kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Internet - Money, what is wrong with you? I said they get money freely without sweat! God doesn't want your money! You feed their stomachs!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni sadaka impendezayo Mwenyezi MunguKuna sehemu umesema Mchungaji au paroko anaweza kuwa Kama dalali Kati yako na Mungu.
Inawezekana vipi Mchungaji akawa karibu zaidi na Mungu kuliko ww? Kwamba ana usafi wa kimwili kukuzidi? Ama ana ushawishi Zaidi mbele ya Mungu?
Sadaka au Dhaka tunazozitoa mm huchukulia kuwa ni michango ya uendeshaji wa Sehemu tunayoabudia. Na kiasi kidogo ni kwaajili ya viongozi wa dini.
Mara nyingi sadaka yangu huitoa kwa watu Baki ninaokutana nao njiani ama niwanunulie chakula, au niwawezeshe kifedha kutokana na Hali halisi niliyoiona na namna nilivyoguswa.
Mungu wangu haitaji mtu wa tatu kuniombeaKwenda Kwa mchungaji au Nabii haimaanishi kuwa wewe unashindwa kuongea na Mungu moja Kwa moja. Ila ni utaratibu tuu wa ki-protocol ambao miungu mingi iliweka, makuhani, manabii, mitume waliwekwa/wameweka kama daraja baina ya Watu na miungu Yao.
Miungu mingi haiwezi kuongea na kila MTU. Hivyo inachagua MTU mmoja wa kuwawakilisha Watu.
Hiyo ni Kanuni ya kiutawala na Kiongozi.
Kuhusu sadaka umeelezea Vizuri.
Kuhusu ishu ya Pesa za kuendeshea mambo ya ibada pia umeelezea vyema.
Tatizo ni pale Uongo unaposemwa kuwa ukitoa Zaka au sadaka unamtolea Mungu Jambo ambalo ni Uongo Mkubwa.
Kingine kama kabisa au msikiti haukusaidii lolote kwenye Maisha haina haja wala ulazima wa kwenda kujumuika Huko(ambalo wengi husema wanaenda kufanya ibada)
Maisha ndio ibada
Mungu wangu haitaji mtu wa tatu kuniombea
Najiombea mwenyewe na ananijibu
Huu ni ushauri wa Bwana wetu Yesu Kristo
Mathayo 6:5-6
Tena msalipo,msiwe kama wanafiki, kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia,ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, wamekwishapata thawabu yao.
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Uhakika nilio nao ni kwamba Bwana wangu Yesu Kristo anamjua Mungu vizuri kuliko hawa wachungaji na mapadri
Kwa hiyo nafuata ushauri wa Bwana wangu Yesu Kristo maishani mwangu
Uko sahihi, kulingana na fundisho rasmi la kanisa langu, baraka na neema za Mungu hazina sharti, ni "gratuitous"MUNGU HAHITAJI ZAKA NA SADAKA YAKO, SADAKA NA ZAKA NI MALIPO YA WATUMISHI WA DINI.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
"Mtolee Mungu"
" Hiyo ni sadaka Kwa Mungu wako"
" Unamnyima Mpaka Mungu anayekupa uhai"
Na kauli zingine kama hizo, ni Utapeli mtupu.
Kuna Ile unaambiwa" mtolee Mungu ili akubariki" huo ni Uchawi na ushirikina mkubwa. Kwamba ati unampa Mungu rushwa kama Samunge, labda Ile miungu ya Kwa msisi.
Mungu hahitaji chochote Kutoka Kwako, endapo Mungu huyo atahitaji chochote Kutoka Kwako basi anapoteza vigezo vya kuwa Mungu. Kwa sababu moja ya Sifa ya Mungu ni kuwa sio mhitaji.
Sadaka au Zaka ni MALIPO tunayowalipa viongozi wa dini tunazoabudia ili waweze kuendesha Maisha Yao kama Sisi tunavyofanya kazi katika shughuli zetu.
Viongozi wa dini wanafamilia zao, wanamahitaji Yao, wanahitaji vyakula, nguo, nyumba, magari na mahitaji mengine
Ukienda Kanisani, au msikitini au madhabahuni popote pale, lazima uingie makubaliano na huyo kuhani au mchungaji, au nabii au Mtume kwamba kwako ninakuja Kwa ajili ya Kupata mambo 1,2,3.
Mfano, unakuja Kwa Kuhani Taikon, unaniambia, Kuhani Taikon wa Mungu wa Tibeli, Mungu Mkuu, nimekuja kwako Kwa sababu zifuatazo;
1. Nataka uniombee nipone ugonjwa Fulani,
2. Nataka Njia zangu na kazi za mikono yangu ifanikiwe, nataka ndani ya miaka Hii Mitano niwe ninanyumba au Gari.
3. Nataka ulinzi katika familia yangu.
Hapo nitaingia chumba cha Siri kumuuliza Mungu wa Tibeli kama atakusaidia au Laa. Kama akisema atakusaidia, nitakujia nitakuambia Mungu wa Tibeli kasema atakusaidia, kisha nitakuambia nenda alafu Mungu atakapokusaidia ndio ulete malipo(sadaka) ya Kazi niliyokufanyia ya kuwa Dalali baina yako na Mungu wa Tibeli.
Nitakupa sheria na masharti ya kufuata kadiri nitakavyoagizwa na huyo Mungu wa Tibeli.
Mfano nitakuambia Mungu atakujibu ndani ya mwaka mmoja, atakapokujibu utaleta Sehemu ya ishirini ya Mapato yako ndani ya miaka mitatu.
Kisha utaondoka, utaamua kutoa shukrani au usitoe ni wewe mwenyewe, kwani hapo ulikuja kufanya agano/mkataba na Mungu wa Tibeli. Haukuja kutoa Sadaka wala Zaka wala dhabihu.
Sio nikuombe Sadaka na Zaka Wakati hakuna kazi niliyoifanya, huo ni Utapeli.
Kufumba macho na kuanza kuomba hiyo sio kazi. Hiyo kila MTU anaweza Kufanya, hata mtoto Mdogo anaweza kufumba macho akaomba.
Mchungaji au nabii anayetanguliza umlipe Kabla ya Kazi huyo ni Mhuni, tapeli.
Manabii na mitume wakweli anakupa Huduma kisha wewe mwenyewe utaamua uvunja makubaliano au uwe mwaminifu. Hii ni Kwa sababu, kama wanauwezo wa kukupa Mali au kukusaidia basi ni hakika Wanauwezo wa kuvichukua vyote walivyokupa.
Hata hivyo, kama umeenda Kanisani au msikitini kusikiliza Mawaidha au kufundishwa Neno la Mungu basi itakupasa uwalipe Kwa kazi hiyo ya kukufundisha, ndio Yale mambo ha kwenda kila mwisho wa juma Kanisani au misikitini ili mfundishwe habari za miungu yenu. Hivyo lazima muwalipe sadaka na Zaka zao Kwa kazi ya kuwafunza.
Ila kama haukuenda kujifunza, ulienda kutafuta Maisha mazuri, au unatatizo unataka litatuliwe basi hakikisha tatizo Hilo linatatuliwa ndio utoe sadaka au Zaka kama malipo ya Kazi waliyoifanya.
Zingatia, sio lazima kwenda kujifunza neno la Mungu ikiwa tangu ukiwa mtoto ulifundishwa habari za Mungu wako. Utapewa hadithi zilezile na mafunzo yaleyale tuu.
Manabii na watumishi wa Mungu wapo kwaajili ya Kutatua matatizo ya jamii ili nao walipwe Kwa kazi Yao.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umenena vyema.Sasa ukienda kanisani au msikitini ukakuta jengo zuri, viti, meza, viyoyozi,mazuria, vyombo vya mziki na mengineyo
We hujui kuna watu waliwajibika hivo vikapatikana na wewe umefika ukaabudu kwa amani na raha.
Sasa kwanini unaona uzito kutoa sadaka ili wengine wavutiwe kumjua Mungu na kusali katika sehemu nzuri
Mungu anahitaji sadaka na zaka zetu ili injili ihubiriwe
Kuhubiri injili ni gharama
Ili watu wamjue Mungu
Naninatawajika kutoa hizo gharama ili injili iende pote duniani ikiwa sisi waumini tumejawa na kibri hivi
Acha kibri toa zaka na sadaka
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu hana dini mkuu. Acha kupotosha watu. Ninaheshimu sana imani za watu lakini kamwe siungi mkono shughuli za kitapeli kwa mgongo wa dini.Sasa ukienda kanisani au msikitini ukakuta jengo zuri, viti, meza, viyoyozi,mazuria, vyombo vya mziki na mengineyo
We hujui kuna watu waliwajibika hivo vikapatikana na wewe umefika ukaabudu kwa amani na raha.
Sasa kwanini unaona uzito kutoa sadaka ili wengine wavutiwe kumjua Mungu na kusali katika sehemu nzuri
Mungu anahitaji sadaka na zaka zetu ili injili ihubiriwe
Kuhubiri injili ni gharama
Ili watu wamjue Mungu
Naninatawajika kutoa hizo gharama ili injili iende pote duniani ikiwa sisi waumini tumejawa na kibri hivi
Acha kibri toa zaka na sadaka
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu hana dini. Dini ni mali ya mwanadamu.Umenena vyema.
Ili injili iendelee kuhubiriwa ni lazima watu wajitoe.
Mungu yupi mkuu, kila dini ina Mungu wake.Mungu hana dini. Dini ni mali ya mwanadamu.
Hakuna kitu kama hicho mkuu.Mungu yupi mkuu, kila dini ina Mungu wake.
Mungu wa wabudha na waislam ni sawa?? Mungu wa wakristo na waislam.Hakuna kitu kama hicho mkuu.
Mbona jua (Sun) ni moja?? Alafu Mungu anayefanana na binadamu na kukaa kwenye kiti cha enzi huyo hayupo. All natural powers brought together ndio inaitwa Mungu collectively kama ambavyo table, chair na bed huitwa furnitures.Mungu wa wabudha na waislam ni sawa?? Mungu wa wakristo na waislam.
Sasa jua ni kiumbe??Mbona jua (Sun) ni moja?? Alafu Mungu anayefanana na binadamu na kukaa kwenye kiti cha enzi huyo hayupo. All natural powers brought together ndio inaitwa Mungu collectively kama ambavyo table, chair na bed huitwa furnitures.
MUNGU HAHITAJI ZAKA NA SADAKA YAKO, SADAKA NA ZAKA NI MALIPO YA WATUMISHI WA DINI.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
"Mtolee Mungu"
" Hiyo ni sadaka Kwa Mungu wako"
" Unamnyima Mpaka Mungu anayekupa uhai"
Na kauli zingine kama hizo, ni Utapeli mtupu.
Kuna Ile unaambiwa" mtolee Mungu ili akubariki" huo ni Uchawi na ushirikina mkubwa. Kwamba ati unampa Mungu rushwa kama Samunge, labda Ile miungu ya Kwa msisi.
Mungu hahitaji chochote Kutoka Kwako, endapo Mungu huyo atahitaji chochote Kutoka Kwako basi anapoteza vigezo vya kuwa Mungu. Kwa sababu moja ya Sifa ya Mungu ni kuwa sio mhitaji.
Sadaka au Zaka ni MALIPO tunayowalipa viongozi wa dini tunazoabudia ili waweze kuendesha Maisha Yao kama Sisi tunavyofanya kazi katika shughuli zetu.
Viongozi wa dini wanafamilia zao, wanamahitaji Yao, wanahitaji vyakula, nguo, nyumba, magari na mahitaji mengine
Ukienda Kanisani, au msikitini au madhabahuni popote pale, lazima uingie makubaliano na huyo kuhani au mchungaji, au nabii au Mtume kwamba kwako ninakuja Kwa ajili ya Kupata mambo 1,2,3.
Mfano, unakuja Kwa Kuhani Taikon, unaniambia, Kuhani Taikon wa Mungu wa Tibeli, Mungu Mkuu, nimekuja kwako Kwa sababu zifuatazo;
1. Nataka uniombee nipone ugonjwa Fulani,
2. Nataka Njia zangu na kazi za mikono yangu ifanikiwe, nataka ndani ya miaka Hii Mitano niwe ninanyumba au Gari.
3. Nataka ulinzi katika familia yangu.
Hapo nitaingia chumba cha Siri kumuuliza Mungu wa Tibeli kama atakusaidia au Laa. Kama akisema atakusaidia, nitakujia nitakuambia Mungu wa Tibeli kasema atakusaidia, kisha nitakuambia nenda alafu Mungu atakapokusaidia ndio ulete malipo(sadaka) ya Kazi niliyokufanyia ya kuwa Dalali baina yako na Mungu wa Tibeli.
Nitakupa sheria na masharti ya kufuata kadiri nitakavyoagizwa na huyo Mungu wa Tibeli.
Mfano nitakuambia Mungu atakujibu ndani ya mwaka mmoja, atakapokujibu utaleta Sehemu ya ishirini ya Mapato yako ndani ya miaka mitatu.
Kisha utaondoka, utaamua kutoa shukrani au usitoe ni wewe mwenyewe, kwani hapo ulikuja kufanya agano/mkataba na Mungu wa Tibeli. Haukuja kutoa Sadaka wala Zaka wala dhabihu.
Sio nikuombe Sadaka na Zaka Wakati hakuna kazi niliyoifanya, huo ni Utapeli.
Kufumba macho na kuanza kuomba hiyo sio kazi. Hiyo kila MTU anaweza Kufanya, hata mtoto Mdogo anaweza kufumba macho akaomba.
Mchungaji au nabii anayetanguliza umlipe Kabla ya Kazi huyo ni Mhuni, tapeli.
Manabii na mitume wakweli anakupa Huduma kisha wewe mwenyewe utaamua uvunja makubaliano au uwe mwaminifu. Hii ni Kwa sababu, kama wanauwezo wa kukupa Mali au kukusaidia basi ni hakika Wanauwezo wa kuvichukua vyote walivyokupa.
Hata hivyo, kama umeenda Kanisani au msikitini kusikiliza Mawaidha au kufundishwa Neno la Mungu basi itakupasa uwalipe Kwa kazi hiyo ya kukufundisha, ndio Yale mambo ha kwenda kila mwisho wa juma Kanisani au misikitini ili mfundishwe habari za miungu yenu. Hivyo lazima muwalipe sadaka na Zaka zao Kwa kazi ya kuwafunza.
Ila kama haukuenda kujifunza, ulienda kutafuta Maisha mazuri, au unatatizo unataka litatuliwe basi hakikisha tatizo Hilo linatatuliwa ndio utoe sadaka au Zaka kama malipo ya Kazi waliyoifanya.
Zingatia, sio lazima kwenda kujifunza neno la Mungu ikiwa tangu ukiwa mtoto ulifundishwa habari za Mungu wako. Utapewa hadithi zilezile na mafunzo yaleyale tuu.
Manabii na watumishi wa Mungu wapo kwaajili ya Kutatua matatizo ya jamii ili nao walipwe Kwa kazi Yao.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Hivyo visa vya wayahudi wapelekee wayahudi sisi ni AfricansKama ni hivyo - MUNGU asingetaka sadaka ya Ibrahim amchinje Isaka
Yesu asinge angalia watu wanatoa kiasi gani katika sadaka , kwa kumwambia yule Mama masikini yeye ametoa kubwa kuliko wale matajiri - kutokana alitoa alichobakiwa
Wewe ni mtu wa ajabu sana, what is your reference?