Mungu hahitaji Zaka na Sadaka yako, Sadaka na Zaka ni Malipo ya Watumishi wa dini

1 Sam 15:22-23 SUV
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.

You are very super Rubbish, na nakushauri, kama hujui mambo ya dini usiandike, haina maana na haikusaidii. Huu mstari hauna maana yeyote kwenye andiko lako.

Kwa hiyo bwana hupenda hizo sadaka, ila anataka utii kwanza, kwa hiyo ukishatii kutoa sadaka ni sawa? Au ukitii yeye ndo anashuka kuzichukua?

Na hapa alikuwa anaongea na nani? Ana address character ya mtu au la? Na huyu mtu status yake ikoje mpaka aambiwe hayo?

Of course hakuna maana ya kutoa sadaka kama humtii Mungu, na ndo maana tumeambiwa tupatane na tusiwe na neno na mtu kabla ya kutoa sadaka.

Sasa wewe unaleta sakayonsa zako kwamba Mungu hataki na ana namna ya kupokea sadaka? Kwa hiyo yale majengo yanajengwa na nani?
 
Kwa hiyo Kwa uelewa wako na maandiko uliyoyasoma/someshwa au kukaririshwa unafikiri Mungu anataka Sadaka au zaka zako?

Sasa tutaenda Sawa alafu waamuzi watakuwa wasomaji.
Watu kama ninyi sio Wageni kwangu humu jamvini, wengi wa Aina yako waliishia Kupata aibu ya kudumu pale waliposhindwa kutoa hoja katika uwanja.

Leo ni weekend sina kazi.

Kipi unaelewa kuhusu utoaji WA sadaka, dhabihu na zaka?
Unafikiri ni Kwa nini Watu wanatoa Sadaka au zaka au dhabihu?

Tuanzie hapo alafu Rubbish atajitokeza tuu
 
Hicho kisa hukijui ungeenda kusoma kisa kizima Kwanza.
Kisha nenda kasome kisa cha Ibrahim na isaka.
Alafu uje hapa utaelewa Mungu anataka nini.
 
I have no time to discuss with such a low life character kama wewe, ur referring to a Bible, ambayo unajua leo J2 inaelekeza tukakutane kwenye Ibada kama ilivyo desturi yetu.

Wewe umelala nyumbani, and unachukua mstari ambao huuelewi unaandiko mambo ya kijinga yasiyo na maana, bora ungesema ni hisia zako na huna reference.

Au ungerefer kitabu ambacho sikijui, ushauri wa bure, achana na maandiko yanayohusu dini kama hujui kitu, au kosoa but do not refer vitu ambavyo hujui.

Kukosoa ni sawa, but achana na mambo ya kufanya references na vitabu ambavyo huelewi, bora ungesema ni maoni yangu ningeheshimu.
 
Do u believe in a Bible? If u don't, then do not refer it, Kosoa, una haki ya kukosoa na kufanya lolote, but tafuta references sahihi zinazo support theory zako.
 
Unfortunately, kwenye andiko lako hukuweka justification kutoka kwenye biblia, so I rest my case.

Ila kumbuka, unapoongea masuala ya kibiblia weka vifungu kutoka kwenye biblia.
 
I have no time to discuss with such a low life character kama wewe, ur referring to a Bible, ambayo unajua leo J2 inaelekeza tukakutane kwenye Ibada kama ilivyo desturi yetu.

Wewe umelala nyumbani, and unachukua mstari ambao huuelewi unaandiko mambo ya kijinga yasiyo na maana, bora ungesema ni hisia zako na huna reference.

Au ungerefer kitabu ambacho sikijui, ushauri wa bure, achana na maandiko yanayohusu dini kama hujui kitu, au kosoa but do not refer vitu ambavyo hujui.

Kukosoa ni sawa, but achana na mambo ya kufanya references na vitabu ambavyo huelewi, bora ungesema ni maoni yangu ningeheshimu.

Ni Biblia gani Kwa sheria ipi ya Mungu inakutaka Mkutane Leo siku ya jumapili Huko Kanisani?
Maana unaitaja Biblia alafu muda huohuo huelezi mambo ya Biblia.

Tujadili mada iliyopo mezani alafu mengine wasomaji wataamua.
 
Do u believe in a Bible? If u don't, then do not refer it, Kosoa, una haki ya kukosoa na kufanya lolote, but tafuta references sahihi zinazo support theory zako.

Kwa nini unataka MTU ili ajadili kitu au asijadili unamuuliza habari ya kuamini?
Kwa nini usiniulize unaijua Biblia? Hili ndio lingekuwa swali
 
Sasa jua ni kiumbe??
Kuna ulimwengu usiionekana (ulimwengu wa giza) majini, wachawi, vibwengo nk hivyo navyo tuviitaje maana vina nguvu isiyoonekana na vinafanikisha mambo kwa uwezo zaidi ya binadam na kwa hizohizo natural power navyo ni miungu??
Umekwishasema ulimwengu usioonekana. Sasa kama hauonekani, wewe umejuaje kama upo? Hizo ndio moja wapo ya dalili za kutaka kuwatapeli wajinga.
 
MUNGU HAHITAJI ZAKA NA SADAKA YAKO, SADAKA NA ZAKA NI MALIPO YA WATUMISHI WA DINI.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

"Mtolee Mungu"
" Hiyo ni sadaka Kwa Mungu wako"
" Unamnyima Mpaka Mungu anayekupa uhai"
Na kauli zingine kama hizo, ni Utapeli mtupu.
Kuna Ile unaambiwa" mtolee Mungu ili akubariki" huo ni Uchawi na ushirikina mkubwa. Kwamba ati unampa Mungu rushwa kama Samunge, labda Ile miungu ya Kwa msisi.

Mungu hahitaji chochote Kutoka Kwako, endapo Mungu huyo atahitaji chochote Kutoka Kwako basi anapoteza vigezo vya kuwa Mungu. Kwa sababu moja ya Sifa ya Mungu ni kuwa sio mhitaji.

Sadaka au Zaka ni MALIPO tunayowalipa viongozi wa dini tunazoabudia ili waweze kuendesha Maisha Yao kama Sisi tunavyofanya kazi katika shughuli zetu.
Viongozi wa dini wanafamilia zao, wanamahitaji Yao, wanahitaji vyakula, nguo, nyumba, magari na mahitaji mengine

Ukienda Kanisani, au msikitini au madhabahuni popote pale, lazima uingie makubaliano na huyo kuhani au mchungaji, au nabii au Mtume kwamba kwako ninakuja Kwa ajili ya Kupata mambo 1,2,3.

Mfano, unakuja Kwa Kuhani Taikon, unaniambia, Kuhani Taikon wa Mungu wa Tibeli, Mungu Mkuu, nimekuja kwako Kwa sababu zifuatazo;
1. Nataka uniombee nipone ugonjwa Fulani,
2. Nataka Njia zangu na kazi za mikono yangu ifanikiwe, nataka ndani ya miaka Hii Mitano niwe ninanyumba au Gari.
3. Nataka ulinzi katika familia yangu.

Hapo nitaingia chumba cha Siri kumuuliza Mungu wa Tibeli kama atakusaidia au Laa. Kama akisema atakusaidia, nitakujia nitakuambia Mungu wa Tibeli kasema atakusaidia, kisha nitakuambia nenda alafu Mungu atakapokusaidia ndio ulete malipo(sadaka) ya Kazi niliyokufanyia ya kuwa Dalali baina yako na Mungu wa Tibeli.
Nitakupa sheria na masharti ya kufuata kadiri nitakavyoagizwa na huyo Mungu wa Tibeli.
Mfano nitakuambia Mungu atakujibu ndani ya mwaka mmoja, atakapokujibu utaleta Sehemu ya ishirini ya Mapato yako ndani ya miaka mitatu.

Kisha utaondoka, utaamua kutoa shukrani au usitoe ni wewe mwenyewe, kwani hapo ulikuja kufanya agano/mkataba na Mungu wa Tibeli. Haukuja kutoa Sadaka wala Zaka wala dhabihu.

Sio nikuombe Sadaka na Zaka Wakati hakuna kazi niliyoifanya, huo ni Utapeli.
Kufumba macho na kuanza kuomba hiyo sio kazi. Hiyo kila MTU anaweza Kufanya, hata mtoto Mdogo anaweza kufumba macho akaomba.

Mchungaji au nabii anayetanguliza umlipe Kabla ya Kazi huyo ni Mhuni, tapeli.

Manabii na mitume wakweli anakupa Huduma kisha wewe mwenyewe utaamua uvunja makubaliano au uwe mwaminifu. Hii ni Kwa sababu, kama wanauwezo wa kukupa Mali au kukusaidia basi ni hakika Wanauwezo wa kuvichukua vyote walivyokupa.

Hata hivyo, kama umeenda Kanisani au msikitini kusikiliza Mawaidha au kufundishwa Neno la Mungu basi itakupasa uwalipe Kwa kazi hiyo ya kukufundisha, ndio Yale mambo ha kwenda kila mwisho wa juma Kanisani au misikitini ili mfundishwe habari za miungu yenu. Hivyo lazima muwalipe sadaka na Zaka zao Kwa kazi ya kuwafunza.

Ila kama haukuenda kujifunza, ulienda kutafuta Maisha mazuri, au unatatizo unataka litatuliwe basi hakikisha tatizo Hilo linatatuliwa ndio utoe sadaka au Zaka kama malipo ya Kazi waliyoifanya.

Zingatia, sio lazima kwenda kujifunza neno la Mungu ikiwa tangu ukiwa mtoto ulifundishwa habari za Mungu wako. Utapewa hadithi zilezile na mafunzo yaleyale tuu.

Manabii na watumishi wa Mungu wapo kwaajili ya Kutatua matatizo ya jamii ili nao walipwe Kwa kazi Yao.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Matendo ya Mitume 20:32-35..Blessed is the hand that giveth than the one that taketh
2 Wakorintho 8-10
IMANI YA MKRISTO INATAKIWE UNAPOTOA SADAKA UJUE UNAMTOLEA MUNGU HAIJALISHI NANI ANAIPOKEA AU ANAITUMIA VP refer habari ya Anania na Safira Acts 5
 
1 Sam 15:22-23 SUV
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.

Mkuu unajua chimbuko la neno hili hadi Sauli akaelezwa mambo kama hayo?

Sadaka, zaka na dhabihu ni muhimu sana sana katika mamlaka za falme za kiroho. Hata Agano la kale Ukisoma unaona taifa teule la Israeli kila walipokosa au walipokua wakivuka kutoka hatua moja kwenda nyingine walimtolea Mungu dhabihu, sadaka na zaka.

Agano jipya Mungu anamtoa Yesu Mwanawe kua sadaka kwa ajili ya ulimwengu huu. Wewe unasema sadaka, zaka na dhabihu ni mradi wa watu? Hata huogopi kabisa?

Unajua ndio vyote ni Mali ya Bwana na Bwana hujaribu mioyo ya watu kuona wanampenda kwa kiasi gani ili ajipatie utukufu? Umesoma kisa cha Ayubu? Unafikiri kwa nini Mungu anaruhusu Ayubu ajaribiwe?

Ndio zipo sadaka ambazo ni miradi ya watu kwa sababu hata maandiko yanasema nyakati za mwisho manabii wa uongo watatokea. Lakini hii haina maana sadaka na dhabihu zote ni mradi wa watu, na pia Kumbuka aongozwae na Roho ajua namna bora ya kumtolea Mungu sadak na dhabihu.

Na hakuna maombi yanayojibiwa haraka na Mungu yakifanyika katika kweli na kwa imani kama Yale ya kuungamanisha na sadaka.

Mimi nachoamini kila Mtu Ana kupata katika eneo lake na sio kwamba kila sehemu au nyanja unaweza ukaijua kikamilifu. Ni busara kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika jambo lisilo kamilifu na potofu
 
Ila ukumbuke kisa cha Kaini na ndugu yake

Hapo ndio Wakristo tunapopigwa na kitu kizito.

Sadaka inatumika kama kipimo cha utii. Na sio kama kinachohitajika ni hiyo Sadaka.
Ndio maana sadaka zinabadilika badilika kila Zama lakini utiifu ni Ileile unaohitajika.

Mfano, Ibrahim aliambiwa amtoe sadaka mwanaye wapekee, lakini Mungu alichokuwa anataka sio hiyo Sadaka isipokuwa alikuwa anataka kuona Kicho na utiifu wa Ibrahim.

Kuna Watu wanawatapeli Watu na watu wanafikiri kutoa sadaka ndio kumtolea Mungu Wakati huohuo hawamtii Mungu Kwa kushika maagizo yake.

Zaburi 51:16-17
[16]Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
For thou desirest not sacrifice; else would I give it: thou delightest not in burnt offering.
[17]Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka,
Ee Mungu, hutaudharau.
The sacrifices of God are a broken spirit: a broken and a contrite heart, O God, thou wilt not despise.
 
Mungu aliagiza Watu watoe sadaka Kwa sababu kadhaa, kuu ni hizi
1. Kwaajili ya watumishi wanaodumu madhabahuni, wakiwemo Makuhani, maaskofu n.k. ( Hii ni kuhusu Huduma, haihusu Imani) hivyo ni Mshahara
2. Kupima utiifu na upendo wa Watu wake.
(Hii inahusu Imani) namna MTU anavyomcha Mungu.

Hiyo ni zamani ambapo watumishi wa madhabahuni walifanya kazi kubwa ya kukemea uovu na kuwalingania Watu. Lakini sio siku hizi ambapo Hao watumishi hawawezi hara kukemea Maovu ya serikali, kazi kufanya biashara kupitia dini, zipo biashara za shule, hospitali, bank, redio n.k.

Hiyo sio kazi ya Kanisa au msikiti kufanya hayo. Hizo kazi ziachiwe wafanyabiashara.

Kazi ya watumishi wa dini ili tuwalipe Mishahara (tutor sadaka) ni kukemea Maovu na kuhakikisha taifa linanyooka.
Sasa hao ndio wanaambiwa wasichanganye siasa na Dini.
Badala wamsikilize boss wao(Mungu) na job descriptions inayowaongoza wao wanasikiliza wanasiasa na kuwafuata
 
Kwenye uislamu sadaka ni kwa ajili ya kitu fulani kwa mtoaji mfano amemkuta mtu akapendezewa ampatie sadaka anampa hii haina maelezo meengi

Kwenye zaka nako wameorodheshwa watu wa kupewa hizo dhaka kama wajane maskini mayatima nk. Hakuna kwa ajili ya kumpa mungu pesa kwamza haiingii akilini mungu kupewa pesa.

Kila pesa inakazi yake maalumu mfano ukuta wa msikiti au madrasa umeanguka unaona kabisa pale kumeanguka panahitaji pesa ili parekebishwe vyenginevyo ni upigaji
 
Ni kweli Kabisa
 
MUNGU HAHITAJI ZAKA NA SADAKA YAKO, SADAKA NA ZAKA NI MALIPO YA WATUMISHI WA DINI.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

"Mtolee Mungu"
" Hiyo ni sadaka Kwa Mungu wako"
" Unamnyima Mpaka Mungu anayekupa uhai"
Na kauli zingine kama hizo, ni Utapeli mtupu.
Kuna Ile unaambiwa" mtolee Mungu ili akubariki" huo ni Uchawi na ushirikina mkubwa. Kwamba ati unampa Mungu rushwa kama Samunge, labda Ile miungu ya Kwa msisi.

Mungu hahitaji chochote Kutoka Kwako, endapo Mungu huyo atahitaji chochote Kutoka Kwako basi anapoteza vigezo vya kuwa Mungu. Kwa sababu moja ya Sifa ya Mungu ni kuwa sio mhitaji.

Sadaka au Zaka ni MALIPO tunayowalipa viongozi wa dini tunazoabudia ili waweze kuendesha Maisha Yao kama Sisi tunavyofanya kazi katika shughuli zetu.
Viongozi wa dini wanafamilia zao, wanamahitaji Yao, wanahitaji vyakula, nguo, nyumba, magari na mahitaji mengine

Ukienda Kanisani, au msikitini au madhabahuni popote pale, lazima uingie makubaliano na huyo kuhani au mchungaji, au nabii au Mtume kwamba kwako ninakuja Kwa ajili ya Kupata mambo 1,2,3.

Mfano, unakuja Kwa Kuhani Taikon, unaniambia, Kuhani Taikon wa Mungu wa Tibeli, Mungu Mkuu, nimekuja kwako Kwa sababu zifuatazo;
1. Nataka uniombee nipone ugonjwa Fulani,
2. Nataka Njia zangu na kazi za mikono yangu ifanikiwe, nataka ndani ya miaka Hii Mitano niwe ninanyumba au Gari.
3. Nataka ulinzi katika familia yangu.

Hapo nitaingia chumba cha Siri kumuuliza Mungu wa Tibeli kama atakusaidia au Laa. Kama akisema atakusaidia, nitakujia nitakuambia Mungu wa Tibeli kasema atakusaidia, kisha nitakuambia nenda alafu Mungu atakapokusaidia ndio ulete malipo(sadaka) ya Kazi niliyokufanyia ya kuwa Dalali baina yako na Mungu wa Tibeli.
Nitakupa sheria na masharti ya kufuata kadiri nitakavyoagizwa na huyo Mungu wa Tibeli.
Mfano nitakuambia Mungu atakujibu ndani ya mwaka mmoja, atakapokujibu utaleta Sehemu ya ishirini ya Mapato yako ndani ya miaka mitatu.

Kisha utaondoka, utaamua kutoa shukrani au usitoe ni wewe mwenyewe, kwani hapo ulikuja kufanya agano/mkataba na Mungu wa Tibeli. Haukuja kutoa Sadaka wala Zaka wala dhabihu.

Sio nikuombe Sadaka na Zaka Wakati hakuna kazi niliyoifanya, huo ni Utapeli.
Kufumba macho na kuanza kuomba hiyo sio kazi. Hiyo kila MTU anaweza Kufanya, hata mtoto Mdogo anaweza kufumba macho akaomba.

Mchungaji au nabii anayetanguliza umlipe Kabla ya Kazi huyo ni Mhuni, tapeli.

Manabii na mitume wakweli anakupa Huduma kisha wewe mwenyewe utaamua uvunja makubaliano au uwe mwaminifu. Hii ni Kwa sababu, kama wanauwezo wa kukupa Mali au kukusaidia basi ni hakika Wanauwezo wa kuvichukua vyote walivyokupa.

Hata hivyo, kama umeenda Kanisani au msikitini kusikiliza Mawaidha au kufundishwa Neno la Mungu basi itakupasa uwalipe Kwa kazi hiyo ya kukufundisha, ndio Yale mambo ha kwenda kila mwisho wa juma Kanisani au misikitini ili mfundishwe habari za miungu yenu. Hivyo lazima muwalipe sadaka na Zaka zao Kwa kazi ya kuwafunza.

Ila kama haukuenda kujifunza, ulienda kutafuta Maisha mazuri, au unatatizo unataka litatuliwe basi hakikisha tatizo Hilo linatatuliwa ndio utoe sadaka au Zaka kama malipo ya Kazi waliyoifanya.

Zingatia, sio lazima kwenda kujifunza neno la Mungu ikiwa tangu ukiwa mtoto ulifundishwa habari za Mungu wako. Utapewa hadithi zilezile na mafunzo yaleyale tuu.

Manabii na watumishi wa Mungu wapo kwaajili ya Kutatua matatizo ya jamii ili nao walipwe Kwa kazi Yao.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Niliwahi kumwambia mchungaji wangu mmoja kuwa paulo mtume aliishi KWA kushona matenti ya matumizi mbali mbali ya majumbani wala hakutegemea SADAKA za watu,na nyie mnapaswa muwe na kazi za kufanya kujikimu!!

Akachukia na KUSEMA eti anajuta kupokea vyote nilivyowahi kumtumia eti ninamsimanga!

Nikaishia kukejeliwa sana na hapo ukawa mwisho wa mawasiliano!!

JAMBO hili nilijifunza TOKA KWA zac poonen mhindi mchungajir wa kikristo huko Bangalore india!baada ya kumsikiliza,mzee HUWA haombi SADAKA KWA wazungu wala mtu YEYOTE yule!

Nilimkubali sana!!
 
Kama ni hivyo - MUNGU asingetaka sadaka ya Ibrahim amchinje Isaka

Yesu asinge angalia watu wanatoa kiasi gani katika sadaka , kwa kumwambia yule Mama masikini yeye ametoa kubwa kuliko wale matajiri - kutokana alitoa alichobakiwa
Ndugu hizo sadaka/zaka ziliamriwa ili kuwawezesha ukoo wa Lawi kukidhi mahitaji yao maana hawakupewa sehemu ya urithi kwenye nchi ya Israeli na si kwa ajili ya hawa wahuni wa siku hizi wanaochipuka kila mahali na kujiita mitume,manabii,maaskofu n.k. Ndiyo maana mambo hayo huyakuti kwenye Agano Jipya. Kuhusu Ibrahimu kumtoa sadaka Isaka lilikuwa jaribio la imani ndio maana anaitwa baba wa imani.
 
Back
Top Bottom