Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mada imeisha
 
Sasa ikiwa mnaona ni vibaya kumtumikia Yehova chagueni leo yule mtakaemtumia, iwe ni miungu ambayo mababu zenu waliabudu ngaΒ°ambo ya mto. Yoshua 24:15

HULAZIMISHWI KUMWAMINI YEHOVA, CHAGUA MUNGU UTAKAE ONA ANA KUFAA.
Wewe utakuwa Mashahidi wa Yehova ndugu yangu. Nimerudi huku juu kwa Maana Moja Tu

Kama Kweli Mungu ni Mmoja Basi Hata Nyie Mngekuwa Wamoja. Wakatoliki.. Waislamu.. Wasabato.. Wa Anglicana.. n.k lakini Mmetenganishwa Kwa Sababu Dini hizi si Za Mungu Bali Ni Dini Za Viumbe Wasio Mungu ila Ni wenye Kutaka Kutawala

Ndio maana Utakuta wameandika hivi
1. Mungu kakaa
2. Mungu kasema
3. Mungu kaketi kwenye Kiti
4. Mungu kazungukwa na Malaika
5. Mungu kazungukwa na Makerubi
6. Mungu analindwa na Malaika na Makerubi
7..Mungu wa majeshi

Hizo zote ni Sifa za Viumbe wanaotawala Hata Sisi hapa Duniani Wanadamu tuna Sifa Hizo
 
Duu, kwa mfano jina kikwete. Kuna jakaya, je jakaya akiitwa kikwete ni kosa? Hilo jina si ni la kurithi?
Vivyo hivyo Yesu karithi Jina la baba yake ndiposa anaitwa Mungu.
Kurithi Jina Haimanishi wewe ndio Mungu. Sijui kama Tunaelewna Hapa Ndugu yangu. Huwezi ukawa Mungu kisa Wewe unaitwa Mungu. Kuna Watu hapa Duniani wanaitwa Jesus Hata Mchezaji wa Yanga anaitwa Hivyo Jesus Moloko. Ila Si Jesus aliyepo kwenye Biblia mnayomsema.
View attachment 2139406
Kwahiyo Usimwite Yesu Mungu ukimaanisha Mungu mwenye Vyote ingawa kwenye Utatu mnaousema Wewe utaonekana Unapingana nao maana Wenyewe unamsema Yesu ni Mungu sawa na Baba
 
Mkuu, ni simple logic tu, mungu hayupo kwa sababu hajawahi kuonekana, simple. Wewe kwenye maisha yako umewahi kumuona Mungu? Unaweza kutupatia picha anafananaje?

Kama hujawahi basi hadithi za Mungu ni za kutunga tu na wala hazina maana yoyote.
Ndio maana nikakuuliza una uhakika gani kuwa hayupo? Maana unaposema hajawahi kuonekana nitakuuliza ni wapi huko ambako unakusudia kuwa hajawahi kuonekana ni hapa duniani au hata huko panapodaiwa kuwa ndio yupo?

Usijipe majibu mepesi kwenye maswali magumu utakuwa huna tofauti na waumini wa dini tu, wewe kutoamini Mungu hilo ni jambo moja ila ukija hapa na kutuambia kabisa kuwa Mungu hayupo basi itabidi utupe maelezo ya kina kuhusu hayo madai yako.
 
Ni muujiza upi huo wa mungu ambao alifunuliwa huyo binaadamu wa kwanza hebu elezea huo muujiza ili nikuelewe.

Suala la kuomba nishakwambia sio issue ya msingi hapa kwa sababu hata hao wazee wako wanaweza kuwa walikuwa wanajibiwa maombi na hao hao mashetani au kuna alama inayoonesha kuwa utofauti wa majibu ya maombi?
 
Tuna Mungu mmoja aliye baba na ana mwanawe wa Pekee anaitwa Yesu.
Nikuulize mwanao akitumia jina lako ni kosa?
sasa Mwanangu akitumia jina langu anakua Mimi ?
Mimi nabaki kua Mimi na Yeye anabaki ku Yeye .

kwa hio Yesu ni Mungu mwenzake na Baba yake ?

halafu Yesu ni Mwana wa Mungu wa kumzaa au ni Mwana wa Mungu k'vipi ?
 
Daughter of Mutah , Allah kakairi alimtengeneza ISSA bandia alafu wewe unambishia

Nimeshamaliza kazi wewe endeleza mutah
 
sasa Mwanangu akitumia jina langu anakua Mimi ?
Mimi nabaki kua Mimi na Yeye anabaki ku Yeye .

kwa hio Yesu ni Mungu mwenzake na Baba yake ?

halafu Yesu ni Mwana wa Mungu wa kumzaa au ni Mwana wa Mungu k'vipi ?

Mwanao akitumia jina lako anakuwa ameririthi kutoka kwako ndio ilivyo kwa Yesu. Karithi jina la Baba yake yaani Mungu.

Yesu ni mwana wa Mungu wa kumzaa.
 
Mungu hamjazi mimba mtu kama binadamu afanyavyo, na ana watoto wengi tu.
Naam, sisi wote ni watoto wa Mungu kwa kutuumba.

Biblia inasema (ya Kiingereza inasema) "Begotten", hiyo ni kazi ya kibinaadam au wanyama.
 
Ukija kwa ustaarab utakutana na ustaarabu hujapatapo kuuona, ujkija kwa ku beep, napiga, kumbuka hilo.

1) Manabii na Mitume sio washirika wa Mungu. Unaelewa Nabii ni nani na Mtume ni nani, na mshirika ni nani? Au unajiongelea tu?

Uliza swali moja moja tulijadili kwa kina, sio unajaza maswali chungu nzima, una haraka ya nini?
 
Ni muujiza upi huo wa mungu ambao alifunuliwa huyo binaadamu wa kwanza hebu elezea huo muujiza ili nikuelewe.

Muujiza Huo huo Ulioumba

Suala la kuomba nishakwambia sio issue ya msingi hapa kwa sababu hata hao wazee wako wanaweza kuwa walikuwa wanajibiwa maombi na hao hao mashetani au kuna alama inayoonesha kuwa utofauti wa majibu ya maombi?

Kikubwa hapa Ni Sala. Maana Ukisema Wanajibiwa na MASHETANI ni kuweka Sala. Halafu unaichambua Sala Hiyo uone kama Wanaomba kwa Mashetani au Laaah.

Kumbuka Mitume na manabii hawakuacha Sala Yeyote jinsi gani walivyokuwa wanaomba kwa Mungu
 
Ukija kwa ustaarab utakutana na ustaarabu hujapatapo kuuona, ujkija kwa ku beep, napiga, kumbuka hilo.

1) Manabii na Mitume sio washirika wa Mungu. Unaelewa Nabii ni nani na Mtume ni nani, na mshirika ni nani? Au unajiongelea tu?

Neno Mshirika limetokana na Neno Kushirikiana. Sasa Ikiwa Mungu anamtuma Mtume kumfanyia Kazi maana Yake Yeye Mungu kashirikiana na Huyo Mtume. Kumtuma Malaika maana Yake Malaika anashirikiana na Mungu

Ndio maana ya Neno MSHIRIKINA huyu ni Mtu au Kiumbe kinachofanya mambo yake kwa Kushirikiana na kiumbe kingine. Mchawi akishirikiana na Mchawi mwingine ndio Wanaitw Washirikina

Uliza swali moja moja tulijadili kwa kina, sio unajaza maswali chungu nzima, una haraka ya nini?

Tumeanza Na Hilo.
 
Muujiza huo huo uliyoumba ndio nini sasa mbona unakuwa kama hauna uhakika na unachokieleza unakuwa muoga? wewe eleza ueleweke kuhusu huo muujiza maana hapo ndio mzizi wa tunachojadili hapa.

Hapo tutaishia kubishana tu ndio maana nimekwambia nitajie alama ambayo inatenganisha aina ya majibu ya maombi, ukisema kwa sababu huyu anaomba vile ndio anamuomba shetani na mwengine ataona jinsi unavyoomba wewe ndio unamuomba shetani.
 
Muujiza huo huo uliyoumba ndio nini sasa mbona unakuwa kama hauna uhakika na unachokieleza unakuwa muoga? wewe eleza ueleweke kuhusu huo muujiza maana hapo ndio mzizi wa tunachojadili hapa.

Twende Taratibu tu Ndugu yangu Kwanza Unatakiwa Kuelewa Kwamba Binadamu wa Kwanza Kuumbwa ni Fumbakasa na Mwasi mkewe. Hawa Ndio waliokuwa wa Kwanza Kulingana na Elimu ya Jadi na Wazee. Hawa ndio Waliopewa Elimu ya Kuishi na Wao Kurithisha Elimu hiyo kwa Watoto wao Ndio mpaka Leo hii Elimu hiyo Ipo na Ndio inayofundishwa Elimu hii walipata Kutoka Katika Muujiza Wa Mungu ambao ndio huo Unaoumba Mpaka leo

Hapo tutaishia kubishana tu ndio maana nimekwambia nitajie alama ambayo inatenganisha aina ya majibu ya maombi, ukisema kwa sababu huyu anaomba vile ndio anamuomba shetani na mwengine ataona jinsi unavyoomba wewe ndio unamuomba shetani.

Ubishi unaletwa Kama Mtu mmoja Kati Yetu Atang'angania Jambo analojua Hata Kama Hana Ukweli sahihi wa Ki Mungu.

Sasa Angalia Kwamba Maombi unayoyanajibuwa kwa Wewe kufanya Nini.

1. Watakuambua Peleka Sadaka
2. Huko Nyuma Watu walikuwa wanachinja Wanyama na ndege ambapo ni Sadaka za Damu
3. Usipopeleka Hivyo Vitu Hao Viumbe hukasirika na Kukuletea Mabalaa

Sasa Ili Ujibiwe lazima Huyo unayemuomba Akuombe Wewe kitu kwanza Na Ukimnyima Anakasirika. Sasa Ndugu yangu kwa Akili ya Kawaida Mungu anakuomba Wewe hivyo vitu Ili Yeye afanyie Nini. Hivyo vitu ni Viumbe wasio Mungu ndio wanataka Mfano Wewe mwenyewe Binadamu na Hayo Majini na Malaika ndio Hupenda Hivyo vitu
 
Nilianza kicheka kabla kuusoma Uzi huu..

Binadamu ametunikiwa kitu kikubwa Sana na Mungu lkn shetani atamtesa mno MTU huyu
 
Nilianza kicheka kabla kuusoma Uzi huu..

Binadamu ametunikiwa kitu kikubwa Sana na Mungu lkn shetani atamtesa mno MTU huyu
Kwani Mungu yeye Ndugu yangu anakuogopa Nini wewe mpaka akutolee Sadaka. Maana Kulingana Na Biblia Ww ndio mkosaji. Na Kumbuka Wale wa Sodoma na Gomora walichomwa Moto fasta tu walipomkosea na Wale wa Gharika hivyo hivyo. Ila Wewe ukamsababisha Amtoe Mwanae Badala ya Wewe ndio Ungetakiwa Kumchomwa Moto au Kuangamizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…