Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Wamisionari walitisha watu (hasa waafrika) kuna moto wa milele ili waikubali Imani ya kizungu. Hata mimi niliogopa moto wa milele na kubatizwa. Sasa nimegundua ni fix, nimeamua kurudi kwenye jadi yangu.
Umerudia dhambi?
 
Kuna vitu hatuvioni kwa macho, je ndiyo tuseme havipo? mfano upepo,mawimbi ya sauti,electronic signals etc . Wewe kutokumuona Mungu haimaanishi hayupo
Vitu vyote ulivyovitaja vipo kwenye dimension yetu ni tofauti na Mungu unayemuongelea.

Mungu hayupo kwenye dimension yetu ndiyo maana ni ngumu kumuelezea.

3 main dimensions: Time, Space & Matter.

Kutoka kwenye Biblia Mwanzo 1:1

"Hapo mwanzo, (time) Mungu aliumba mbingu (space) na dunia (matter).

Kwa maana hiyo huwezi kuelezea uwepo wa Mungu kwa kutumia kitu chochote kile kilichopo kwenye ulimwengu wetu kwasababu Mungu kwenye Biblia yeye ndiyo aliumba Time, Space & Matter.
 
Muanzisha uzi ni Agnostic Atheist. Bado ana maswali mengi ambayo yanafanya anashindwa kuelewa asimame wapi kwasababu tokea akiwa mdogo ameshakuwa brainwashed na dini.

Ndio maana nilimwambia awe honestly. Hii nyuzi inaonyesha jinsi gani anavyojua kwamba mungu ni stori za kutungwa lakini bado anashindwa ku confess.
 
Mimi sifahamu fika chanzo cha huo ulimwengu.

Na naamini hakuna ajuaye zaidi ya nadharia tu,

Wewe unaweza kuwa unajua chanzo cha hayo uliyoyasema ili unieleze nami nisiwe mjinga tena!?
Na hivi ndiyo jinsi mwanadamu alivyozaliwa akiwa hajui chochote.

Mimi bado sielewi lengo kuu la dini ni nini ikiwa kuna miungu karibu 3000 na yote ina waumini.

Wote wanaotetea dini ni wanafiki kwasababu ni imani walizochukua kutoka kwa wazazi au walezi, hakuna ambaye hujichagulia dini zaidi ya kufuata tu.

Leo hii mtoto akizaliwa na kukulia kwenye Ukristo ataamini ndiyo dini sahihi ni hivyohivyo kwa mtoto wa Kiislam na dini zote hizi zinakinzana.

Muislam ni sawa kuoa mpaka wake 4 ila mkristo haruhusiwi kuoa mke zaidi ya 1.

Wote hawa ni binadamu wanafanana lakini wanakinzana kiimani ktk miungu wanayoamini. Sasa kwanini Mungu aliyetuumba awe na njia nyingi hivi kutuchanganya wanadamu.
 
Paganism ni tofauti na Atheism.

Wapagani wanaamini miungu tofauti na zile dini kuu: Ukristo, Uislam n.k.

Wapagani hawamuamini Mungu unayemuamini wewe kama ambavyo wewe humuamini Mungu wao.

Atheists hawaamini kabisa uwepo wa Mungu yoyote yule.

Kwanini wewe unajihisi upo sahihi kukataa miungu yote na kuamini wa kwako ndiyo wa kweli?

Ukiwa Muislam maana yake huamini Mungu wa Wakristo, ni hivyohivyo ukiwa Mkristo pia. Sasa hapo kwanini unamshangaa mpagani? Au Atheist anayewakataa wote.

😂
 
Nimechagua kuiamini biblia as my reference kama wewe ulivyochagua kuviamini vyanzo unavyovitumia ingawa hujanieleza ni reference zipi ulizotumia mpaka kusema biblia ni fiction stories
Jibu hili swali kwa ukweli wako wote.

Kwanini ulikuwa Mkristo?

Kama jibu lako ni "kwasababu ya wazazi" usijibu hilo swali jibu hili:

Unaamini ungezaliwa na wazazi Waislam au dini yoyote ile bado ungekuwa Mkristo?
 
Jibu hili swali kwa ukweli wako wote.

Kwanini ulikuwa Mkristo?

Kama jibu lako ni "kwasababu ya wazazi" usijibu hilo swali jibu hili:

Unaamini ungezaliwa na wazazi Waislam au dini yoyote ile bado ungekuwa Mkristo?

Ndiyo
 
Mkuu ukitaga kutegua kitendawili hicho kama ulizaliwa kwenye imani, lazima ufanye self diagnosis ya ubongoni mwako kwa kujiuliza maswali kama haya.

Hili huwa swali la kwanza mtu anapaswa kujiuliza.

Kwanini anapondea upande wa pili ambao hauamini?

Vipi kama ingetokea akazaliwa kwenye upande wa pili ambao kwasasa hauamini, je asingekuwa anaponda ule upande aliosasa?

Vipi kama angezaliwa japani huko ama kwenye ubudha?

 
 
Nimechagua kuiamini biblia as my reference kama wewe ulivyochagua kuviamini vyanzo unavyovitumia ingawa hujanieleza ni reference zipi ulizotumia mpaka kusema biblia ni fiction stories
Ni fiction stories kwasababu inahadithi za uongo wa wazi kabisa halafu inajipinga yenyewe.

Hadithi za nyoka kuongea

Hii unaitofautisha vipi na ile hadithi ya Pazi na jogoo?,
Unaitofautisha vipi na hadithi ya nani atamvika paka kengele?
Unaitofautisha vipi na hadithi ya sungura na fisi!?

Si ajabu hata hujui history ya biblia.
 
Huyo anayesema hivi ni mpumbavu.
Na nahsi namfahamu

Hakuna kitu kama hiko.

Huyo Mungu wa design hiyo itoshe tu kusema kuwa ni mpumbavu.

Kujidhihirisha kwako ni kwa kuumiza watu na vichanga?

Si mnasemaga kuwa watu wana free will ya kuchagua.

Sasa iwaje tena huyu Mungu akasirishwe eti kisa hapendi dhambi na uovu!?

Is God frustrated?
Au ni Coma hiyo

I think he is going through a traumatic divorce. Who knows...
Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote alishindwa vipi kuumba ulimwengu usioruhusu kuwezekana kwa dhambi na uovu?
 
Ninyi mlio na asili Kutoka CHINI, Wana wa Mungu wakiwafuata, watapotea mazima!!!
 
Wanakutisha hivyo kwamaana Allah hayupo.

Huwezi kuchunguza kisichokuwepo.

Dini zinatumia mbinu ya kutisha watu ndo waamini.

Huu ni uthibitisho mwingine kuwa Allah amaye ni muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.

Ingawaje hataki kujionesha, Inakuwaje Allah akose mbinu bora ya kuwafanya watu wamwamini ?

Yaani kwa sifa alizonazo kweli Mungu anaishiwa mbinu?
 
Ninyi mlio na asili Kutoka CHINI, Wana wa Mungu wakiwafuata, watapotea mazima!!!
Huyo Mungu haishi nje ya hadithi za vitabu vyenu.

Kama unabisha thibitisha uwepo wake tujue kweli yupo kwenye uhalisia.
 
Huyo Mungu haishi nje ya hadithi za vitabu vyenu.

Kama unabisha thibitisha uwepo wake tujue kweli yupo kwenye uhalisia.
Mungu huyo anaishi ndani yangu.

Ninaongea naye kupitia maombi na kusoma Neno lake.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Mungu huyo anaishi ndani yangu.

Ninaongea naye kupitia maombi na kusoma Neno lake.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
Hujaweza kuthibitisha zaidi ni kuwa umenihubiria tu

Mahubiri maana yake ni kamba za kufungia kondoo
 
Huyo Mungu haishi nje ya hadithi za vitabu vyenu.

Kama unabisha thibitisha uwepo wake tujue kweli yupo kwenye uhalisia.
Siku Theist akiweza kujibu kwanini kuna dini na miungu mingi lakini anaamini Mungu wake ndiyo wa kweli nitaweza kumsikiliza.

Hawana points za msingi zaidi ya kutetea dini zao tu. Theist haamini Mungu mwingine bali wa kwake ila Atheist akisema basi mimi siwaamini wote anaonekana anakosea.
 
Mungu huyo anaishi ndani yangu.

Ninaongea naye kupitia maombi na kusoma Neno lake.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
Kwahiyo Waislamu na waumini wa dini nyingine zote duniani wataenda motoni maana Mungu wao ni wa uongo?
 
Imani ni shambulio la akili.

Reasoning na logic haifanyi kazi kwa wafia dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…