Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Utaelezeaje kitu ambacho hakipo?

Kama sio hadithi hadithi tu na stori uchwara uchwara kama mnavyofanya.
Nikueleze tu kwamba hakuna ambacho hakipo - kila kitu kipo ilimradi akili ipo.

Mfano huu mdogo ukusaidie kujifunza.

Kabla ya uvumbuzi ( sijui hata unajua uvumbuzi ni nini) wa kumputa au simu - kabla ya kuwa na kitu kinachoitwa kumputa au simu leo hilo, neno hilo kumputa au simu halikuwepo.

Unajua nini kitakuwepo miaka 1000 ijayo? Bila shaka jibu lako ni kwamba mimi sitakuwepo hivyo nitawezaje kujua! Basi mfano huu ukufundishe miaka 1000 iliyopita.
 
Wewe hata kuandika huwezi una bwabwaja bwabwaja tu..

Wala huelewi hata unacho andika.

Unafanya a lot of logical fallacies kuanza kutaka ziwe fact kumbe hakuna kitu.

Unaruka ruka tu.
 
Aiseeee
Mkuu unamaanisha Dunia yote hii hawajui Mungu ni nini ndio maana wanashindwa kumchakata kisayansi isipokua wewe tu?

Ni wapi umewahi kuona imetengenezwa scientific theories kuhusu Mungu? Au peponi au malaika nk nk?
Hao Manguli wenyewe wa sayansi walikua na dini zao lakini walijiepusha na kuchanganya imani zao na sayansi

Mungu amefafanuliwa kinaga ubaga kwenye scriptures.
Kwa mujibu wa maandiko (Tanakh, Bible,Quran)Mungu hafananishwi wala kulinganishwa na chochote..... NI KUFURU.
Njia zake sio njia zetu wanadamu.......... Halafu wewe unataka tuanze kumtengenezea NADHARIA?
Sasa kama na wewe umekuja na Mungu wako mpya ambaye hatumjui ni nini au nani na anayeweza kuchakatwa kisayansi basi utupe hizo data zake tuzichakate..... Ila Mungu wa kwenye scriptures tajwa ameelezwa wazi kabisa ni nani na kwanini katuumba na anataka tufanye nini na hachunguziki

Theory za kisayansi hazitengenezwi from nowhere au kwa mtu kusema tu kuna kitu fulani halafu sayansi ianze kutengene nadharia based na ulichoropoka tu....... science doesn’t work that way mkuu.
Nadharia Zinatangenezwa pale physical data(accessible) zilizo kusanywa zinapokua hazitoshelezi kutoa hitimisho ndio inatengenezwa NADHARIA
Big Bang imetengenezwa baada ya ku access data zilizopo ambazo ni kila kitu kilichopo duniani na angani, zikachakatwa ikatengenezwa Bing Bang.
Nadharia ya Solar system ilianza kwa kukusanya data za sayari zingine zilizo kua accessible kwa darubini hadi ilipokuja kuwa proven..... haikuanza kwa Hadithi za alfa ulela wa ulela

Sayansi inachakata kitu ambacho ni accessible kujua ukweli wake au kutengeneza nadharia.

Sasa huyo Mungu unaanza kukusanya data gani? Unapata wapi data za kuchakata kujua malaika? Kwa kusoma Wagalatia 2? au sijui Surat inayosema ukifa unampigania Mungu utapewa mabikra 72 wa kuzagamua peponi?
 
Mungu ni roho kamili na ukamilifu wake hauna mipaka
 
Mkuu nikuulize swali
Hivi wewe Huyu “Mungu” umemjulia wapi hadi “ukajua” yupo?
Reference gani zilitumika ili kupata “kumjua” Mungu?
 
Sasa hata kama wewe hujijui ni binadamu, sidhani uthibitisho upi utakufaa ujue kwamba wewe ni binadamu.

Ukitaka uthibitisho, look at yourself.

Ukijiona wewe ni roboti basi wahi kituo cha afya.
Soma nlichondika, Then angalia majibu yako


Nadhani unajishangaa hata wewe mwenyewe, Wewe umeshindwa kuthibitisha kama wewe ni Binadamu ila unataka mimi nkuthibitishie kuhusu Mungu hahaha
 
Soma nlichondika, Then angalia majibu yako


Nadhani unajishangaa hata wewe mwenyewe, Wewe umeshindwa kuthibitisha kama wewe ni Binadamu ila unataka mimi nkuthibitishie kuhusu Mungu hahaha
Sawa roboti..
 
Soma nlichondika, Then angalia majibu yako


Nadhani unajishangaa hata wewe mwenyewe, Wewe umeshindwa kuthibitisha kama wewe ni Binadamu ila unataka mimi nkuthibitishie kuhusu Mungu hahaha
Mkuu umeanza kwa kumuuliza anataka ushahidi gani kuwa kuna Mungu ili umthibitishie.
Na ukataka akuthibitishie kama yeye ni binadamu.
Akikwambia aje sehemu ulipo mkutane na ujiridhishe kuwa ni binadamu Je wewe utaweza kuthibitisha kama Mungu yupo?
Utaweza kumpeleka kwa Mungu akamuome kama ulivyo muona yeye?

Mnaulizaga maswali ya kitoto sana badala ya kutoa uthibitisho tu
 
Mkuu nikuulize swali
Hivi wewe Huyu “Mungu” umemjulia wapi hadi “ukajua” yupo?
Reference gani zilitumika ili kupata “kumjua” Mungu?
Mkuu.

Swali lako linanirudisha wakati wa umri wangu wa kuanza kutumia akili. Wakati ule nilipoanza kufikiri, kujifunza, kuwasiliana na kutafuta maana ya vitu mbalimbali. Ukiacha vitu vingine vyote vilivyopo, ukiacha na ufanyaji kazi wao na jinsi yao, mtu pia ni kitu kilichonistajaabisha na bado ananistaajabisha sana.

Hivi ndivyo nilivyojua kuna Mungu - jina tunaloita Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili.

Swali langu daima lilikuwa: Je! Vitu hivi yaani ulimwengu upo tu, bila kusababishwa na hali fulani au nguvu fulani? Yaani ulimwengu ndio wenyewe vitu na ndiyo wenyewe nguvu au hali iliyosababisha ulimwengu au vitu vyote vilivyopo kutokea na kuwepo na kuendelea kuwepo?

Na kama ulimwengu upo tu, yaani hauna mwanzo wala mwisho; haujasababishwa na nguvu yoyote au hali yoyote kutokea au kuwepo-wenyewe ndio hiyo hali au ndiyo hiyo nguvu ya kutokea, kuwepo na kuendelea kwake: moja, hii hali ya viumbe kuwa tofauti, kwa mfano mtu na viumbe wengine inaashiria nini au inaelezea nini?

Mbili, ikiwa kama ulimwengu wenyewe upo tu hauna chanzo wala mwisho, haujasababishwa na nguvu yoyote au hali yoyote - wenyewe ndio hiyo nguvu au ndiyo hiyo hali ya kutokea, kuwepo na kuendelea kwake, kwa nini vitu au viumbe vingine vinatoweka kabisa?

Hivyo nimejua kwamba ulimwengu yaani vitu vyote vilivyopo as material things hauna mamlaka dhidi yake kama ulimwengu. Yaani kwa mfano, mwili kama mwili asa material things hauwezi kufanya au kutengeneza kitu. The mental processes that is the power of mind can create things.

Kwa kurejelea ulimwengu kama vitu vyote vilivyopo. Iwe ni kama baadhi ya wanafalsafa waliosema ulimwengu ndio Mungu Mwenyewe au vyovyote vile watu wanavyoelewa na kufafanua ulimwengu, haimanishi chochote isipokuwa Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Utambuzi yaani Akili.
 
Huo "uwepo wa hali ya juu wenye utambuzi yaani Akili" ulikujaje au ulitokeaje?

Au ulitokea tu from no where?
 
Nadharia ya mlipuko mkubwa (big bang theory) ni mawazo (kama ulivyosema physical data) zinazoelezea tokeo la ulimwengu: vitu vyote vilivyopo vilitokeaje. Physical data za nadharia ya big bang zinaeleza vitu vilivyopo vilivyotokea

Nadharia ya big bang inasema ulimwengu ulitokea kwa sababu ya mlipuko mkubwa. Kwa maneno mengine, nadharia ya big bang anasema mlipuko mkubwa (nishati - energy) ndio ulioumba ulimwengu. Na Dini inasema Mungu Ndiye aliyeumba ulimwengu. Sasa, ni nini usichoelewa hapo? Kama sio sayansi?
 
Maandiko matakatifu yanahusu maadili - jinsi gani ya kutenda. Ndiyo jinsi gani ya kuishi: nini unatakiwa kufanya na nini hutakiwi kufanya na kuwafanyia wengine. They're all about natural law or moral law.
 
Wewe hata kuandika huwezi una bwabwaja bwabwaja tu..

Wala huelewi hata unacho andika.

Unafanya a lot of logical fallacies kuanza kutaka ziwe fact kumbe hakuna kitu.

Unaruka ruka tu.
Kwa sababu wewe uwezo wako wa kuchakata taarifa na kung'amua mambo ni hafifu.

Wewe ni mnyama ambaye unatawaliwa na mwili si busara.
 
Kwa sababu wewe uwezo wako wa kuchakata taarifa na kung'amua mambo ni hafifu.

Wewe ni mnyama ambaye unatawaliwa na mwili si busara.
Umeishiwa hoja unaanza Viroja.

Umebaki kutapatapa..

Bure kabisa.
 
Umeishiwa hoja unaanza Viroja.

Umebaki kutapatapa..

Bure kabisa.
Uko sahihi kusema viroja kwa sababu uwezo wako wa kuchakata taarifa, kuona uwezekano na kutafisiri ni hafifu sana hivi kwamba nakuweka kundi moja na mnyama asiye na busara.

Ovyo kabisa.
 
Umeniuliza vizuri kuwa akija akanithibitishia yeye ni binadamu je nitaweza kumthibitishia kuhusu Mungu ? Lakini kabla hujasubiri jibu langu umemaliza kwa kuita ni swali la kitoto,,

Lakini vile vile haujafahamu mantiki ya mimi kutaka uthibitisho kuhusu yeye, Huoni kama wewe ndio unaleta utoto ?
 
Mi kwa mtizamo wangu. Huyu Mungu tunaemzungumzia atakuwa kaumba viumbe vingi sana na madunia mengi sana. Sasa kila dunia kaiwekea viumbe vyake tofauti tofauti na kanuni za asili zinazoviongoza hivyo viumbe.
Mfano wanyama kila mnyama unaemuona anaongea na mwenzie wa jamii yke kabisa wanautaratibu wa asili unaoongoza dunia yao. Na vile tunavyoona labda paka hana akili sio kweli wana akili zinazoishia kwenye levo yao. Sisi binadamu pia tunajiona tuna ufahamu sio kweli ni ufahamu unoishia levo yetu. Sasa sisi juu yetu utakuta tena Kuna malaika. wanatuona tunamapungufu na tu wadhaifu na levo yao iko juu kuliko sisi. Na ndio maana unakuta ukisoma Biblia unakuta kuna mahali Mungu anamtuma kunguru ampelekee Eliya chakula. Sasa utajiuliza tangu lin kunguru akatumwa. Ni kwamba Mungu kila kiumbe kakiwekea kinafuata kanuni ile ile ya asili bila kuingiliana japo yeye vinamjua japo kwa kuhisi na vikitumwa vinajua mamlaka ya Mungu na kutii. Ukimsikiliza Yesu anasema amepewa mamlaka juu ya wote wenye mwili yaan ishu ya kwenda Mbinguni kwa wnadam Yesu kaachiwa. Kingine viumbe vyote vya Mungu vinamjua kwa asilimia 00000.01. na tena utamjua tu kwa yeye kukufunulia katika ile levo anayotaka yeye. Tena ukisoma Biblia utagundua badhi ya siri nzito kwamb kuna wenye uhai wanne wamekizunguka kiti kikuu Mbinguni na biblia haijatuambia ni viumbe gan hivyo. So kma alivyosema mleta muda ishu ya Mungu ni kubwa mno kiasi kwamba uwezo wa mwanadam kuelewa ni mdogo sana. Bado hujaweka ule mstar Yesu aliosema nina kwenda kwa Baba kuwaandalia makao. It means kuna madunia kibao bdo unaendelea kujengwa. Hayo ni machache kuhusu ufahamu wangu. Ila kuhusu Mwenyezi Mungu ni kweli yupo. Ni kma vile giza na mwanga au mema na mabaya. So dunia imeumbwa kuwili hasi na chnya so kama unawez kuwaza au kutenda mema basi unaweza kufanya hivyo vibaya pia so huo ubaba wa huo ubaya ni shetan na ubaba wa huo wema ni Mungu. Asanten
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…