Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo!
1. Mwezi huu uwe mwezi wenye Baraka na Neema ya Mungu naam yule MUNGU Mwenye Nguvu nyingi aliyetuumba wote.
2. Mwezi huu Mungu atuepushe na Mabaya na kushindwa na adui zetu.
3. Wokovu wa Mungu uwe upande wetu. Naye atatupa Wokovu mkuu na ushindi kwa namna isiyoelezeka.
4. Adui zetu watachanganyikiwa na kuwa na hofu kuu na kuanguka mara elfu wao na vibaraka wao.
5. Eeh Mola wetu Mlezi, Mungu muumbaji. Mfalme wa majeshi. Mungu mwenye nguvu. Sisi watoto wako. Imetupasa kukuamini na kukuabudu wewe peke yako. Tunakiri mara kadhaa tumekuwa tukikukosea lakini bado wewe ni Mungu wetu. Tusamehe kwa Makosa yetu ikiwemo kosa la kuogopa na kuabudu Sanamu, kuabudu shetani na vibaraka wake.
6. Tuepushe sisi na watoto wetu na laana yako ya kutoipenda Haki yako. Kutoitetea Haki yako. Kutopinga dhulma na uonevu kutokana na kuogopa Sanamu. Eeh Mola wetu. Tusamehe Sana na laana hiyo.
7. Kamwe tusibaki kimya kutetea Haki. Kamwe tusibaki kimya kukemea dhulma na waovu. Usije ukatulaani kwa kushindwa kufanya hivyo. Maana umewalaani wale wote wanaoshindwa kuipenda haki na kuitetea haki na kupinga maovu.
8. Tunakuamini. Tupo moyo wenye nguvu. Tunajua wokovu wako haututegemei sisi. Tunachoomba ni hekima na subira yako. Pia utupe akili ya kuona mapenzi yako.
9. Wasaidie na bariki wale wote ambao wao wamekuwa mstari wa mbele kuipigania haki popote pale walipo. Wao na familia zao wabariki. Wasamehe kwa mapenzi yako makosa yao. Ujasiri na kujitoa kwa muhanga visiende bure.
10. Tunahitaji taifa letu liwe na HAKI ili tuweze kuishi kwa AMANI. Eeeh Mola wetu wewe ndiye ujuaye utafanya nini kuweka mambo sawa.
11. Tunakuamini. Tutakusapoti Mungu wetu kwa maamuzi yoyote utakayofanya hata kama yatatugharimu ikiwa ni mapenzi yako.
12. Wape watu wako moyo wa ujasiri na ushujaa katika kuona mapenzi yako.
13. Mwezi huu uwe mwezi wenye Baraka. Haki yako itufunike na kutulinda.
14. Yote yafanyike kwa Mapenzi yako. Amini.
Nawatakia Mwezi mpya. Mungu Mkuu awe nanyi.
Tusameheane.
Tukae pamoja tuwekane sawa.
Aliyedhulumiwa apewe haki yake.
Waliodhulumu wajinyenyekeze na wawajibike.
Wasiwe na kiburi kusubiri kuona Huyo Mungu mkuu atafanya nini.
Tunataka mwezi huu uwe wa Baraka.
Ukaidi, jeuri na kiburi ndiyo mambo ambayo Mungu anayapenda anapotaka kumnyoosha MTU na kumuangamiza. Hekima na Neema ya Mungu ziwe juu ya Kila mmoja atakaye Amani kwa njia ya HAKI.
Na wala sio Amani kwa njia ya Dhulma.
Acha nipumzike sasa.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam