Mungu anipe nguvu ya kupuuzia mambo ili kuokoa afya yangu

Mungu anipe nguvu ya kupuuzia mambo ili kuokoa afya yangu

Najiona kwenda kuangukia kwenye ugonjwa wa moyo kutokana na changamoto za huyu mwanamke. Nimekosea sana kupuuzia baadhi ya mambo kipindi cha uchumba nikidhan atabadilika.

  • Anamatumizi mabaya ya hela.
  • mvivu
  • anakiburi
  • ukimuelekeza anaona anaonewa
Kuna muda hadi nawaza huenda uwezo wake wa akili ni mdogo sana. Mana jinsi anavyojaji vitu ni shida tupu.
Nakili nimekosea sana.
Jipende wewe kwanza usimfuatilie utakufa bure uache watoto.
 
S

Sasa kwa nini usimpe talaka arudi kwao?,nawe utafute mwengine?
Au ndio upo kwenye ile dini,kunywa pombe ila hautakiwi ulewe.
Maaana huko hakuna kuachaa nasikia😄
Unavyosema hakuna kuachana una maanisha nini?
Kwamba ukisepa zako kuna mtu atakulazimisha urudi?. Kuachana na mtu ni maamuzi tu
 
Ndugu yangu......

Uvumilivu uliokusudiwa kwenye maisha ya ndoa ni yale mapungufu ya kibinadamu ambayo kila kiumbe hakijakamilika nayo kama sehemu ya maumbile nayo....na sio mambo ya makusudi yanayofanywa na mtu ili akukere.......

Kuvumilia mambo ya makusudi ambayo mtu anapaswa kuyaacha muishi kwa amani sio uvumilivu bali ni UPUMBAVU......

NDOA ni ya wawili kwa maana kila mmoja anatakiwa kuonyesha uhitaji kwa mwenzake ili zidumu jitihada na kufurahia muunganiko huo......

NDOA sio jela useme unatumikia kifungo bali ni muunganiko wa wawili wapendanao walioamua kuishi pamoja ili kufurahia kilichopo mioyoni mwao.......

Ukiona anayetakiwa kukupa tabasamu na furaha maishani mwako badala yake anakupa majuto, maumivu na vilio.....huna budi kuondoka mahali hapo pasi na kujiuliza mara mbili mbili.......kwani masononeko ya nafsi na majonzi yasiyo na ukomo ni dalili za ufupi wa maisha......kwani kicheko na furaha ya moyo hurefusha maisha

Yeye ambaye haikumfaa akili yake, basi utamdhuru ujinga wake........
Well said....
 
Unavyosema hakuna kuachana una maanisha nini?
Kwamba ukisepa zako kuna mtu atakulazimisha urudi?. Kuachana na mtu ni maamuzi tu
Ivo yaan ...hakuna pingamizi...ni wewe tu uamue kukaa
 
Back
Top Bottom