Kwamba sasa kuanze kuwa na Scientific Theories za Mungu, shetani, malaika, life after death, jehanam peponi nk nk?
Mkuu sina hakika kama unajua maana ya Scientific theory.
Ninacho kiona kwako ni unatumia nguvu kubwa kutaka kuthibitisha Imani ya dini Kisayansi
Narudia tena kwamba Imani ya dini inakengeuka principal zote za kisayansi
Hakuna namna unaweza ku access “data” za imani ili zichakatwe kisayansi
Sayansi huwa haichakati from NOTHING
Mkuu. Sio nia yangu kumshawishi yeyote. Lakini kama wanyama wenye busara, umakini unapaswa kuzingatia akili kutuongoza sio tu kuelewa ulimwengu, bali kwa jinsi gani tunafikia hatua hiyo.
Pamoja na kwamba mtu ana wajibika kwa mambo mbalimbali, nyajibu hizo ni pia kujifunza. Kama mtu unataka kuwa salama; unataka kuendelea, unalazimika kufuatilia kwa karibu vitu mbalimbali - elimu ya vitu mbalimbali, kujifunza.
Watu huenda shule na vyuo kujifunza. Watu hufanya tafiti na utafiti wa kisayansi kujifunza. Kujifunza ni kutafuta ukweli au kujua ukweli - jinsi vitu au mambo yalivyo na jinsi gani ya kutenda au kufanya mambo au vitu.
Kabla ya kusema sayansi inafanyaje kazi zake na kazi hizo lengo lake ni nini; kwa sababu si kweli kwamba sayansi inajishughulisha tu na vitu vinavyoonekana na vinavyoweza kupimika, bila ya lengo lolote, ni vema tukajua kwanza sayansi maana yake ni nini kabla ya kuangalia msingi wake mkuu, nadharia.
Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli mbalimbali zilizobainishwa hazijathibitishwa. Kuna misamiati msingi katika maana hiyo ya sayansi. Nayo ni hii hapa chini:-
Moja, sayansi ni maarifa - hili ni muhimu sana kujua kwa sababu hili la maarifa ndiyo linatengeneza msingi mkuu wa sayansi,
Nadharia (Theory). Kwa hiyo ni muhimu sana kujua maarifa maana yake ni nini. Kwa sababu kwa kujua maarifa ni nini unaweza kuelewa msingi wa sayansi, nadharia.
Mbili ni
"kweli zilizobainishwa hazijathibitishwa" . Hii inamaanisha kwamba sayansi inashughulika na kuthibitisha kweli zilizobainishwa hazijathibitishwa, kwa kufanya vitendo, kwa kutazama, na kwa kufanya majaribio.
Lakini hatahivyo,
kweli zilizobainishwa ni nini au maana yake ni nini hadi sayansi idhithibitishe?
Kweli zilizobainishwa maana yake ni ulimwengu wote - mwanzo wake na mwisho wake. Yaani vitu vinatoka wapi, vinaenda wapi? Mtu anatoka wapi, anaenda wapi? Mtu anatakiwa aishije - jinsi gani ya kutenda katika maisha? Ouvu ni nini? Kwa nini duniani kuna ouvu? Unatoka wapi? Wema ni nini? Na kwa nini wema na si ouvu? Kifo ni nini? Nini huendelea baada ya kifo?
Kwa lugha rahisi, sayansi inafanya kazi ya kuthibitisha kama mambo hayo (kweli zilizobainishwa hazijathibitishwa), ni kweli au si kweli, yapo au hayapo.
Sasa, kwa jinsi gani tunathibitisha jambo hili au jambo fulani ni ukweli au sio ukweli, lipo au halipo. Kwa maneno mengine, tunaelezaje katika utaratibu unaoeleweka (kiakili) wenye mpangilio ulionyooka (kimantiki) na kupimika (kuonekana) kuwa jambo hili au jambo fulani lipo au halipo, ni ukweli au sio ukweli. Hii ndio huitwa nadharia - msingi mkuu wa sayansi.
Na kama nilivyoandika kwamba nadharia maana yake ni ujuzi wa kuunda mfumo wa mawazo au wa maelezo; au muongozo uliopangwa ili kuelezea ukweli wa jambo fulani.
Jambo muhimu katika maana hiyo ya nadharia ni,
ujuzi kama ilivyo sayansi ni,
maarifa (Fuatilia maarifa na ujuzi).
Jambo moja muhimu kuhusu sayansi. Sayansi ni kama mwili - una viungo mbalimbali. Maana yake sayansi imegawanyika katika elimu (matawi) mbalimbali (Natural sciences, social sciences, formal sciences)na kila elimu (tawi) nayo limegawanyika katika elimu (aina) mbalimbali. Hizo zote ni sayansi -sawa ulivyo mwili mmoja viungo mbalimbali, inaelezea upi ni ukweli na upi sio ukweli kuhusu ulimwengu, ukweli ambao tuko nao (bayana), ila bado hatujui waziwazi.