Mungu kwenye Quran kusema kwamba Jua hutuama kwenye kisima cha matope mazito alikuwa na maana gani?

Mungu kwenye Quran kusema kwamba Jua hutuama kwenye kisima cha matope mazito alikuwa na maana gani?

Hiki ni kisa kinasimuliwa,ukisimulia kisa chochote,utaeleza vile kilivyotokea.Kwa mfano mtu asiyeona vizuri,atakapo ona kitu,itakuwa tofauti na mwenye macho mazima,kikiwa kitu hicho kiko mbali,na alipo.
Msimuliaji,wa maelezo ya asiyeona mbali,atasimulia vile,yule alivyoona,hata kama aliona kimakosa.
Kulikuwa na ulazima gani Allah kusimulia visa vya uongo?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Jinsi ilivoandikwa naamini ndio ukweli ..hata masuala ya solar system theory ziko nyingi ..juzi tuh elon musk kasema ile safar ya mwezini ilikua uongo .hapo inatupa picha kua mambo mengi wanatudanganya ...jua kuzama kwenye tope inawezekana hasa ukiangalia lile joto lake la mchana Ni tofaut na usiku au asubui .nb sio kila wasemacho hao wazungu Ni kweli mfano story za aliens Ni hao hao nasa ndio wameleta
Jua kuzama kwenye tope ni uongo mtupu.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Sitakubali mumpinge muhammad
Muhammad kasema
  • Imesimuliwa Abu Dharr:
    Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ambaye alikuwa akipanda punda wakati jua linachomoza. Akauliza: Je! Unajua jua linazama wapi? Nilimjibu: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua bora. Alisema: linazama katika chemchemi ya maji ya joto (Hamiyah).
    Grade Sahih
Kwanza ushakubali sasa kua hadithi yako haija taja tope vizuri ukome kukurupuka.

Sasa nakujibu hadithi yako ni dhaifu na ya uongo.

Nilianza kukataa mwanzo maneno unayo yaongeza kwenye hadithi au aya ili upate maana unayo taka wewe.

Sasa narudi kutakatisha na hiyo hadithi yako ya kuokoteza lete sources hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sina elim kubwa ila nadhan hio hadith sio sahih sabab inapingana na qur'an. Qur-an
.
Inapingana wakati Ina support , Aya ya inayosema alikuta Jua linazama kwenye maji yenye matope meusi

Muhammad katoa maelezo sawa na Koran kabisa

  • Imesimuliwa Abu Dharr:
    Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ambaye alikuwa akipanda punda wakati jua linachomoza. Akauliza: Je! Unajua jua linazama wapi? Nilimjibu: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua bora. Alisema: linazama katika chemchemi ya maji ya joto (Hamiyah).
    Grade Sahih
 
Miongoni mwa masuala ambayo wamishenari wa Kikristo wanayatumia kupinga Qur'ani Tukufu ni kifungu kifuatacho.

"Wanakuuliza juu ya Zul-Qarnain. Sema nitakusomea khabari zake. Hakika sisi tuliuweka uwezo wake katika ardhi, na tukampa njia na njia za kila jambo. Njia moja (hiyo) akaifuata. Hata alipofika machweo ya jua alilikuta limetua katika chemchemi ya maji ya uvuguvugu, akakuta watu karibu nayo." (Kurani Tukufu 18:83-86)

Pingamizi lao ni kwamba jinsi jua linavyoweza kutua kwenye chemchemi ya maji ya kiza ilhali ni kubwa zaidi ya mara bilioni kuliko dunia na haliwezi kamwe kutua kwenye chemchemi ya maji yenye kiza! Wanatukabili kwa pingamizi hili katika hoja zao zote zinazohusu vipengele vya kisayansi vya Qur'an.

Naam, tunakwenda, insha'Allah, kuwajibu. Ninaanza na kunukuu mstari ufuatao wa kibiblia,

“Je! haziko ng’ambo ya Yordani, kando ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani, wakaao katika Araba, kukabili Gilgali, kando ya nchi tambarare za More?
( Kumbukumbu la Torati 11:30 )

Kama tunavyojua, hakuna njia ambapo jua linatua kwa sababu jua ni kubwa zaidi kuliko dunia. n.k. wakati ikiwa maana ni kwamba ni njia ambayo inaonekana kwa watu kwamba jua linazama ndani, pingamizi hilo litatatuliwa. Lakini kwa hakika wanakubali maelezo kama hayo kwa Maandiko yao, si yetu! Zaidi ya hayo, aya hiyo ni mbovu sana kama mmoja wa ndugu zetu Waarabu anavyosema,

Maandishi unayoyaona ni magumu sana kana kwamba yanaeleza anwani ya mtu aliyepotea: Mahali-jua-linaposhuka St., Jiji la Wakanaani, ondoka uwanda wa kwanza wa More, moja kwa moja dhidi ya Gilgali!

Wacha tuendelee kwenye aya nyingine,

"Jua halitakupiga mchana, wala mwezi usiku."
( Zaburi 121:6 )

Tunaelewa kabisa nini maana ya jua kumpiga mtu, lakini nini maana ya mwezi kupiga?! Je, kuna chochote kinachojulikana - kwa mfano - kama kiharusi cha mwezi?! Labda tunapaswa kujua!

Nukuu yetu ya mwisho ya kibiblia ni hii,

"Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili." ( Ufunuo 12:1 )

Mwanamke anawezaje kuvikwa jua ambalo ni kubwa kuliko dunia?!! Kweli hii ni hadithi!

Sasa, tunaacha Biblia ili kuzungumzia pingamizi la wamishonari. Aya inasema, “akaikuta imewekwa kwenye chemchemi ya maji ya uvugu” yaani kwa mujibu wa muono na uoni wake ndio maana Mwenyezi Mungu hasemi “inazama”.

Imam Al-Baidawi anabainisha,

Pengine alifika ufukoni mwa bahari akaona hivyo kwa sababu kulikuwa na maji lakini pembeni kabisa ya macho yake ndiyo maana Anasema “amekuta limetua” wala hasemi “linatuwa”. (Al-Baidawi, Anwar-ut-Tanzil wa Asrar-ut-Taw'il, Juzuu 3, ukurasa wa 394. Kimechapishwa na Dar-ul-Ashraf, Cairo, Misri)

Imam Al-Qurtubi anasema,

Al-Qaffal amesema: Haikusudii kufika kuchomoza au kuzama kwa jua kwamba aliufikia mwili wake na kuugusa kwa sababu linapita angani kuzunguka ardhi bila kuligusa na ni kubwa mno kuingia katika chemchemi yoyote duniani. Ni kubwa sana kuliko ardhi. Lakini ina maana kwamba alifika mwisho wa ardhi yenye watu wengi mashariki na magharibi, hivyo akaikuta - kwa mujibu wa maono yake - ikiwa imekaa kwenye chemchemi ya maji ya uvugu kama vile tunayatazama katika ardhi laini kana kwamba yanaingia ndani ya ardhi.

Ndio maana Akasema: "Ameikuta inawazukia watu ambao hatukuwa tumewawekea ulinzi dhidi ya jua." (Kurani Tukufu 18:90) na haikuwa na maana kwamba inawagusa au kushikamana nao; lakini wao ndio wa kwanza kuinuka.

Al-Qutabiy amesema: Huenda chemchemi hii ni sehemu ya bahari na jua linazama nyuma yake, likiwa na au ndani yake, basi pendekezo hilo linachukua nafasi ya kivumishi na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. (Al-Qurtubi, Al-Game' le Ahkam-el-Qur'an, Juzuu 16, ukurasa wa 47. Kimechapishwa na Dar-ul-Hadith, Cairo, Misri. ISBN 977-5227-44-5)

Imam Fakhr-ud-Deen Ar-Razi anasema,

Zul-Qarnain alipofika upande wa mbali kabisa wa magharibi na hakuna ardhi yenye watu iliyoachwa, alilikuta jua kana kwamba linatua kwenye chemchemi ya giza, lakini si kweli. Vile vile msafiri wa baharini anapoona jua kana kwamba linazama baharini ikiwa haoni ufuo na hali halisi linatua nyuma ya bahari. (Ar-Razi, At-Tafsir-ul-Kabir, Juzuu 21, ukurasa wa 166)

Imam Ibn Kathir anasema,

“Mpaka alipofika machweo ya jua” maana yake alifuata njia fulani mpaka akafika nchi ya mbali zaidi ambayo angeweza kwenda kutoka magharibi. Ama kufikia machweo ya jua angani, haiwezekani. Yale wanayosema wapokezi na wasimuliaji wa hadithi kwamba yeye alitembea muda katika ardhi na jua linapozama nyuma yake si kweli, na mengi katika ngano za Wakristo na Wayahudi na uzushi wa waongo wao.

"aliikuta imetua kwenye chemchemi ya maji ya uvugu" maana yake aliliona jua kulingana na maono yake yakitua ndani ya bahari na hii ni sawa na kila mtu anayeishia ufukweni kuona kana kwamba jua linazama ndani yake (yaani bahari).
(Ibn Kathir, Tafsir-ul-Qur'ân Al-'Azim, Juzuu ya 5, ukurasa wa 120. Kimechapishwa na Maktabat-ul-Iman, Mansoura, Misri)

Ninaamini hii inatosha kukanusha tafsiri iliyowekwa na wamisionari. Na kwa Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hukumu katika kila jambo.
Haujaleza chochote cha maana zaidi ya hoja za kuungaunga. Swali ulilouliza kuhusu ishara inayoelezwa kwenye Kitabu cha Ufunuo ni la ovyo sana. Mtu kaeleza kuwa aliona ishara mbinguni ( just signs) afu unauliza hii ishara inawezekana vipi wakati mwezi ni mkubwa kuliko dunia.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili." ( Ufunuo 12:1 )

Mwanamke anawezaje kuvikwa jua ambalo ni kubwa zaidi ya mara nyingi kuliko dunia?!! bila kujali tempetarure
Hii Familia ya Mtume muhammad hii.. haya kioja kingine...
 
Attachments

  • Sheikh Kipoozeo.mp4
    3.8 MB
Thibitisha Hadith ni yangu? Na si ya waislamu

Pili thibitisha Hadith ni dhaifu na ya uongo
Hiyo hadithi sio yako wala waislamu nimekwambia ni hadithi ya uongo kwa maana nyingine dhaifu

Hadithi sahihi ni hii hapa imepokelewa na imam Bukhary kitab bado u l wahyi

Lazima uwe na elimu ya hadithi wewe. Unajiona una toa nondo kumbe Makolo kolo tu soma hii chini

Sahih al-Bukhari

Narrated Abu Dhar:

The Prophet (ﷺ) asked me at sunset, "Do you know where the sun goes (at the time of sunset)?" I replied, "Allah and His Apostle know better." He said, "It goes (i.e. travels) till it prostrates Itself underneath the Throne and takes the permission to rise again, and it is permitted and then (a time will come when) it will be about to prostrate itself but its prostration will not be accepted, and it will ask permission to go on its course but it will not be permitted, but it will be ordered to return whence it has come and so it will rise in the west.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo hadithi sio yako wala waislamu nimekwambia ni hadithi ya uongo kwa maana nyingine dhaifu

Narrated Abu Dhar:

The Prophet (ﷺ) asked me at sunset, "Do you know where the sun goes (at the time of sunset)?" I replied, "Allah and His Apostle know better." He said, "It goes (i.e. travels) till it prostrates Itself underneath the Throne and takes the permission to rise again, and it is permitted and then (a time will come when) it will be about to prostrate itself but its prostration will not be accepted, and it will ask permission to go on its course but it will not be permitted, but it will be ordered to return whence it has come and so it will rise in the west.
😂😂😂🤣 Umeshahitimisha Jua kuzama kwenye maji
Kumbuka chini ya kiti Cha Allah ambapo Jua tusipo liona linaenda kusujudu Kuna maji 😂😂😂😂

Umefunga mada kibabe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787] Umeshahitimisha Jua kuzama kwenye maji
Kumbuka chini ya kiti Cha Allah ambapo Jua tusipo liona linaenda kusujudu Kuna maji [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Umefunga mada kibabe
Chizi wewe kwenye arsh ya ALLAH kuna tope

Usijichekeshe na hadeeth zako dhaifu una tuletea sisi hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo Mungu akawa anamsimulia Mohammad vitu vya uongo?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Kwaio ulitak mung aseme uongo. Muhammad (pbh) aliulizwa na watu wake kuhus huyo mtu "WANAKUULIZA JUU YA DHUL-KANAIN"

Ilikua lazima story ya Dhul-kanain iwe kama ilivokua ili watu wafaham dhul-kanain ni nan.

Kuongeza au kupunguza chochote kweny hio story kungemfany Muhammad (phb) aonekan muongo,sabab mpka watu wanakuuliza kuhus mtu tafsir wanahabar nae vip ukipotosha [emoji2369].

Kuhusu jua kauli ya Allah ni jua linaelea [21:33].
 
Hadithi yangu mimi haija taja maji wewe unaumwa uchizi enh

Hadithi yako ni ya uongo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kusujudu Jua linasujudu limesimama ? Tumia akili
Linaenda kwenye kiti Cha Allah kusujudu na chini ya kiti Cha Allah Kuna maji , embu connect dots

Ingine hii Muhammad kapigilia msumari
 
Inapingana wakati Ina support , Aya ya inayosema alikuta Jua linazama kwenye maji yenye matope meusi

Muhammad katoa maelezo sawa na Koran kabisa

  • Imesimuliwa Abu Dharr:
    Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ambaye alikuwa akipanda punda wakati jua linachomoza. Akauliza: Je! Unajua jua linazama wapi? Nilimjibu: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua bora. Alisema: linazama katika chemchemi ya maji ya joto (Hamiyah).
    Grade Sahih

Mbona vitu hiv havihitaj akili kubwa kuvielewa. Kwanza hadith inasema chemchem ya maji ya moto.Qur an inasema chemchem ya matope meusi mpka hapo hio hadith sio sahih.

Hatuwez zungumzia hadith dhaif.
 
Hadith ni waislamu na ni sahih
Gusa link usiogope

Elewa haya maelezo ya wanachuoni Kwanza

Sheikh al khattab Undoubtedly the reports in the books of al-Bukhaari and Muslim take precedence, according to the critics and scholars, than those in other books and Musnads.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona vitu hiv havihitaj akili kubwa kuvielewa. Kwanza hadith inasema chemchem ya maji ya moto.Qur an inasema chemchem ya matope meusi mpka hapo hio hadith sio sahih.

Hatuwez zungumzia hadith dhaif.
Gusa link kawashauri walio weka sahih wafute kwani wewe ni mjuzi kuliko wao

Back
Top Bottom