Mungu kama upo unapaswa kuniomba msamaha

Mungu kama upo unapaswa kuniomba msamaha

Habari wanajamiiforums?
Leo nina kesi na Mungu, Kama yupo kweli anapaswa aniombe msamaha.

Sijawahi kumkosea kwa chochote ila yeye amenikosea mara nyingi zaidi.

Pia, Sikumuomba anilete duniani, ila yeye alinileta bila ridhaa yangu kisha aninyime kila ninachostahili.

Mungu toka ulipo uje uniombe msamaha.
Unataka uombwe msamaha na Mungu ambaye unaamini hayupo..!!!! Milembe inakuhitaji.
 
Mungu ameshindwa kwenye maisha yangu
MWENYEZI MUNGU akupiganie kaka

Akupe ujumbe mpya upate kuwaza kwa upya

Usimwache MUNGU bado yuko kazini anakupambania , shetani asikutishe na kukukatisha tamaa

MUNGU ni MWEMA sana na anatoa msamaha kwa kila kosa

Mrudie hujachelewa mtumish
 
Katika utafiti nilioufanya, Nimekuja na hitimisho kuwa wanaojifanya kumuamini Mungu kwa asilimia kubwa ndio wanaongoza kwa unafiki na nahisi hata dhambi wananizidi.

Mungu anajua alichonifanyia ndio maana bado nina kesi naye.

Hamuwezi kujua nyie, Kaeni kwa kutulia alaaaah😉
Kwa namna Fulani ni kweli kwamba wengi wanaitumia dini kama kivuli ijapokuwa sio wote
 
Katika utafiti nilioufanya, Nimekuja na hitimisho kuwa wanaojifanya kumuamini Mungu kwa asilimia kubwa ndio wanaongoza kwa unafiki na nahisi hata dhambi wananizidi.

Mungu anajua alichonifanyia ndio maana bado nina kesi naye.

Hamuwezi kujua nyie, Kaeni kwa kutulia alaaaah😉
Kwahiyo, unangoja Mungu unayeamini kuwa hayupo aje akujibu hapa JF..!!! We wahi Milembe kama hujaharibikiwa zaidi.
 
Wahi mirembe unachangamoto ya akili.

Yaani wewe badala ukawaulize wazazi wako ambao ndo wamekuzaa unakuja kutusumbua huko JF.

Nitoe wito kwa vijana kabla hamjazaa watoto, hakikisha unasababu za msingi za kumleta huyo kiumbe hapa duniani kama huna tumia CONDOM au CHOMOA.

Usije ukawa unatafuta mtoto kwa kufata mkumbo,kwakua umekuta watu katika jamii yako wakifika umri flani lazima waoe au waolewe na kupata watoto. Hakikisha wewe unasababu madhubuti ili siku ya siku mwanao atakapokuuliza uwe na majibu mujarabu.

Kama huna sababu huna hela bora usizae mnatuletea machizi humu duniani.

Hakuna laana na watoto wa leo watawauliza maswali magumu na hamtakuwa na lakuwajibu.Mambo ya kutishia kutoa laana hawa watoto hawatambui na hayana ukweli wowote.

Tafuteni hela!!!Tafuteni hela!!! ndio mfikirie kuzaa,watoto wanataka urithi wao😄😄😄😄

Elimu sio urithi ni wajibu!!!
Huwezi elewa kwanini nina kesi na Mungu.

Endelea kutafakari
 
Huna adabu kwa Mungu. Mwombe msamaha na tubia uovu wako huu. Mungu ni wa rehema atakusamehe na atakuwezesha kuanza upya.
Yeye ndo anapaswa kuniomba msamaha maana anajua ni kwa kiasi gani amenikatili🙏
 
Mzee!

Mungu hadhihakiwi, hilo balaa unalotafuta naomba likupitie mbali .
Mambo ambayo nimepitia ni makubwa. Na sidhani kama kuna balaa kubwa ambayo itakuwa zaidi ya mwanzo.
 
Kwani Kuna watu amewapa vichwa vinne?
Unamiguu miwili kama watu wengine?
Unamikono miwili kama watu wengine siyo?
Hakuna mtu aliyependelewa mkuu
Wote Huwa tunazaliwa katika hali sawa,wakati unalalamika Kuna watu hawana hata miguu,ama mikono ?
Wewe kinachokufanya ulalamike ni nini?
Kwa kuwa unashinda kwenye kijiwe kutwa nzima?
Kwa kuwa haupo kwenye nchi ambayo haina vita?
Kwa kuwa unaweza kupata chakula?
Kwa kuwa hauumwi ugonjwa mkubwa kama cancer?
Acha kukufuru
 
Watoto mnawaanzisha shule bado wadogo, mnawabebesha mabegi makubwa yaliyosheheni vitabu , madaftari na chupa ya maji ya kunywa.

Matokeo yake hawalali ipasavyo maana mnawaamsha usiku usiku ili wajiandae kwenda shule.

Huko shuleni mnawapakia maarifa meeengi kuzidi uwezo wa ubongo wao, matokeo yake ndio kama haya hapa, wengi wao ukubwani wanakumbwa na tatizo la afya ya akili (they can not think properly). Ni sawa na kuibebesha kirikuu mzigo unaotakiwa kubebwa na fuso halafu unalazimisha kirikuu itembee, madhara yake lazima utayaona tu siku za mbeleni.

Kwa mtu aliye timamu hawezi kuwa na fikra za namna hii. Maisha hayajawahi na kamwe hatowahi kuwa mepesi. Ni lazima uumize sana ubongo na nguvu ya mwili ili uyakabili maisha.
 
Ok
Kwani Kuna watu amewapa vichwa vinne?
Unamiguu miwili kama watu wengine?
Unamikono miwili kama watu wengine siyo?
Hakuna mtu aliyependelewa mkuu
Wote Huwa tunazaliwa katika hali sawa,wakati unalalamika Kuna watu hawana hata miguu,ama mikono ?
Wewe kinachokufanya ulalamike ni nini?
Kwa kuwa unashinda kwenye kijiwe kutwa nzima?
Kwa kuwa haupo kwenye nchi ambayo haina vita?
Kwa kuwa unaweza kupata chakula?
Kwa kuwa hauumwi ugonjwa mkubwa kama cancer?
Acha kukufuru
 
Back
Top Bottom