Mungu hahitaji Zaka na Sadaka yako, Sadaka na Zaka ni Malipo ya Watumishi wa dini

Hii ni sadaka impendezayo Mwenyezi Mungu
 
Mungu wangu haitaji mtu wa tatu kuniombea

Najiombea mwenyewe na ananijibu

Huu ni ushauri wa Bwana wetu Yesu Kristo

Mathayo 6:5-6

Tena msalipo,msiwe kama wanafiki, kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia,ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, wamekwishapata thawabu yao.

Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Uhakika nilio nao ni kwamba Bwana wangu Yesu Kristo anamjua Mungu vizuri kuliko hawa wachungaji na mapadri

Kwa hiyo nafuata ushauri wa Bwana wangu Yesu Kristo maishani mwangu
 

Ni kweli
 
Sasa ukienda kanisani au msikitini ukakuta jengo zuri, viti, meza, viyoyozi,mazuria, vyombo vya mziki na mengineyo
We hujui kuna watu waliwajibika hivo vikapatikana na wewe umefika ukaabudu kwa amani na raha.
Sasa kwanini unaona uzito kutoa sadaka ili wengine wavutiwe kumjua Mungu na kusali katika sehemu nzuri
Mungu anahitaji sadaka na zaka zetu ili injili ihubiriwe
Kuhubiri injili ni gharama
Ili watu wamjue Mungu
Naninatawajika kutoa hizo gharama ili injili iende pote duniani ikiwa sisi waumini tumejawa na kibri hivi

Acha kibri toa zaka na sadaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sadaka ya nini? Unanihubiria kuwa Mungu ananipenda, mimi sijui kuwa ananipenda? Unataka ule bila jasho?? Hupati kitu! Ama kweli dini zimeundwa na wajanja.
 
Uko sahihi, kulingana na fundisho rasmi la kanisa langu, baraka na neema za Mungu hazina sharti, ni "gratuitous"
 
Umenena vyema.

Ili injili iendelee kuhubiriwa ni lazima watu wajitoe.
 
Mungu hana dini mkuu. Acha kupotosha watu. Ninaheshimu sana imani za watu lakini kamwe siungi mkono shughuli za kitapeli kwa mgongo wa dini.
 
Mungu wa wabudha na waislam ni sawa?? Mungu wa wakristo na waislam.
Mbona jua (Sun) ni moja?? Alafu Mungu anayefanana na binadamu na kukaa kwenye kiti cha enzi huyo hayupo. All natural powers brought together ndio inaitwa Mungu collectively kama ambavyo table, chair na bed huitwa furnitures.
 
Mbona jua (Sun) ni moja?? Alafu Mungu anayefanana na binadamu na kukaa kwenye kiti cha enzi huyo hayupo. All natural powers brought together ndio inaitwa Mungu collectively kama ambavyo table, chair na bed huitwa furnitures.
Sasa jua ni kiumbe??
Kuna ulimwengu usiionekana (ulimwengu wa giza) majini, wachawi, vibwengo nk hivyo navyo tuviitaje maana vina nguvu isiyoonekana na vinafanikisha mambo kwa uwezo zaidi ya binadam na kwa hizohizo natural power navyo ni miungu??
 


Wewe ni mtu wa ajabu sana, what is your reference?
 
Kama ni hivyo - MUNGU asingetaka sadaka ya Ibrahim amchinje Isaka

Yesu asinge angalia watu wanatoa kiasi gani katika sadaka , kwa kumwambia yule Mama masikini yeye ametoa kubwa kuliko wale matajiri - kutokana alitoa alichobakiwa
Hivyo visa vya wayahudi wapelekee wayahudi sisi ni Africans
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana, what is your reference?

1 Sam 15:22-23 SUV
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…