Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Mungu yupo maana Dunia haiwezi kujitengeneza yenyewe na viumbe vyake na kila kiumbe kina sababu yake...
Ila uwepo wa Mungu yapo Mataifa makubwa na baadhi ya watu wanafanya fursa ndio maana wengine wanabaki kutokuamini...
 
Mungu ni asili, yeye ndiyo chanzo cha vyote vinavyoonekana na visivyo onekana.
Ili Mungu akure maarifa, hana haja ya kukuandikia kiatabu.

Jiulize maarifa makubwa waliyonayo wanyama mbalimbali, wameyasoma kwenye kitabu gani kitakatifu?

Mungu yupo, hasomi, haandiki, wala hana dini. Dini ni mpango wa mwanadamu. Dini imejaa vitisho, Mungu hana haja ya kumtisha mtu.

Dini zimeenezwa kwa kufanya mauaji makubwa. Mungu wetu anachukia mauaji.

Dini ni mpango halisi wa shetani, kuwadanganya watu, wajione wanamfuata Mungu kumbe wako maili nyingi sana na mpango wa Mungu kwa mwanadamu.

Kama dini haiwezi kukupeleka Kariakoo, itawezaje kukupelela mbinguni?

Ukiweza kumpenda jirani yako kama nafsi yako mwenyewe wewe utakuwa bora kuliko mtu anayesali kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Upendo ndio kusudi la mwanadamu kuwepo duniani. Tukipendana kwa dhati, dunia ndio Paradiso yenyewe.
Wakati mwingine ukisha andika uwe unasoma uliyoyaandika kabla ya kuyaleta hapa
 
Uko sahihi.Mungu hajaumba dini.Jinsi unavyomuona mtoto mdogo alivyo ndivyo jinsi ambavyo binadamu tumeumbwa kabla yakufundishwa dini.Mtoto mdogo ana kila kitu ambacho Mungu amemuumba nacho,kinachokuja kuongezeka kwake nivyakibinadamu,dini,pesa,chuki,ndoa na ujinga.hayo anakutana nayo ukubwani.lakini upendo,uzazi,karama,kipaji,thaman ya uhai anazaliwa navyo kwasababu viko ndani yake toka kuumbwa nahivyo utavipata kwa viumbe vyote hai ambavyo havijui Dini ni nini.
 
Upo sahihi kabisa
Dini ni mradi kama zilivyo project nyingine na hutumika kwa malengo mbalimbali kama kutawala akili za watu, kutisha na kuwaletea watu hofu pamoja na kuwagawanya watu ili iwe rahisi kuwamudu na kuwaswaga kama ngombe, mbuzi au kondoo.

Halikadhalika dini zote ni matawi ya Serikali duniani kuhakikisha waumini wanafuata na kutii Sheria na kuheshimu mamlaka.
 
Eti kuna moto wa milele ameuandaa Mungu huyo Mungu gani anampango wa kuwafanya mishikaki watoto zake wapenzi
Ukifanya dhambi/maovu au ukimkosea binadamu mwenzako nature itakuadhibu hapa hapa duniani wala hakuna moto.
 
Back
Top Bottom