Mungu na Allah mbona wana itikadi tofauti? Je, ni wamoja au pande mbili zinazokinzana?

1. Kitabu halisi Kiko wapi? (Nani alithibisha hiko ni halisi na kile sio? Na kwanini tumuamini?)

2. Alitabiriwa na nani? wapi?

3. Injili ipi kati ya zile nne imemtaja Muhammad?

4. Mungu anatabiriwa vipi wakati yupo na aliabudiwa tangu kale?

5. Mungu aliyeabudiwa na wakristu anafanana nini na wa Muhammad

6. Wangu ni ujinga na chuki kwa muktadha upi? Thibitisha kama sijui nilichoandika

7. Kwanini nilichoandika kiwaumize waislamu?
 
 
mkuu we ndo unatuchanganya
 
Mungu na Allah ni mmoja yaani mwanzo, ndiye aliyeandikwa katika vitabu kuwa ni mwanzo na mwisho.

Ufunuo 22:13
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

Ila huyu mwanzo alipewa asimamie uumbaji na Muumba yaani THE REAL SOURCE asiye na mwanzo wala mwisho ila ulitekwa nyara akaabudiwa mwengine kabisa,wachache kwa kujua(falme na mamlaka) na wengi kwa kutojua.

Matendo 19:27
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi, kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.

Ile upate uelewa kunatofauti kati ya Mwanzo na Chanzo, kwa kingereza Genesis na The Source,mwanzo hata yeye aliumbwa.

Wengi tulimjua zaidi mwanzo (Mwenyezi,Allah,Mola,Yehova,niko ambae niko,Mungu wa majeshi,Mungu wa ibrahim,Mungu wa daniel, Mungu wa Daudi, Alfa na Omega)ambapo ndo ameandikwa kwenye vitabu vya dini.

Ila Chanzo Halisi ni mmoja tu (hagawanyiki) na yeye hana mwanzo wala mwisho na hana dini bali wote tumetoka kwake na lazima turejee kwake.

👇🏾Hii ni baadhi ya mistari michache iliyoelezea majira yake ikifika itakuwaje.

Warumi 11:36
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele.

Zekaria 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
 
Kama Kweli nia yako ni Kujifunza.

1. Wakristo wa Middle East wanamuita Mungu Allah
2. Wakristo wa Middle East hata kabla ya kuja Mtume Muhammad (s.a.w) wanamuita Mungu Allah, na Ukristo na uyahudi umeanzia Middle East.
3. Semitic language nyengine kama Aramaic ambayo Aliongea Yesu anaitwa Elaha, na Syriac inatamkwa Alaha zote hizi ni lugha kongwe zilizotumika wakati wa mitume.

So Allah maana yake ni The God ama kiswahili Mungu mmoja, ni neno linalotumika na Monotheist kumaanisha Mungu ni mmoja thats it, Halijaanzia kwenye uisilamu wa Muhammad (s.a.w) lipo enzi na enzi.

Ni kama vile mimi nilete Ubishi wa Kijinga kwamba Yesu na Jesus ni vitu viwili tofauti.
 
comment ndefu ujinga mtupu, Akisoma mwarabu mkristo lazima acheke, umeshawahi hata kuuliza Biblia ya Kiarabu neno Mungu linaandikwaje?


Hii picha hapa chini sio Quran bali ni page ya Biblia ya Kiarabu
 


JEHOVAH VS ALLAH.

Ni tofauti kabisa.
 
Allah hukaa kwenye anga (nyota na mwezi). Watumishi wake ni majini! Lugha yake kiarabu

"Allah" katika Biblia ametafsiriwa katika kitabu cha Efeso 2:2 kuwa ni mfalme wa uweza wa anga anayefanya kazi katika wana wa kuasi

Waefeso 2:2
[2]ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…