Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Nasubiri majibu ya maswali yangu. Kisha tuendelee na hili.
 
Kijana naona unaendeleza tabia yako ya kukimbia maswali. Swali nililo anza nalo ni kuwa wapi Yesu alisema yeye ni mwana wa mungu au yeye ni Mungu.

Mkanukuu andiko toka kwa Luka, nikawataka mthibitishe huyo Luka amewahi kumuona Yesu kama hajamuona hayo maneno ameyapata wapi.

Kisha turudi huku.
 
Kama Mna muita nabii issa lakini mnasema hajafaaa mtu gani wa kawaida gani asiyekufa huyo, Yesu ni njia na kweli na uzima
 
Imeandikwa wapi kwamba Yesu siyo Mungu?
Usinishike kwa maana sijapaa kwenda kwa baba,baba yangu ambaye baba yenu,mungu wangu ambaye mungu wenu.....haya niyafanyayo si kwa uwezo wangu Bali yeye aliyenituma
 
Wewe ndio umesema Ndugu yangu kwamna Mungu kazaa. Sasa Yanakuwaje tena maneno yangu

Kama Alizaa kwa Neno Mariam alihusikaje sasa. Si angetamka au kumuumna Yesu kwa Udongo kama Alivyofanya Kwa Adam

Kuna swala ambalo inabidi uelewe.
Wewe unamjua Yesu baada ya kuzaliwa na maria lakini Yesu alikuwepo kabla ya maria. Yeye ndio MWANZO. Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana. Ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
 
Huwezi. Niambie kwamba nabii issa tokea kipindi kile Cha mitume yeye hajafaaa tu Kuna ,halafu eti atarudi Kuna Siri hapo,kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri ya kwamba Yesu Kristo ni mwana wa Mungu it matter of time tu
 
Mungu anateswaa kwa ajili yetu sasa anateswa na Nani na yeye ndio Mungu [emoji28][emoji1787][emoji1787] hapa tulipigwa na kitu kizito
halafu anakuja kutuhukumuu mamaweeeh
Umepewa tahadhari.
Roho asema wazi wazi siku za baadaye watu wengine watatii roho danganyifu nakufuata mafundisho ya pepo
Timotheo4°
 
Ungekua unamjua Yesu usingeuliza hilo swali
Rudi nyuma kasome comments utanielewa

YESU NI MUNGU
Kumbukeni nilivyowambia nitakwenda na nitarudi, kama kweli mnanipenda mngefurahi na kushangilia maana nakwenda kwa baba: na baba yangu ni mkuu kuliko mimi°
Yesu anasema Mungu ni Mkuu kuliko yeye.
 
Acha kupoteza muda kujadili story za Abunwasi. Huyo Yesu hakuwahi kuwepo. Vyanzo vyote huru (visivyofungamana na dini) vya kihustoria vimeonesha wazi hakuna ushahidi wa kushikika wa huyo wanayemuita Yesu na hao wanafunzi wake kuwahi kuwepo hapa duniani.

Kuna wakati tuache kutangliza kuamini (Imani) badala ya kutanguliza kuelewa (Ukweli).
 
Kumbukeni nilivyowambia nitakwenda na nitarudi, kama kweli mnanipenda mngefurahi na kushangilia maana nakwenda kwa baba: na baba yangu ni mkuu kuliko mimi°
Yesu anasema Mungu ni Mkuu kuliko yeye.

Soma kwa kuelewa

Yohana 14:2-10
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.

Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.
 
Kwani nyie hamtendi dhambi?!
Kijana kutoka suala la kumuamini yesu na kutenda dhambi yameingiaje hapa?

m nimekwambia I am a Muslim

jaribu kutafuta swali linaloendana kidogo
 
Sikutumwa Ila kwa kondoo waliopotea wa israeli
Hhhhhhhh kwaio katumwa kwa kondoo tena wa israel tuu sasa hawa kondoo wa nchi nyingine wanamfuata ili iweje? inachekesha kweli yani
 
Sema wakristo wengi hatusomi biblia kikamilifu, matokeo ni kupwaya pale zinapoibuka hoja kinzani kama hizi, unakuta swali moja linaleta majibu 40, na hayajitoshelezi. Tusomeni Biblia na kuielewa vyema wakuu.
Yesu amesoma biblia au alishushiwa injili?
 
Yesu alikufa kwa sababu ya dhambi zetu, kifo chake kilithibitisha kuwa mwanadamu anaweza kudumisha ushikamanifu na Mungu.
Aisee kila mtu atabeba mzigo.wake msijidanganye kabisaaa ety kafa kwa ajili.ya dhambi zetu
Yni uue,uzini,uibe hlf useme kuna mtu kashanitubia dhambi zangu its non sense

Sasa mbona mnaenda makanisani ili msamehewe dhambi zenu? Na ubaya zaidi ety Pastor au Padri ndie anaesamehe dhambi wakati yy hpo anamichepuko kibao

kusema ukweli wakristo jitafakarini bhna mumeingizwa chaka na iyo imani yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…