Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Hivi kiuhalisia mkuu, kitu kinaweza kuwepo bila ya kufanyika, mfano ulimwengu?
 

Unadhan kabla hujazaliwa, ulikuwa wapi
 
Hivi kiuhalisia mkuu, kitu kinaweza kuwepo bila ya kufanyika, mfano ulimwengu?
Ndio kinaweza kuwepo.

Ulimwengu upo tu bila kufanyika.

Kama kila kitu kilichopo kinahitaji kufanyika, Hata aliyefanya vitu kufanyika atahitaji kufanyika vilevile.

Na pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo kufanyika.

Yani kutakuwa na process za "kufanyika" zisizo na mwisho.

Na kama haiwezekani ulimwengu kufanyika wenyewe, Hata Mungu haiwezekani afanyike mwenyewe tu.
 
Umewahi kusikia au kusoma bailojia?

Unajua bailojia nini? Inaeleza vizuri unaweza kujifunza.
Nimesha kwambia hapo kwamba binadamu sio mnyama ila ana baadhi ya sifa za wanyama hata hiyo baiolojia ina eleza hivyo.

Kusema kwamba binadamu ni mnyama kwa kulinganisha sifa chache tunazo fanana na wanyama, Ni sawa na kusema wanyama ni binadamu kwa vile binadamu wanasifa za wanyama.
 
Kwahyo Mungu maana yake ni uwepo wa hali ya juu wenye akili?
 
Nadhani tatizo ni uelewa.

Binadamu ana mwili na wanyama wengine vilevile wana mwili. Binadamu ana milango mitano ya fahamu na wanyama wengine vilevile wana milango mitano ya fahamu.

Ubora wa binadamu sio kwamba si mnyama au hana sifa zinazofanana na wanyama wengine, bali ubora wa binadamu ni ubongo wake kuwa na akili kuliko ubongo wa wanyama wengine.

Wacha nifafanue kwa kukuuliza hivi:

"Kwa nini hakuna kiumbe mwingine yeyote anayefanya uchunguzi kwenye sayari nyingine, kuzalisha chanjo za kuokoa maisha, kutunga mashairi nakadhalika, ila binadamu peke yake?

Kimsingi swali hilo halijaribu kusema wanyama wasio binadamu hawana akili. Kwa hakika wanayo. Hatahivyo akili -utambuzi au ufahamu wa wanyama wengine, ni utambuzi au ufahamu unaotokana na unaotegemea milango ya fahamu.

Neno akili tofauti na ufahamu unaotokana na unaotegemea milango ya fahamu, ni hali inayomwezesha mtu kuwa na maarifa kamilifu ya kitu au vitu, ya jambo au mambo (ushahidi wao wa ndani) jinsi yalivyo na yanavyotakiwa.
 
Pamoja na vyote ulivyo andika hapa lakini binadamu sio mnyama tunashea sifa tu na wanyama.

Na hiyo haitufanyi tuwe wanyama, bado tunabaki binadamu.

Uki elewa hili, utaacha kumlinganisha binadamu na mnyama kwenye kila kitu.
 
Hakika, akili wazo lenye akili ndio tunachotafuta na ndicho sie wenyewe tulicho.
Mkana wazo la Mungu mara nyingi kama sio zote hukana pia yeye kuwepo. Hukana kila kitu, atakana uhakika, atakana muda, atakana akili, atakana upendo. Ni watu wakumbatiao na kupendelea kutokuwepo kiasi kwamba mwisho wakiyapata mauti 'wanafurahia' kwerikweri. Maana ndicho walichokipigania maisha yao yote.

Mada moja inayojitambua sana broh.
 
Nguvu/Akili/ Mungu, Vyote hivi havipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika vipo kwa vile ni dhana za kufikirika tu zisizo katika uhalisia.
Hahahaaaaah! 😆. Seee! Nyie jamaa mnaamini sana katika kutokuwepo (kifo) na ndicho mnakipigania siku zote.

Huwa inaniacha na maswali hivi ni kwa namna gani mtu anakuwa na utayari na utamani wa kifo kwa kiwango hicho? Inashangaza sana.

Ndiyo maana wanadamu tunaaswa kuwa kamwe tusijidhanie kujua kile mtu mwingine anataka. Tutabashiri kitu kingine kumbe yeye anataka kitu kingine kabisa kinyume na hicho.

Na ndio maana Mungu akasema sitawachagulia mimi, basi ninaweka mbele yenu UZIMA na MAUTI....... Mifano ya uzima na mauti kwenye miili yetu ya nyama ni uhai na kifo....... Je? haitakishangaza mtu kuchagua kifo hapa duniani? Sasa ndugu ndio unafanya hicho katika roho, kuchagua mauti (KUTOKUWEPO)🤯🤯🤯.
 
Huyo Mungu alisema wapi?

Mungu huyo mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe.
 
Pamoja na vyote ulivyo andika hapa lakini binadamu sio mnyama tunashea sifa tu na wanyama.

Na hiyo haitufanyi tuwe wanyama, bado tunabaki binadamu.

Uki elewa hili, utaacha kumlinganisha binadamu na mnyama kwenye kila kitu.
Hicho kinachomfanya binadamu (mtu) kuwa wa kipekee kati ya wanyama wengine (akili) ndio wewe unakana.

Kwa maneno mengine, wewe mwenyewe unajikana huna ufahamu. Pia hata ujuzi wa kuandika, au kuunda au kutunga maneno, unavyoandika hapa unaukana.
 
Huyo Mungu alisema wapi?

Mungu huyo mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe.
Kiukweli hata sasa Mungu anasema na wewe kupitia KWELI hizi unazosoma humu Jf

Aepm na mie na wengine wakitype ukweli basi ujue ni Mungu anasema kupitia wao. Unanakili??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…