Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

It seems you are too young to learn.
Wewe unauliza nini kimesababisha kutokea kwa ulimwengu maana yake unataka chanzo,

Kwani ni lazima ulimwengu uwe na chanzo?

Ulimwengu ndio origin/chanzo chenyewe.
 
Nature ilivyo pangilia oxygen iwepo duniani na isiwepo kwenye sayari nyingine
๐Ÿ‘Š๐Ÿ‘Š Nature ilivyopangilia ewaaah!.

Haijalishi unamtaja Mungu kwa kutumia neno gani, unamkiri kwa imani yako kwa 'Nature'.

Basi bwana info, wewe wala huhitajiki tena kutafuta sifa za mungu achana naye. Bakia hapohapo kwenye nature, endelea kuchimba sifa za nature, tafakari nature, chunguza nature yatosha. Hukohuko utamuona Mungu. Maana sie waamini tunasema: kila sehemu ya nature ni kitabu kinachoimba sifa za Mungu. Ukimsoma mbuzi ukamuelewa utamuona Mungu, ukimsoma kondoo ukamuelewa utamuona Mungu. Jani ni surat katika kitabu cha Mungu. Go on bora, nenda endelea kuisoma nature kwa dhati utafika tu mkataa.
 
Huyo Mungu ni jina uchwara tu.

Nature ni nature haihitaji muumbaji.

Nature ipo yenyewe kama ilivyo.
 
Maelezo yote dunia ya watu wanaoamini katika Mungu huwa mna dhana moja....... Kwamba haiwezekani ulimwengu huu ulivyopangika kwa ustadi wa hali ya juu kabisa usiwe na muumbaji....... huu ndio msingi zingine ni mbwembwe tu

Kuna swali moja la msingi sana waamini Mungu huwa hamtaki kuulizwa

Kama ulimwengu huu umweumbwa kwa ustadi wa hali yajuu kiasi hiki maana yake huyo aliyeumba huu ulimwengu ni stadi kupindukia
Je ni nani alimuumba โ€œMunguโ€ huyo mwenye ustadi wa hali ya juu kiasi hicho?
Swali hili likijibika litazaa maswali yasio na mwisho....... kila kitu lazima kina chanzo

Kama hatujui Mungu katoka wapi sio lazima pia tujue ulimwengu ulitoka wapi

Kila ukijiuliza chanzo cha dunia basi jiulize pia chanzo cha chanzo cha dunia
Jinsi unavyoona Mungu hajaumbwa wala hana ulazima wa kuumbwa ndivyo wengine wanavyoona dunia aijaumbwa wala haina ulazima wakuumbwa
 
Maelezo yote dunia ya watu wanaoamini katika Mungu huwa mna dhana moja....... Kwamba haiwezekani ulimwengu huu ulivyopangika kwa ustadi wa hali ya juu kabisa usiwe na muumbaji....... huu ndio msingi zingine ni mbwembwe tu
Kimsingi ninaeleza hilo.

Kwamba ulimwengu umeumbwa, na aliyeuumba ni Mungu.

Lakini hatahivyo, huyo Mungu aliyeuumba ulimwengu maana yake ni nini? Mimi nimejibu swali hilo.

Na nimejibu kuwa Mungu maana yake ni Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili. Kwa maneno mengine, Mungu ni neno tunaloita Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili.

Maelezo yangu si zaidi ya hayo, na wala hayaelezi Uwepo Huo wa Hali ya Juu Wenye Akili Wenyewe umefanyikaje, au Wenyewe umetoka wapi, unafananaje na uliumbaje ulimwengu.

Kwa maneno mengine, mimi sisemi au sielezi akili (intelligence - the faculty of thought) imefanyikaje, bali akili ni nini. Wala sielezi akili inafananaje na au inafanyaje vitu.

Msingi wa uwepo wa Mungu kama nilivyoeleza maana ya Mungu unatokana na ulimwengu wenyewe yaani, vitu vyote vya asili vilivyopo jinsi upatano wao ulivyo wa hali ya juu na mtu anadhihirisha Uwepo Huo wa Hali ya Juu Wenye Akili.
 
Msingi wako huu wa โ€œMunguโ€ itakua hauhusi Mungu wa kwenye ancient scriptures kama Tanakh Bible Quran nk nk

Hakuna mahali popote unaweza kupata elimu ya โ€œMunguโ€ nje ya scriptures au simulizi za kidini, kwasababu nje ya dini kuna logic(sayansi)

โ€œMunguโ€ amefafanuliwa kinaga ubaga kwenye ancient scriptures ambazo hamtaki kuzitumia kuthibitisha uwepo wake badala yake mnajificha kwenye kivuli cha ulimwengu stadi ni LAZIMA umeumbwa

Hakuna Mungu nje ya ancient scriptures....... HAKUNA
scriptures zinasema Mungu yupo na amewahi kuja duniani kama Yesu watu wakampiga na mijeredi, ameongea na manabii(Bibilia), Mungu ameongea na Mudi kupitia jibrili(quran), Mungu anaonekana kama jua(greek) nk nk

Hii elimu yenu ya Mungu mnayo ingiza sayansi kuhalalisha uwepo wake hakuna kiongozi wa kidini anaitambua, sio Papa wala khalifa gani sijui, Sio Rabi wa kiyahudi wala Kirish wa kihindu
Scriptures zinata IMANI TU na sio logic.

Mnapo ona IMANI hazina MANTIKI mnaanza kumtengeneza Mungu upya na mnaacha MAANDIKO
Mnatumia nguvu nyingi kujenga hoja kwamba Mungu ni FACT na sio IMANI
 
Uwepo huo wa hali ya juu wenye ufahamu ndio huo ulimwengu wenyewe.

Kuita uwepo huo mara sijui nguvu/ Akili/ Mungu ni kupachika pachika tu majina uchwara.

Uwepo huo wenye ufahamu wa hali ya juu ndio ulimwengu.
Mh! Nakufuatilia muda sasa naona unaenda ndivyo sivyo. Kama hauafiko jambo lijengee hoja itapendeza
 
Ni kweli Scriptures ni msingi wa mafundisho ya dini licha ya kasoro mbalimbali za kidini zinazoweza kuwako.

Holy scriptures zinafunua "kweli za akili" zilizotufikia kwa njia ya imani.

Maandiko matakatifu yanaanzisha utafiti wa kisayansi: maarifa yanayofuatilia ukweli - kwa jinsi gani kweli hizo za akili zilizofunuliwa kwa njia ya imani ni ukweli; na kwa kweli dini nayo kama sayansi inamtafuta Mungu, yaani ukweli.

Kosa kubwa ni kufikiri kwamba sayansi inapinga imani (dini) au kwamba imani (dini) inapinga sayansi. Huwezi kuachanisha imani (dini) na sayansi: wakati wote palipokuwa na dini na sayansi pia ilikuwepo.
 
Hapo sawa.

Mimi ninacho pingana na watu sana sana ni kudai kwamba sisi binadamu tuliumbwa na hiyo nature ambayo kiimani mnaiita mungu, ilhali hata sisi binadamu wenyewe ni nature hiyohiyo.
Mimi nliumbwa na Mungu,
 
Kiukweli hata sasa Mungu anasema na wewe kupitia KWELI hizi unazosoma humu Jf

Aepm na mie na wengine wakitype ukweli basi ujue ni Mungu anasema kupitia wao. Unanakili??
Mkuu bado upo kwenye kifungo cha imani na wewe pia ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Mungu angekuwepo kweli kama anavyonadiwa kwenye vitabu vya dini wala huu mjadala usingekuwepo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ