Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Ni kweli Scriptures ni msingi wa mafundisho ya dini licha ya kasoro mbalimbali za kidini zinazoweza kuwako.

Holy scriptures zinafunua "kweli za akili" zilizotufikia kwa njia ya imani.

Maandiko matakatifu yanaanzisha utafiti wa kisayansi: maarifa yanayofuatilia ukweli - kwa jinsi gani kweli hizo za akili zilizofunuliwa kwa njia ya imani ni ukweli; na kwa kweli dini nayo kama sayansi inamtafuta Mungu, yaani ukweli.

Kosa kubwa ni kufikiri kwamba sayansi inapinga imani (dini) au kwamba imani (dini) inapinga sayansi. Huwezi kuachanisha imani (dini) na sayansi: wakati wote palipokuwa na dini na sayansi pia ilikuwepo.
Mkuu Sayansi haipo kwaajili ya kupinga Imani ya Dini,
Imani ya Dini na Sayansi ni vitu viwili tofauti kabisa
Tatizo linakuja pale mnapotaka kutumia Sayansi kuthibitisha Imani ya Dini

Imani inakengeuka principals zote za kisayansi kwasababu kwenye imani ya Mungu kila kitu kinawezekana....... I mean every thing

Unless other wise uwe na tafsiri yako peke yako ya maneno IMANI na SAYANSI
 
Hakuna Mungu nje ya ancient scriptures....... HAKUNA
scriptures zinasema Mungu yupo na amewahi kuja duniani kama Yesu watu wakampiga na mijeredi, ameongea na manabii(Bibilia), Mungu ameongea na Mudi kupitia jibrili(quran), Mungu anaonekana kama jua(greek) nk nk
Tatizo kubwa la waafrika (I am sorry to say this) ni kutotaka kujifunza na kutafuta ukweli.

Ni jamii ilioanguka - isioweza kufuatilia ukweli.

Wayahudi ambao umerejelea kitabu chao (Tanakh) ndio wanasayansi na watafiti wakubwa duniani. Kanisa Katoliki ni wanasayansi na watafiti wakubwa ulimwenguni. Jamii za wazungu, wajapani ni wanasayansi na watafiti wakubwa duniani.

Wao wanafuatilia ukweli, waafrika wao hawafuatilii ukweli. Kwa mfano jambo kwamba Mungu alikuja duniani (Yesu) au Mungu aliongea na Mohamed. Je! Jambo hilo likoje?

Au ni kwa jinsi gani mtoto anaweza kuzaliwa pasipo kufanyika tendo la ndoa au mchakato wa kimaabara wa utungishaji mimba?

Imani inaeleza hayo. Lakini hatahivyo, mambo hayo ukweli wake ukoje? Wenzetu wanafuatilia si tu hayo, bali kila kitu kujua ukweli wao - sayansi.
 
Tatizo kubwa la waafrika (I am sorry to say this) ni kutotaka kujifunza na kutafuta ukweli.

Ni jamii ilioanguka - isioweza kufuatilia ukweli.

Wayahudi ambao umerejelea kitabu chao (Tanakh) ndio wanasayansi na watafiti wakubwa duniani. Kanisa Katoliki ni wanasayansi na watafiti wakubwa ulimwenguni. Jamii za wazungu, wajapani ni wanasayansi na watafiti wakubwa duniani.

Wao wanafuatilia ukweli, waafrika wao hawafuatilii ukweli. Kwa mfano jambo kwamba Mungu alikuja duniani (Yesu) au Mungu aliongea na Mohamed. Je! Jambo hilo likoje?

Au ni kwa jinsi gani mtoto anaweza kuzaliwa pasipo kufanyika tendo la ndoa au mchakato wa kimaabara wa utungishaji mimba?

Imani inaeleza hayo. Lakini hatahivyo, mambo hayo ukweli wake ukoje? Wenzetu wanafuatilia si tu hayo, bali kila kitu kujua ukweli wao.
Mkuu imani za dini kwa wenzetu zimebaki kama tamaduni tu,
Shida ipo kwetu tunaojifanya wafia dini

Huwezi kuwakuta wayahudi wanakesha kwenye masinagogi na Tanakh mikononi kuomba favour kwa Mungu ili kuleta mvua, utawakuta maabara wanachakata mbegu bora, wanatengeneza mbolea na madawa na wanavumbua mitambo ya kuchimba maji kwa umwagilijiaji..... wakati sisi huku tunakesha makanisa, mafuta ya upako nk tukiomba favour kwa Mungu atupe wake na waume, atupe utajiri na kutuponya na ukame nk

My friend USA au UK au China hazipo pale kwasababu ya ancient scriptures...... BIG NO

Kama kuna mabara yalio athiriwa pakubwa na imani ya dini basi ni bara la Afrika pamoja na mashariki ya kati ukiondoa Israel
Sisi kwetu dini ni maisha ya kila siku lakini wenzetu dini imebaki kama UTAMADUNI tu

Mkuu wenzetu sasa hivi hawana habari za kukomaa na imani za dini tena wapo busy kuporesha maisha yao logically(sayansi) badala ya kukaa unaomba kwa Mungu akupe favor,
Yaani Makanisani ukitaka kuwa shoga wewe tu, ukitaka kuoa na kuacha wewe tu...... hawajali maandiko yanasema nini kwasababu wanachojua wao maisha ndio haya haya na sio maisha mengine ya kufikirika

Habari ya kubisha Yesu ni Mungu au la wenzetu walikwisha pita kitambo sana mkuu, wanaona ujinga kudeal na vitu vya kufikirika
Shida tunayo sisi tunaokomaa kwamba kuna Mungu muweza wa yote unachotakiwa ni kumuomba tu na kuamini
 
Upo kifungo cha nnje mkuu ,imani tu ni dhana isiyo na uhuru wowote 😁
Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaah! Wrong!

Je kama imani hiyo nimeiamua mwenyewe? Swali la kujibu hapa ni: Kama tukikaa wananchi tukapiga kura tukachagua kuongozwa kidikteta na say Magufuli/Maalim Seif...... je hiyo ni demokrasia au sio demokrasia??
 
Uhuru wa kuchagua kutokuwa huru nalo pia ni gereza kama haujui haki zako za kuwa huru , ila kama una fahamu uhuru wa kuwa huru ,umeamua tu ni sawa katika huo uhuru wako .
 
Ewaaaaaah! Umeelewa vizuri. Hivyo ndivyo ilivyo
 
Mkuu Sayansi haipo kwaajili ya kupinga Imani ya Dini,
Imani ya Dini na Sayansi ni vitu viwili tofauti kabisa
Tatizo linakuja pale mnapotaka kutumia Sayansi kuthibitisha Imani ya Dini

Imani inakengeuka principals zote za kisayansi kwasababu kwenye imani ya Mungu kila kitu kinawezekana....... I mean every thing

Unless other wise uwe na tafsiri yako peke yako ya maneno IMANI na SAYANSI
Mkuu.

Ni kweli sayansi inashughulika na vitu vinavyoonekana na vinavyoweza kupimika. Na imani inashughulika na mambo ya badae na bayana ya vitu visivyoonekana.

Kwa lugha nyingine, imani inafunua kweli za akili na sayansi inatafuta kuthibitisha kweli hizo. Nitaeleza kwa mfano, imani inaeleza kuwa ulimwengu uliumbwa na Mungu. Sayansi inatafuta ukweli wa wazo hilo - kwa jinsi gani ulimwengu umetokea? That's science.

Imani inaeleza kuwa Bikra Maria alimzaa Yesu bila kufanya tendo la ndoa na mwanaume; na kwamba kuzaliwa kwa Yesu hakukuwa kwa uhandisi wa kimaabara - imani inaeleza hivyo. Sayansi inatafuta ukweli wa jambo hilo - kwa jinsi gani (mtu) mtoto anaweza kuzaliwa pasipo ya mwanamke na mwanaume kufanya tendo la ndoa? Au pasipo ya mbegu za mwanaume na yai la mwanamke kupitia mchakato wa uhandisi wa kimaabara?

Muhimu kajua ni kwamba kati ya sayansi na imani - moja yaani, sayansi inashughulika na vitu vinavyoonekana na vinavyoweza kupimika: mambo au vitu vilivyopo sasa.

Na nyingine - yaani, imani inashughulika na mambo ya badae na bayana ya vitu visivyoonekana: mambo au vitu ambavyo kwa sasa havipo au havionekani.

Aidha, pamoja na imani, sayansi ni maarifa yanayokua na yanayoendelea.
 
Imani hasa hizi mnazoita za kiroho ni chaka la ujinga Africa .
 
Watafanyaje uchunguzi wakati wanambiwa kila siku jp kanisani kazi za. Mungu hazichunguziki😁😁😁
🤣🤣
Kusema ukweli nimecheka sana hasa hapo kwenye neno kazi za Mungu hazichunguziki 🤣🤣
 
Usicheke mkuu kwani haujawahi kukutana na hawa viumbe wanaitwa walokole?
 
Back
Top Bottom