Mungu hafichi ukweli: Mama Samia leo umejionea ubovu wa askari wetu wa Jeshi la Polisi

Mungu hafichi ukweli: Mama Samia leo umejionea ubovu wa askari wetu wa Jeshi la Polisi

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
4,555
Reaction score
6,773
Mapema September mwaka 2020 wakati wa kampeni za uchaguzi mama yetu alisema askari akikosa risasi tatu anafukuzwa kazi.

Natoa pole kwa ndugu na jamaaa na watanzania kwa askari wawili waliopoteza maisha leo pale Kinondoni. Pili nimeshangaa kuona mtu mmoja alivyohangaishana na askari eneo la wazi kama lile hadi kupelekea baadhi ya askari wetu kupoteza maisha. Ingekuwa mtu yule kawashtukiza askari ningekubali lakini kwa hali ya leo naingiwa mashaka.


Inakuwaje askari kupiga marisasi mengi vile huku wanakosa target? Ni silaha duni walizo nazo au uwezo wao? Wengi tutakuwa tumeona moja ya kipande cha video mtu mmoja akimkaribia yule mhalifu lakini askari wa kupatia cover hawakuwa tayari.

Anaonekana anawapa ishara kwa mkono lakini imechukua muda hadi kapigwa. Yaani mhalifu kanyanyuka mafichoni na kufyatua risasi kadhaa huku hakuna risasi ya polisi inaonekana kumpata.

Huu ni udhaifu mkubwa sana na kamanda Sirro anapaswa ajitafakari mbinu wanazotumia kupambana na uhalifu wa namna hii.

Mwisho namkumbusha mheshimiwa kuwa askari wetu wana uwezo mkubwa sana wa kukosea shabaha wala asiwakweze kwa uwezo wasio nao.
 
Samia wakati anagombea urais alikebehi tukio la Lissu kupigwa risasi 36 akasema police wao (soma polisiccm) hawawezi piga mtu risasi 36 asife. Akifanya hivyo kazi hana.

Leo kiko wapi? Polisi wao (soma polisiccm) wametumia risasi zisizo na idadi na bado wameuwawa. Malipo ni hapa hapa
 
Samia wakati anagombea urais alikebehi tukio la Lissu kupigwa risasi 36 akasema police wao (soma polisiccm) hawawezi piga mtu risasi 36 asife. Akaifanya hivyo kazi hana.

Leo kiko wapi? Polisi wao (soma polisiccm) wametumia risasi zizsizo na idadi na bado wameuwawa. Malipo ni hapa hapa
Uzi ufungwe..umeutendea haki.
 
Mapema september mwaka 2020 wakati wa campeni za uchaguzi mama yetu alisema askari akikosa risasi tatu anafukuzwa kazi.

Natoa pole kwa ndugu na jamaaa na watanzania kwa askari wawili waliopoteza maisha leo pale kinondoni. Pili nimeshangaa kuona mtu mmoja alivyohangaishana na askari eneo la wazi kama lile hadi kupelekea baadhi ya askari wetu kupoteza maisha. Ingekua mtu yule kawashtukiza askari ningekubali lakini kwa hali ya leo naingiwa mashaka.

Inakuwaje askari kupiga marisasi mengi vile huku wanakosa target? Ni silaha duni walizo nazo au uwezo wao? Wengi tutakua tumeona moja ya kipande cha video mtu mmoja akimkaribia yule mhalifu lakini askari wa kupatia cover hawakuwa tayari. Anaonekana anawapa ishara kwa mkono lakini imechukua muda hadi kapigwa. Yaani mhalifu kanyanyuka mafichoni na kufyatua risasi kadhaa huku hakuna risasi ya polisi inaonekana kumpata.
Huu ni udhaifu mkubwa sana na kamanda Siro anapaswa ajitafakari mbinu wanazotumia kupambana na uhalifu wa namna hii.
Mwisho namkumbusha mheshimiwa kuwa askari wetu wana uwezo mkubwa sana wa kukusea shabaha wala asiwakweze kwa uwezo wasio nao.
Polisi hawajui kulenga shabaha ni hatari sana anyway walikuwa wanamtishia tu hawakutaka kuuwa nadhani Teh tehh.
 
Uaskari polisi ni kazi ambayo kwakweli ina changamoto sana,hakika na JWTZ wangepewa kazi wanazozifanya polisi,tungeyang'amua mapungufu yao na yawezekana tungewachukia sana.Uzuri wa JWTZ,unaweza ukastaafu haujakutana na mikikimikiki na sifa kadha wa kadha zukawa zinakumiminikia kutoka Kwa raia,ambao maranyingi wanajua askari wa jeshi la polisi analipwa mshahara duni na hana mafunzo,bali askari wengine mishahara yao ni mikubwa na wanajaliwa.
 
Amani tuliyonayo ndo sababu ya kuwa na watu kama wewe Yani unahisi kila jambo linawezekana simple tu kama life style yako ilivyo simple.

Matukio kama haya yanatokea hata kwa nchi zilizoendelea, mfano mdogo tu ni yule Rais wa ufaransa aliyepigwa na raia, unazani lile eneo halikuwa na ulinzi?
 
Amani tuliyonayo ndo sababu ya kuwa na watu kama wewe Yani unahisi kila jambo linawezekana simple tu kama life style yako ilivyo simple.

Matukio kama haya yanatokea hata kwa nchi zilizoendelea, mfano mdogo tu ni yule Rais wa ufaransa aliyepigwa na raia, unazani lile eneo halikuwa na ulinzi?
Unaelewa tofauti ya usalama na amani?
 
Back
Top Bottom