Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Hawaogopi. Anawapenda wanadamu
Kumbuka aliiitengeza Dunia kwa lengo tu amuumbe mwanadam aje aishi hu

Mbona hujiulizi kwa Nini Shetani anamng'ang'ania mwanadamu amkoseshe asitende mapenzi ya Mungu Kuna Nini humo?

Ngoja nikuambie Shetani ana wivu sana na mwanadamu kwa sababu Mwanadamu anasanehewa dhambi. Shetani hasamehewi dhambi kwa hiyo anataka aende jehanam na wanadamu wengi sana
So anapofusha fikra zao wasielewe mpango wa Mungu waendelee kucheza na dhambi mwisho wake jehanam mile
Kumbuka mshahara wa dhambi ni mauti Bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
 
Tungekua tunatafuta kuujua ukweli kabla ya kubisha tusiyoyajua tungekua na amani sana
Na tungekua tunaujua mpango wa Mungu ni kwa kila aliyemuumba na yeye ni wa wote tusingejidai kumbinafsisha
Jibu hoja izo m sina shida ila kwanini mseme mshabebewa dhambi zenu hlf mnaenda makanisani kutubu?
 
Ubaguzi uko wapi? unajua uko nyuma tumejibizana vipi au unasema tuu

Mungu sio mbaguzi na wapi mm nimefanya ubaguzi? au kudhihirisha imani yangu ndo nimefanya ubaguzi?
 
Watu wengi humu haulizi maswali kwa maana ya kutaka kujifunza wasichokijua bali kwa mtazamo wa kutaka kuchallenge.
Imagine wewe ni mwanafunzi/mwanachuo umeenda darasani kwa lengo tu la kutaka kuchallenge mwalimu/lecturer wako HAKUNA namna utakaa uelewa somo lake. Utabakia vile ulivyo.

Wewe ni mwanadamu tena u mavumbi tuu kisha unataka kuyachallenge mambo ya Mungu (divinity) kabla ya kumwamini, HAKUNA namna utakaa uyaelewe pasipo kumwamini kwanza. Utabakia na ujinga wako huku ukijiona mwerevu mbele zake.

Kaa chini uwe tayari kujifunza.
 
lete andiko kua Mungu alikua anazungumza na binadamu moja kwa moja
 

Mt 11:25-26 SUV​

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.
 
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu. Yesu alisoma torati iliyoandikwa na manabii kama Isaya, kwa hiyo jibu kwa swali lako ni NDIYO
Sasa huo mkusanyiko uyo Yesu wenu hakuusoma alishushiwa injili tu na Mungu wake

hlf kaangalie kwenye iyo biblia yako Maana ya hekalu hlf utanambia uyo Yesu alikua anaswali wapi na nyinyi mnaswali wapi
 
Mungu alitaka kuwa mtu wa familia, basi Mungu akasema kama mtu mwenye familia lazima familia yangu inifahamu lakini kama Mungu hivi nilivyo hawawezi kunijua. Kwa sababu katika namna yangu kama Mungu mimi ni Nuru isiyoweza kufikiwa na mwanadamu mwenye mwili wa kufa.

Kwa hiyo Mungu aliketi na Mungu akatoka nje ya Mungu na Mungu akamtazama Mungu. Mungu akasema na Mungu. Wewe nenda! Mimi nasubiri hapa.

"Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, hata niwaweke adui zako kuwa chini ya miguu yako?" Mathayo 22:44 [Zab. 110:1.]

Mungu alikuwa akiongea na yeye mwenyewe. Basi Mungu mwingine akaingia katika tumbo la mwanamke (Bikira Maria).

Kuzaliwa kwa Yesu mara ya kwanza hakukuwa kuzaliwa kihalisi kwa maana halisi ya kuzaliwa bali kudhihirishwa.

16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu: *Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na malaika,
Akahubiriwa katika mataifa,
Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.
1 Timotheo 3:16

Mungu alidhihirishwa haina maana ya kuzaliwa kama "kuzaliwa" bali kudhahirishwa.

Kwa hiyo kuzaliwa kwa Yesu mara ya kwanza ilikuwa ni KUONEKANA KWA MUNGU KWA MARA YA KWANZA KATIKA UMBO LA BINADAMU.

Karibu katika familia ya Mungu. Unakuwa mtoto wa Mungu na Mungu anakuwa Baba yako. Kuamini katika kazi kamilifu ya Yesu Kristo ni kupata haki yako halisi ya uzaliwa sio kuasiliwa.

Duniani na mbinguni hushangilia wewe kuwa mwana wa Mungu. Mungu akiishi ndani yako milele.

Nakutakia Kujifunza kwema
 
Hahahahah unafurahisha sana kwamba mtoto wa pekee angetakiwa kuwa Adam. Soma maandiko ndugu uyaelewe na siyo kuja na majibu yako kichwani.

Kwanj Majibu yako ndugu unayatoa Wapi. Maana Kama Huwezi Shirikisha Ubongo wako sahau kuja Kujua Yaliyojificha Kwenye Maandiko hayo unayoyatoa na Kuyaamini sana. Mmepotoshwa Ndio maana hamuwezi Kujua Ukweli ulipo mnakomaa kuomba Maandiko

Kama Yesu ndio mwanae wa Pekee Adam si Alikuwa Binadamu pia na Yesu si Mwanadamu aliyekuwa Hapa Duniani leo hii huo Upekee wa Yesu unakuwaje Ni mkubwa Kuliko upekee wa Adam!?

Yaani wewe uzae Watoto Halafu mtoto wa Pekee aje kuwa Mwanao wa Mwisho. Utakuwa na Akili timamu kweli





Yesu ndio mwana pekee wa Mungu. Yesu ndio MWANZO. Amekuwepo kabla ya Adam na nikupe siri moja ambayo huijui,
Yesu alishiriki uumbaji wa Adam

Hakuna Siri inayowekwa Kwenye Kitabu Kilichosambaa Dunia Nzima. Na Ukisema Siri maana Yake Ni Kitu kilichofichwa ukishakijiua siyo Siri hiyo.

Yesu awezi kuwa Mwana na Hapo hapo Akawa Tena Mungu muumbaji . Yaani ni Sawa na Wewe kujiita Mwana wa Fulani halafu Ukataka Tena Uwe Baba. Huwezi kuitwa Mwana da costa halafu hapo hapo wakakuita Da costa

Tutumieni Akili kuchambua Mnayoletewa
 
Bwana eeh.. mi siku izi nimeacha kuhangaika na haya mambo. Kama mungu aliniumba ili aje anichome moto mwishoni hiyo ni juu yake maana tunaambiwa yeye anatujua kabla hatujazaliwa na pia anajua mwenyewe alipopanga kutupeleka baada ya maisha haya... 😐
 

Wewe ndio unasema kwamba kuzaa ni sifa ya kiumbe ila maandiko yanasema Mungu anazaa.
Waebrania : 1 : 5 - Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

Maandiko hayo hapo Mungu anazaa. Lete andiko katika biblia Mungu anasema hazai tujue mbivu na mbichi leo
 
Jamani nyieeee Mungu hazaliwi nyie
Walokuleteeni iyo dini saivi wanaslimu kwa kasi huko
 
vizuri sana
Enheeee yesu kazaliwa na nani?

Waebrania : 1 : 5 - Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?
 
Yesu katika Mahubiri yake haymjawahi Kuzungumza Haya mnayoyasema. Mwandishi wa Hicho kitabu Hata Hakuwa Mwanafunzi wake wala Kuwahi kuwa Karibu yake.

Leo hii anakuandikia hayo unayaamini. Yaani ni sawa na Mzungu kutoka ulaya Aje Tanzania akusimulie Historia ya Wangoni.
 
Wewe jibu kwanza swali langu kisha uniulize kuhusu Mtume, ili uone tofauti yangu na yako iko wapi.
 
Waebrania : 1 : 5 - Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?
hujanitajia alomzaa ila m ninavojua alimzaa ni Mariam kwaio Mariam ndo Mungu wa Yesu?
 

Mungu hazai ukimpa Hiyo Sifa Basi Baba Yako na Mama Yako Pia Ni Mungu si Wanazaa bhana. Nyie kila Siku mnaimba Hafafani na Yeyote ila Mnampa Sifa Ya Kuzaa Mungu akishazaa Basi Hana Tofauti na Wewe NA wanyama Wengine wanaozaa pia.

Unakimbilia Maandiko yako wakati Hata Huko hakuna Andiko linalosema Mungu kazaa[/QUOTE]

Mada imeisha
Mungu anazaa na ana mwanawe anaitwa Yesu Kristo
Kwa taarifa yako
BILA YESU MBINGUNI HUTOBOI
 
Kuna Utata mkubwa Sana Katika kuzaliwa kwa Yesu kutokana Na Maandiko ya Biblia. Ila Kwa Akili Timamu Binadamu yeyote lazima Azaliwe kwa Mifumo maalumu ya Mbegu ya Kiume kuungana Na Mbegu ya Kike Tofauti na Hapo Binadamu hawezi Kutokea
kwa hiyo kuna uwezekano kuna siri imefichwa?
 
Kuna watu humu jf wanajua kila kitu, Sasa umkute jumapili kwa baba paroko kashika mikono tumboni utadhani ndo papa yohana wa pili. Utashangaa kama ni yeye wa jf.
kwa ground mambo ni tofauti aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…