati havikuwepo, mpaka ukasema vina umri??
Kuna vitu vya asili ambavyo vimekuwepo milele na havina umri mfano ardhi, maji, anga, hewa, jua, mwezi, nyota n.k Hivi vitu ni sehemu ya dunia ambavyo vipo milele na havina umri.

Pia kuna vitu vingine vya asili vyenye umri kama wanyama, binadamu mimea, wadudu n.k ambavyo vimekuwepo milele lakini vyenyewe hupungua na kufa kadiri ya muda unavyokwenda.

Lakini huzalisha vitu vipya copy and paste ya muundo wao uleule na kuendeleza mzunguko wa kuwepo vitu hivi duniani milele.

Pia kuna vitu vingine vina umri ambavyo ni "Man-made" mfano magari, nyumba, meli, simu, ndege, kompyuta, viti, meza n.k

Vitu hivi humtegemea binadamu Avitengeneze ndipo viongezeke. Vitu hivi haviwezi kujiongeza idadi vyenyewe tu, pasipo kutengenezwa na binadamu.
ili tuone kama una consistency kwenye kujenga hoja zako......
 
Pia kuna vitu vingine vya asili vyenye umri kama wanyama, binadamu mimea, wadudu n.k ambavyo vimekuwepo milele lakini vyenyewe hupungua na kufa kadiri ya muda unavyokwenda.

Lakini huzalisha vitu vipya copy and paste ya muundo wao uleule na kuendeleza mzunguko wa kuwepo vitu hivi duniani milele.
Vizuri,. kwahiyo Kila Mnyama, Binadamu,. mimea, wadudu n.k wote wana umri?

Na, kama jibu ni "NDIYO"..unakubali kwamba kila chenye umri (wanyama, binadamu mimea, wadudu n.k) means kuna wakati hakikuwepo?

Na, kama wanyama, binadamu mimea, wadudu n.k kuna kipindi hawakuwepo Je,.ilikuaje wakawepo mpaka kuanza kwa hiyo system ya kujizalisha kwa Copy & paste?
 
Vizuri,. kwahiyo Kila Mnyama, Binadamu,. mimea, wadudu n.k wote wana umri?
Ndio.
Na, kama jibu ni "NDIYO"..unakubali kwamba kila chenye umri (wanyama, binadamu mimea, wadudu n.k) means kuna wakati hakikuwepo?
Ndio.

Lakini kila kitu kina mtangulizi wake, Going backward in time to infinity.
Na, kama wanyama, binadamu mimea, wadudu n.k kuna kipindi hawakuwepo Je,.ilikuaje wakawepo mpaka kuanza kwa hiyo system ya kujizalisha kwa Copy & paste?
Kila kitu wanyama, binadamu, mimea, wadudu n.k Kina mtangulizi wake ambaye amekuwepo kabla yake.

Kwa sababu Time imekuwepo, ipo na itaendelea kuwepo milele.
 
Yeap,. nimesoma hizo nadharia lakini nikahusisha na akili ili kufikia hitimisho..........yaani sijahitimisha kwamba kila nilichosoma ndiyo uhalisia ulivyo 100%.

Kwanini unaona haiwezekani kwa Sayari na nyota zote kuwa kwenye anga la dunia? ukubwa wa hizo sayari hakuzifanyi sayari na makundi hayo ya nyota kuwa nje ya anga la dunia bali tunaweza tu kusema kwamba kuna sayari na nyota ambazo zipo anga la karibu na anga la mbali la Dunia. yaani kuna ambazo unaweza kuona hata kwa macho na nyingine kwa msaada ya vifaa saidizi kulingana na umbali.
Unajua Nyota Ina ukubwa gani Mkuu?

Au unadhani ni kama unavyoiona??
Nyota iliyo karibu na Dunia Ni Jua na ndo n8 kubwa kuliko Dunia Mara Sita sasa unasema kuna nyota zipo karibu na Dunia.?
 
Unajua Nyota Ina ukubwa gani Mkuu?

Au unadhani ni kama unavyoiona??
Nyota iliyo karibu na Dunia Ni Jua na ndo n8 kubwa kuliko Dunia Mara Sita sasa unasema kuna nyota zipo karibu na Dunia.?
Hizo ni nadharia na estimations tu mkuu,.. hakuna mtu anaejua exactly nyota zina ukubwa gani.

So, kusema Jua ni kubwa mara sita kwa Dunia still ni debatable na upo free kuamini hivyo.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi ni kwamba ulisema Mungu hajasema kama Kaumba ulimwengu mzima,...Mimi nikakupa Verse inayoonyesha kwamba YEYE NI MUUMBA WA KILA KITU.....
So,. nadhani hilo neno kila kitu linajumuisha nyota ndogo na kubwa.,, na vyote tuvionavyo na tusivyoviona..............Kama sijakosea.
 
Kutaka kujua mfano kautoa wapi huko ni mbali unajikomaza.

Unachotakika kujua hilo neno au Concept "MFANO" yeye ndio aliliumba na kuliwekea huo utaratibu ambao wewe Leo unauzungumia hapa.

Angeamua Concept ya MFANO isiwepo pia wala usingekua hata na Idea kwamba kuna kitu kinaitwa kugelezea mfano.

IN SHORT: MUNGU NI YUPO VERY COMPLEX UNAFOSI KUMJUA KWA SIMPLE INTELLIGENCE AMBAZO AMEKUWEKEA YEYE MWENYEWE.

NISAWA NA MFUMO MZIMA WA INTERNET UNAOSHIKILIA MAELFU YA WEBS, APPS, SAAS, SOFTWARES then itokee kama Web kamoja kama Jamiiforums kianze kuhoji HOW INTERNET INA WORK LIKE BUTTONS ZAKE ZIKO WAPI, INA SEHEMU YA KUSHEA UZI....kwamba JF inajiuliza maswali kuhusu Internet kwa uwelewa wake wa kujijua yeye JF alive hatojua iyo Internet inauwezo wa kutuma pesa na kupokea wala haiwezi jua hio pesa nini nini.

Uelewa tulionao ni sawa na hako kaduara kadogo hapo ambao uwelewa wenyewe umejifunga kujua yaliyo ndani ya hako Kaduara, unachofanya unataka kutumia uwelewa huo mdogo tena uliojufunga kujua kitu ambacho kikubwa kuliko huo mduara mkubwa hapo lazima uwe CONFUSED.
View attachment 3028026
Nimekuelewa boss
 
M
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
M/Mungu ni mbunifu namba Moja. Hana haja ya kuona kitu sehemu halafu akaiga au kuboresha. Kila kitu kilichopo, kisichoonekana na kinachoonekana yeye ndiye katengeneza kwa alivyoona inafaa.
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Kuumbwa kwa mbingu na ardhi Qur an inasema "Bila shaka katika hayo zimo ishara kwa watu wenye kufikiri".

Nawapa pole sana binaadamu wa humu Jf na wengineo wanaopinga uwepo wa Mungu

Cc. Kosugi
The Icebreaker
adriz
 
Ndiyo maana sijaamua kulenga wasio amini Mungu kama wewe.
Ningeamua kuwa lengo wote ningekuja na thread hapa "Mungu hayupo au yupo" na wewe ungepata side ya kusimama na uthibitisho wako.

Nakushauri tu : Kuingiza logic and reasoning kwenye mambo ya imani/kiroho/yasiyoonekana kimwili lazima utoke mtupu.

Ndiyo wewe hapo.
Sjui kwanini unatumia nguvu kujibu hoja zake
"To trick a fool is to let them think they tricked you"
And stay calm
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Kwa uelewa wangu,ingekua haya maswali unajiuliza kumhusu binadamu ingekua sawa,lakini unayemzungumzia hapa ndiye aliyekupa maarifa uliyonayo ,Mungu ni kamili na ukamili wake hauna mipaka,
Si kama binadamu
 
Nikiwa mdogo nilikua najiuliza backwards yaani kabla ya Mungu kuumba binadamu alikua yeye na yeye aliwekwa na nani!!?nikifika mwisho naona kiza kama naishiwa nguvu hivi basi na switch ghafula to Basics!
 
Nafikiri hilo ni swali simple sana kuliko la yeye alitokea wapi ?
 
Usimuhukumu
Unaposema MUNGU aliona wapi mfano wa dunia ndipo akaumba, hivi unamfananisha BWANA MUNGU na Mwanadamu?

Umekosa akili, umekosa adabu kwa MUUMBA wako kiasi unaona hawezi kufanya chochote mpaka kwanza awe ameona?

Na kama mpaka aone kwanza, unataka kusema yupo mwingine aliye mkuu kumzidi YEYE?

Kijana kuwa na adabu kwa MUUMBA wako. Usifikie hatua ya kumdharau MUNGU kuwa hawezi kutenda, hawezi kuumba mpaka awe ameona kwanza.
Usimuhukumu Kwa mgando wake wa mawazo ndo mwsho wake wa kuwaza
 
Kasema kaumbs mtu kwa mfano wake, sasa aliumba kioo kwanza akajitazama akawa anaigilizia au ilikuwaje
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Mtoa mada unaamini kwamba, si kila kitu kinachoundwa ni lazima kiwe kimeangaliwa sample yake mahali fulani? Kitu kinaweza kuundwa kwa ubunifu moja kwa moja?
 
Back
Top Bottom