Mungu hahitaji Zaka na Sadaka yako, Sadaka na Zaka ni Malipo ya Watumishi wa dini

Kizazi cha sasa hakitaki Uongo na ulaghai.

Fikiria mchungaji anasema utoe sadaka utabarikiwa, au ukitoa sadaka unamtolea Mungu, mpaka hapo hauoni huo ni Utapeli
Ni utapeli tu. Wanaoutetea aidha wanafaidika nao au wana upungufu mkubwa wa uelewa wa mambo ya dini
 
Zac Poonen ni mhubiri wa kweli. Namkubali sana. Hana ujinga na utapeli wa kutaka pesa
 
Mungu ni baba wa wote ila kuna matapeli siku hizi yanajifanya yapo karibu zaidi na Mungu eti tuende kwao yakatuombee mahitaji yetu kwa Mungu. Upumbavu wa kiwango cha lami huu!! Kama huwezi kuongea na baba yako ukiwa na shida unategemea ndugu yako akusaidie kuongea nae basi huna uhusiano mzuri na baba yako.
 
Hizo zaka na sadaka zingekuwa zinafanyiwa financial control ndo ungejua watu wanavyozifuja. Utetezi wako hauna mashiko kabisa
 
Mungu ana zihitaji sana hizo pesa, ili kuweza kusaidia watu waja wake wenye shida, Mungu hawezi, kushuka chini akakupa chakula, inabidi atumie rasilimali za kibinadamu kusaidia wanadamu
 
Mungu ana zihitaji sana hizo pesa, ili kuweza kusaidia watu waja wake wenye shida, Mungu hawezi, kushuka chini akakupa chakula, inabidi atumie rasilimali za kibinadamu kusaidia wanadamu
Basi mpelekee mhitaji moja kwa moja. Zikipitia kwa hawa matapeli hazifiki zote!
 
Mungu ana zihitaji sana hizo pesa, ili kuweza kusaidia watu waja wake wenye shida, Mungu hawezi, kushuka chini akakupa chakula, inabidi atumie rasilimali za kibinadamu kusaidia wanadamu
Sasa kwanini usisaidie watu kitaa waliokuzunguka ? Huoni huo ndio ufanisi ? Kuliko kumpa mtu ili ampe mtu ili atoe msaada ?

Anyway to each their own..., Fanya kwa mapenzi yako ila hizi justification does not make sense....

2 Pac. If the churches took half the money that they was making and gave it back to the community we'd be alright. If they take half the buildings they use to praise God and gave it to motherfuckers who need God we'd be alright. We'd be alright.
 
Swali zuri
Je na yeye mchungaji dalali wake ni nani wakati anataka kuombewa?
 
Utapeli wa hizi dini umeliza watu wengi duniani. Mtu anaamini mpaka anakuwa kama taahira wa kiaina.
 
Dini Iliyo safi Isiyo na Taka Mbele Za Mungu Baba Ni hii Kwenda Kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao na Kujilinda na dunia pasipo Mawaa. YAKOBO 1:27

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Haya ni mafundisho potofu toka kwa wafuasi wa shetani hayambadilishi moyo Mkristo
 
Utapeli wa hizi dini umeliza watu wengi duniani. Mtu anaamini mpaka anakuwa kama taahira wa kiaina.
Hio ni shida yake binafsi na Sio shida ya dini.
Usipotaka yajua maandiko utalazimika kuyajua kwa kuyalipia toka kwa wajuayo.
Hili Sio tatizo la dini bali akili ya mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…