Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Source ya Mambo haya Ni Elimu ya Jadi na Masimulizi ya Wazee wetu na Kitabu cha Wazee kilichoandikwa na Wacha Mungu.

Na Pia naweza Kukuambia Hili kama Nyongeza . Hudi na Mkewe wa Kwanza Jemi. Ndio waliotambulika kama Adam na Hawa. Adam ndie Hudi na Hawaii ambaye ndie Jemi. Waliitwa Hivyo Walipokuwa Wamekimbilia irak ambayi ndio Iraq [emoji1131] kwa Sasa. Na ukifuatilia kwa Makini utaambiwa na Wanahistoria Bustani ya Edeni ilikuwa Iraq

Mada imeisha
 
Sasa ikiwa mnaona ni vibaya kumtumikia Yehova chagueni leo yule mtakaemtumia, iwe ni miungu ambayo mababu zenu waliabudu nga°ambo ya mto. Yoshua 24:15

HULAZIMISHWI KUMWAMINI YEHOVA, CHAGUA MUNGU UTAKAE ONA ANA KUFAA.
Wewe utakuwa Mashahidi wa Yehova ndugu yangu. Nimerudi huku juu kwa Maana Moja Tu

Kama Kweli Mungu ni Mmoja Basi Hata Nyie Mngekuwa Wamoja. Wakatoliki.. Waislamu.. Wasabato.. Wa Anglicana.. n.k lakini Mmetenganishwa Kwa Sababu Dini hizi si Za Mungu Bali Ni Dini Za Viumbe Wasio Mungu ila Ni wenye Kutaka Kutawala

Ndio maana Utakuta wameandika hivi
1. Mungu kakaa
2. Mungu kasema
3. Mungu kaketi kwenye Kiti
4. Mungu kazungukwa na Malaika
5. Mungu kazungukwa na Makerubi
6. Mungu analindwa na Malaika na Makerubi
7..Mungu wa majeshi

Hizo zote ni Sifa za Viumbe wanaotawala Hata Sisi hapa Duniani Wanadamu tuna Sifa Hizo
 
Duu, kwa mfano jina kikwete. Kuna jakaya, je jakaya akiitwa kikwete ni kosa? Hilo jina si ni la kurithi?
Vivyo hivyo Yesu karithi Jina la baba yake ndiposa anaitwa Mungu.
Kurithi Jina Haimanishi wewe ndio Mungu. Sijui kama Tunaelewna Hapa Ndugu yangu. Huwezi ukawa Mungu kisa Wewe unaitwa Mungu. Kuna Watu hapa Duniani wanaitwa Jesus Hata Mchezaji wa Yanga anaitwa Hivyo Jesus Moloko. Ila Si Jesus aliyepo kwenye Biblia mnayomsema.
View attachment 2139406
Kwahiyo Usimwite Yesu Mungu ukimaanisha Mungu mwenye Vyote ingawa kwenye Utatu mnaousema Wewe utaonekana Unapingana nao maana Wenyewe unamsema Yesu ni Mungu sawa na Baba
 
Mkuu, ni simple logic tu, mungu hayupo kwa sababu hajawahi kuonekana, simple. Wewe kwenye maisha yako umewahi kumuona Mungu? Unaweza kutupatia picha anafananaje?

Kama hujawahi basi hadithi za Mungu ni za kutunga tu na wala hazina maana yoyote.
Ndio maana nikakuuliza una uhakika gani kuwa hayupo? Maana unaposema hajawahi kuonekana nitakuuliza ni wapi huko ambako unakusudia kuwa hajawahi kuonekana ni hapa duniani au hata huko panapodaiwa kuwa ndio yupo?

Usijipe majibu mepesi kwenye maswali magumu utakuwa huna tofauti na waumini wa dini tu, wewe kutoamini Mungu hilo ni jambo moja ila ukija hapa na kutuambia kabisa kuwa Mungu hayupo basi itabidi utupe maelezo ya kina kuhusu hayo madai yako.
 
Swali Zuri Wewe umejua Uwepo wa Huyo Mungu wa Israeli au Mumgu yeyote yule kupitia Masimulizi ya Waandishi wa kwenye Biblia. Ndugu yangu Huwezi Kusema Unamjua Mungu Kama Hujaambiwa au Kusimuliwa labda Kama Ww mwenye Ulikuwepo Mwanzo wa Ulimwengu. Kama Hukuwepo jua Kwamba Uliambiwa tu na Kusoma Sehemu hakuna Njia nyingine ya Kujua Kuwa Yupo.

Wazee wetu Walipata Haya Na Mpaka leo yametunzwa Kwa Njia hiyo hiyo. Mwanadamu wa Kwanza Aliweza kufunuliwa haya Kwa Njia Ya Muujiza wa Mungu si Mungu mwenyewe. Muujiza huu ndio uliweza Kuumba Dunia na Ulimwengu uliopo Leo hii na Kumuumba Huyo Mwanadamu na Mkewe.

Hii ni Elimu iliyokuwepo Mwanzoni na Ilitunzwa Afrika kabla Ya Viumbe wengine Kuja majini na Malaika waovu na Kuleta Neno Dini Duniani

Sidhani kama Nimezungumza Jambo la Kusema Kwamba Kufanikiwa ni lazima Uombe. Sina Maana Hiyo na Wala Siamnini Hivyo kamwe. Washenzi wanafaulu kwenye Mambo yao.. Malaya wanafaulu kwenye mambo yao.. Majini wanafaulu kwenye Mambo yao,malaika wana faulu kwenye Mambo yao pia.

Watu wanaoomba Bila Kujua Ukweli wanafaulu tu baadhi ya Mambo kufanikiwa ni jambo jingine maana Hata shetani huwapa Tuzo wanaomheshimu, malaika huwapa Tuzo wanaowaomba.. MAJINI huwapata Tuzo wanaowaheshimu na Kuwafuga miilini mwao

Wazee wako na Mababu zako waliomba kwa Mungu mwenye Vyote si Hao miungu wengine . (ndicho nilichokuwa namaanisha). Hizi Dini zilizoletwa sasa Hivi jua kwamba Kuna Kiumbe amezisimamia Ndio maana Ukiomba anakupa Ila Tu Kama Akifurahi na Usipompa Baadhi ya Vitu kama Sadaka.. Zaka..Shukrani wanachukia.

Ndio Ujue hili Ndugu yangu. Mungu Hakuombi Chochote kile umpelekee Ndio akubariki yeye Si Kiumbe haitaji Kitu kutoka Kwako maana Yeye nj Mkamilifu si Dhaifu kama Wewe ulivyo. Ukiona Sehemu unaombwa Kitu Jua Kwamba unampa Si Mungu mwenye Vyote ila Ni Kiumbe cha Mungu chenye Tamaa

Sadaka.. Zaka.. Shukrani hivi Vitu Mungu wa Kweli Havihitaji maana Havimsaidiee kwa Chochote kile ila Wanaotaka Hivi vitu ni Viumbe kama wewe na Mimi
Ni muujiza upi huo wa mungu ambao alifunuliwa huyo binaadamu wa kwanza hebu elezea huo muujiza ili nikuelewe.

Suala la kuomba nishakwambia sio issue ya msingi hapa kwa sababu hata hao wazee wako wanaweza kuwa walikuwa wanajibiwa maombi na hao hao mashetani au kuna alama inayoonesha kuwa utofauti wa majibu ya maombi?
 
Tuna Mungu mmoja aliye baba na ana mwanawe wa Pekee anaitwa Yesu.
Nikuulize mwanao akitumia jina lako ni kosa?
sasa Mwanangu akitumia jina langu anakua Mimi ?
Mimi nabaki kua Mimi na Yeye anabaki ku Yeye .

kwa hio Yesu ni Mungu mwenzake na Baba yake ?

halafu Yesu ni Mwana wa Mungu wa kumzaa au ni Mwana wa Mungu k'vipi ?
 
Vipi kijana wa "Shikamoo Baba"? Ushamjua yupi mmoja wao?

Hakuna aliyefananisha wala kufananishiwa. Mnachosoma wewe na hao majuha wenzako hamkielewi. Sasa wewe unaamini maigizo ya Mzungu kutindikwa kwenye msalaba? Fikiri kijana, kama si maigizo na mafananisho hayo ni nini?
Daughter of Mutah , Allah kakairi alimtengeneza ISSA bandia alafu wewe unambishia

Nimeshamaliza kazi wewe endeleza mutah
 
sasa Mwanangu akitumia jina langu anakua Mimi ?
Mimi nabaki kua Mimi na Yeye anabaki ku Yeye .

kwa hio Yesu ni Mungu mwenzake na Baba yake ?

halafu Yesu ni Mwana wa Mungu wa kumzaa au ni Mwana wa Mungu k'vipi ?

Mwanao akitumia jina lako anakuwa ameririthi kutoka kwako ndio ilivyo kwa Yesu. Karithi jina la Baba yake yaani Mungu.

Yesu ni mwana wa Mungu wa kumzaa.
 
Mungu hamjazi mimba mtu kama binadamu afanyavyo, na ana watoto wengi tu.
Naam, sisi wote ni watoto wa Mungu kwa kutuumba.

Biblia inasema (ya Kiingereza inasema) "Begotten", hiyo ni kazi ya kibinaadam au wanyama.
 
Naona Umerudi kunijibu kwa Ustaarabu ndugu. Mimi nina maswali haya

1. Mungu ambaye ni mmoja na Hana Washirika inakuwaje Anakuwa na Manabii na Mitume

2. Je wewe unayoyafanya Haya Katika Uislamu ndivyo mtume Muhammed amekuelekeza! Yeye ndie aliyekuwa anasali hivyo kwa Mungu wake(kutawadha, kuchinja wanyama n.k n.k)

3. Kama Mungu ni Mmoja Kwanini wewe na Wakristo mnasali tofauti.!?
Ukija kwa ustaarab utakutana na ustaarabu hujapatapo kuuona, ujkija kwa ku beep, napiga, kumbuka hilo.

1) Manabii na Mitume sio washirika wa Mungu. Unaelewa Nabii ni nani na Mtume ni nani, na mshirika ni nani? Au unajiongelea tu?

Uliza swali moja moja tulijadili kwa kina, sio unajaza maswali chungu nzima, una haraka ya nini?
 
Ni muujiza upi huo wa mungu ambao alifunuliwa huyo binaadamu wa kwanza hebu elezea huo muujiza ili nikuelewe.

Muujiza Huo huo Ulioumba

Suala la kuomba nishakwambia sio issue ya msingi hapa kwa sababu hata hao wazee wako wanaweza kuwa walikuwa wanajibiwa maombi na hao hao mashetani au kuna alama inayoonesha kuwa utofauti wa majibu ya maombi?

Kikubwa hapa Ni Sala. Maana Ukisema Wanajibiwa na MASHETANI ni kuweka Sala. Halafu unaichambua Sala Hiyo uone kama Wanaomba kwa Mashetani au Laaah.

Kumbuka Mitume na manabii hawakuacha Sala Yeyote jinsi gani walivyokuwa wanaomba kwa Mungu
 
Ukija kwa ustaarab utakutana na ustaarabu hujapatapo kuuona, ujkija kwa ku beep, napiga, kumbuka hilo.

1) Manabii na Mitume sio washirika wa Mungu. Unaelewa Nabii ni nani na Mtume ni nani, na mshirika ni nani? Au unajiongelea tu?

Neno Mshirika limetokana na Neno Kushirikiana. Sasa Ikiwa Mungu anamtuma Mtume kumfanyia Kazi maana Yake Yeye Mungu kashirikiana na Huyo Mtume. Kumtuma Malaika maana Yake Malaika anashirikiana na Mungu

Ndio maana ya Neno MSHIRIKINA huyu ni Mtu au Kiumbe kinachofanya mambo yake kwa Kushirikiana na kiumbe kingine. Mchawi akishirikiana na Mchawi mwingine ndio Wanaitw Washirikina

Uliza swali moja moja tulijadili kwa kina, sio unajaza maswali chungu nzima, una haraka ya nini?

Tumeanza Na Hilo.
 
Muujiza Huo huo Ulioumba

Kikubwa hapa Ni Sala. Maana Ukisema Wanajibiwa na MASHETANI ni kuweka Sala. Halafu unaichambua Sala Hiyo uone kama Wanaomba kwa Mashetani au Laaah.

Kumbuka Mitume na manabii hawakuacha Sala Yeyote jinsi gani walivyokuwa wanaomba kwa Mungu
Muujiza huo huo uliyoumba ndio nini sasa mbona unakuwa kama hauna uhakika na unachokieleza unakuwa muoga? wewe eleza ueleweke kuhusu huo muujiza maana hapo ndio mzizi wa tunachojadili hapa.

Hapo tutaishia kubishana tu ndio maana nimekwambia nitajie alama ambayo inatenganisha aina ya majibu ya maombi, ukisema kwa sababu huyu anaomba vile ndio anamuomba shetani na mwengine ataona jinsi unavyoomba wewe ndio unamuomba shetani.
 
Muujiza huo huo uliyoumba ndio nini sasa mbona unakuwa kama hauna uhakika na unachokieleza unakuwa muoga? wewe eleza ueleweke kuhusu huo muujiza maana hapo ndio mzizi wa tunachojadili hapa.

Twende Taratibu tu Ndugu yangu Kwanza Unatakiwa Kuelewa Kwamba Binadamu wa Kwanza Kuumbwa ni Fumbakasa na Mwasi mkewe. Hawa Ndio waliokuwa wa Kwanza Kulingana na Elimu ya Jadi na Wazee. Hawa ndio Waliopewa Elimu ya Kuishi na Wao Kurithisha Elimu hiyo kwa Watoto wao Ndio mpaka Leo hii Elimu hiyo Ipo na Ndio inayofundishwa Elimu hii walipata Kutoka Katika Muujiza Wa Mungu ambao ndio huo Unaoumba Mpaka leo

Hapo tutaishia kubishana tu ndio maana nimekwambia nitajie alama ambayo inatenganisha aina ya majibu ya maombi, ukisema kwa sababu huyu anaomba vile ndio anamuomba shetani na mwengine ataona jinsi unavyoomba wewe ndio unamuomba shetani.

Ubishi unaletwa Kama Mtu mmoja Kati Yetu Atang'angania Jambo analojua Hata Kama Hana Ukweli sahihi wa Ki Mungu.

Sasa Angalia Kwamba Maombi unayoyanajibuwa kwa Wewe kufanya Nini.

1. Watakuambua Peleka Sadaka
2. Huko Nyuma Watu walikuwa wanachinja Wanyama na ndege ambapo ni Sadaka za Damu
3. Usipopeleka Hivyo Vitu Hao Viumbe hukasirika na Kukuletea Mabalaa

Sasa Ili Ujibiwe lazima Huyo unayemuomba Akuombe Wewe kitu kwanza Na Ukimnyima Anakasirika. Sasa Ndugu yangu kwa Akili ya Kawaida Mungu anakuomba Wewe hivyo vitu Ili Yeye afanyie Nini. Hivyo vitu ni Viumbe wasio Mungu ndio wanataka Mfano Wewe mwenyewe Binadamu na Hayo Majini na Malaika ndio Hupenda Hivyo vitu
 
Nilianza kicheka kabla kuusoma Uzi huu..

Binadamu ametunikiwa kitu kikubwa Sana na Mungu lkn shetani atamtesa mno MTU huyu
 
Nilianza kicheka kabla kuusoma Uzi huu..

Binadamu ametunikiwa kitu kikubwa Sana na Mungu lkn shetani atamtesa mno MTU huyu
Kwani Mungu yeye Ndugu yangu anakuogopa Nini wewe mpaka akutolee Sadaka. Maana Kulingana Na Biblia Ww ndio mkosaji. Na Kumbuka Wale wa Sodoma na Gomora walichomwa Moto fasta tu walipomkosea na Wale wa Gharika hivyo hivyo. Ila Wewe ukamsababisha Amtoe Mwanae Badala ya Wewe ndio Ungetakiwa Kumchomwa Moto au Kuangamizwa
 
Back
Top Bottom