Mungu anipe nguvu ya kupuuzia mambo ili kuokoa afya yangu

Maleven

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2019
Posts
689
Reaction score
3,373
Najiona kwenda kuangukia kwenye ugonjwa wa moyo kutokana na changamoto za huyu mwanamke. Nimekosea sana kupuuzia baadhi ya mambo kipindi cha uchumba nikidhan atabadilika.

  • Anamatumizi mabaya ya hela.
  • mvivu
  • anakiburi
  • ukimuelekeza anaona anaonewa
Kuna muda hadi nawaza huenda uwezo wake wa akili ni mdogo sana. Mana jinsi anavyojaji vitu ni shida tupu.
Nakili nimekosea sana.
 
Nawafahamu wanawake wa aina hiyo. Wanajidai wanajua kumbe wakati kichwani ni weupe. Na anaweza kukuabisha mbele za watu kwa kuongea upuuzi huku akiwa na confidence.

--- Ni shida. Ila jaribu kumpuuza tu. Mind your own business.
 
Ndugu yangu......

Uvumilivu uliokusudiwa kwenye maisha ya ndoa ni yale mapungufu ya kibinadamu ambayo kila kiumbe hakijakamilika nayo kama sehemu ya maumbile nayo....na sio mambo ya makusudi yanayofanywa na mtu ili akukere.......

Kuvumilia mambo ya makusudi ambayo mtu anapaswa kuyaacha muishi kwa amani sio uvumilivu bali ni UPUMBAVU......

NDOA ni ya wawili kwa maana kila mmoja anatakiwa kuonyesha uhitaji kwa mwenzake ili zidumu jitihada na kufurahia muunganiko huo......

NDOA sio jela useme unatumikia kifungo bali ni muunganiko wa wawili wapendanao walioamua kuishi pamoja ili kufurahia kilichopo mioyoni mwao.......

Ukiona anayetakiwa kukupa tabasamu na furaha maishani mwako badala yake anakupa majuto, maumivu na vilio.....huna budi kuondoka mahali hapo pasi na kujiuliza mara mbili mbili.......kwani masononeko ya nafsi na majonzi yasiyo na ukomo ni dalili za ufupi wa maisha......kwani kicheko na furaha ya moyo hurefusha maisha

Yeye ambaye haikumfaa akili yake, basi utamdhuru ujinga wake........
 
 
  • Anamatumizi mabaya ya hela.
  • mvivu
  • anakiburi
  • ukimuelekeza anaona anaonewa😒😒😒
 
Pole muelekeze Kwa upole
 
Duh hasa hapo kwenye matumizi ya pesa nunua vitu vya ndani vyote wewe mpe hela kidogo sana otherwise hamtaendelea
 
Nawafahamu wanawake wa aina hiyo. Wanajidai wanajua kumbe wakati kichwani ni weupe. Na anaweza kukuabisha mbele za watu kwa kuongea upuuzi huku akiwa na confidence.

--- Ni shida. Ila jaribu kumpuuza tu. Mind your own business.
'Own business' ni pamoja na huyo mkewe na vyote vinavyomzunguka.
 
Saaaafi kabisa ushauri mzuri mtaalam
 
Kumwacha sio suluuhu,hata wa kwangu yupo hivyo ,Kuna muda atabadilika ,mzalishe watoto watatu kwanza ,utaona anaanza kuacha tabia za kipuuzi na kuwa mama.
 
Vyote hivyo alikuwa navyo lakini kwa kuwa ana tako ukasema ntavumilia.
 
Ukweli mtupu
Asee pole,Mimi red light zilianza mapema,kwao kwenda hataki,Sasa tuna watoto 3,tabia ndo Kama hizo,Sasa nashughulika na wanangu tu,na sijali.

Nakushauri,kama hujazaa naye mwache tembea mbele.

Nina mpango wa kuhama kimyakimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…