Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Hivyo vitabu vingine havina stori ya uwepo wa mungu mwenye nguvu, mungu mjua yote, mungu mwenye upendo wa dhati ambae anakupenda sana ila atakuchoma moto. Havina.
Kwahiyo hiyo kama Mungu wa kwenye Qur'an na Biblia asingeelezwa kwa hizo sifa (za upendo wote,uwezo na mwenyewe nguvu)ingekuwa Mungu huyo kuwepo?
 
Uliza maswali ya maana kidogo basi kiongozi
Mkuu hii hoja yenu ya kusema Mungu wa Qur'an na Biblia hayupo haileti maana, Mungu ni Mungu tu hivyo vitabu vinaelezea ya kumuhusu huyo Mungu sasa kama kuna maelezo kwenye hivyo vitabu ambayo unaona sio sahihi ungesema kuna maelezo yasio sahihi kuhusu Mungu kwenye hivyo vitabu sio kusema Mungu wa biblia na qur'an hayupo kwangu haileti maana.
 
Labda nikuulize huyo Mungu wewe ulimjua tu mwenyewe uwepo wake( kama ulivyojua kunyonya titi la mama) au uwepo wa anayeitwa Mungu ulijua kupitia watu?
Kabla ya yeye kumjua Mungu hakua anaishi? Aliwezaje kuishi pasipo kumjua Mungu?

Dini ni utapeli Mungu yupo lakini dini ni utapeli
 
NAJIULIZA KITU KIMOJA HIVI ALIYEANDIKA KWAMBA HAPO MWANZO MUNGU ALIWAUMBA ADAM NA HAWA YEYE ALIJUAJE NA KIPINDI HAO ADAM NA HAWA WANAUMBWA YEYE ALIKUWA WAPI NA ALIUMBWA NA NANI.
 
Mungu ni asili, yeye ndiyo chanzo cha vyote vinavyoonekana na visivyo onekana.
Ili Mungu akure maarifa, hana haja ya kukuandikia kiatabu.

Jiulize maarifa makubwa waliyonayo wanyama mbalimbali, wameyasoma kwenye kitabu gani kitakatifu?

Mungu yupo, hasomi, haandiki, wala hana dini. Dini ni mpango wa mwanadamu. Dini imejaa vitisho, Mungu hana haja ya kumtisha mtu.

Dini zimeenezwa kwa kufanya mauaji makubwa. Mungu wetu anachukia mauaji.

Dini ni mpango halisi wa shetani, kuwadanganya watu, wajione wanamfuata Mungu kumbe wako maili nyingi sana na mpango wa Mungu kwa mwanadamu.

Kama dini haiwezi kukupeleka Kariakoo, itawezaje kukupelela mbinguni?

Ukiweza kumpenda jirani yako kama nafsi yako mwenyewe wewe utakuwa bora kuliko mtu anayesali kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Upendo ndio kusudi la mwanadamu kuwepo duniani. Tukipendana kwa dhati, dunia ndio Paradiso yenyewe.
Nakazia
 
Naona swali la msingi unalikwepa kila ukijaribu kuulizwa.

Swali:
Mungu na Concept mzima ya Mungu imeletwa na kuelezewa na hizo Dini na sisi wote tumejua kuna Mungu kupitia hizo Dini, kwa kifupi God issues is religious things, sasa wewe hapa unasema unaamini kuna Mungu ila huamini Dini hizo zilizokuletea Cocept ya huyo Mungu mbona kama haingii akilini.

Muelezee huyo mungu anayemuamini wewe ambae si wadini yeyote, umemjulia wapi, ameamrisha nini, kupitia nini umepata hayo maamrisho au miongozo yake na nini ESSENCES ya hio miongozo wa huyo mungu unayemuamini wewe....na inakuwaje huyo mungu awe na miongozo fulani bila kuwa na mfumo unayesimamia hio miongozo ambapo pale juu mfumo huo unaitwa Dini.

nadhani ungeeleza mambo haya kwa kina tukuelewe.
 
Hivi ulisha wahi kujiuliza viumbe vilivyomo mwilini mwako huwa vinakutambua ww km nani??.Unaweza kuta navyo vinakuita Mungu ama vinakutambua kama muumbaji maana km vikisikia kiu,njaa,kulala,kutoa uchafu,kustarehe ww lazima huku nje upate shida,mfano ni lazima ule ulale unywe maji ili tu viumbe walioko ndani yako wapate mahitaji yao waishi.Ww mtu ukiacha kufanya hivyo viumbe walioko ndabi yako wanaanza kufa na ww pia mtu lazima ufe tunaishi kwa kutegemeana.
Jambo fikirishi..na sisi inaweza tukawa tunaishi ndani ya kiumbe kikubwa ndo maana na sisi hiki kiumbe dunia kisipo tupa mazao ama mvua ama hewa safi kwa wakati lazima sisi viumbe ndani yake tunakufa.
Wazo langu mm ni kwamba inawezeka Mungu ..ama huyo mwenye vyote yuko nje ya uishi wetu sisi viumbe wadogo na hana mda kabisa na sisi km sisi tusivo na mda na viumbe wa mwilini mwetu.maana hakuna anaejua kua vinasali sala tano ama jumapili.Chanzo cha vyote anacho jali ni kwamba tupo kuendeleza uwepo wetu..Inawezekana pia kuna viumbe wakubwa zaidi yetu hao sasa ndo hua wanamuomba huyo Mwenye vyote.
 
Dini nyingine zinasema Mungu hafanani na Chochote yani Mungu hali wala hanywi.sasa ili uweze kuongea unahitaji Mdomo Ulimi na Voice box na Mdomo umewekwa kwa ajili ya kula na kunywa halafu baadae ndio tukaanza kuutumia kwa ajili ya kuguna na kutoa sauti na baadae kuongea.

Sasa unaposema Mungu kaongea na fulani wakati huohuo unasema Mungu hali hanywi huko sio kujipiga pini kweli?
 
Naona swali la msingi unalikwepa kila ukijaribu kuulizwa.

Swali:
Mungu na Concept mzima ya Mungu imeletwa na kuelezewa na hizo Dini na sisi wote tumejua kuna Mungu kupitia hizo Dini, kwa kifupi God issues is religious things, sasa wewe hapa unasema unaamini kuna Mungu ila huamini Dini hizo zilizokuletea Cocept ya huyo Mungu mbona kama haingii akilini.

Muelezee huyo mungu anayemuamini wewe ambae si wadini yeyote, umemjulia wapi, ameamrisha nini, kupitia nini umepata hayo maamrisho au miongozo yake na nini ESSENCES ya hio miongozo wa huyo mungu unayemuamini wewe....na inakuwaje huyo mungu awe na miongozo fulani bila kuwa na mfumo unayesimamia hio miongozo ambapo pale mfumo huo unaitwa Dini.

nadhani ungeeleza mambo haya kwa kina tukuelewe.
Bado nasisitiza Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Tulianza kumuabudu Mungu kabla hata dini hazijaja. Wanyakyusa Mungu wanamwita Kyala, Wasukuma wanamwita Seba, Wanyihaa wanamwita Mulungu.

Wazee wetu walimwomba Mungu naye akawajibu kabla hata dini hazijaja.
Dini zimeleta uongo mwingi na kuharibu kabisa ufahamu na uelewa wetu juu ya Mungu.
 
Bado nasisitiza Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Tulianza kumuabudu Mungu kabla hata dini hazijaja. Wanyakyusa Mungu wanamwita Kyala, Wasukuma wanamwita Seba, Wanyihaa wanamwita Mulungu.

Wazee wetu walimwomba Mungu naye akawajibu kabla hata dini hazijaja.
Dini zimeleta uongo mwingi na kuharibu kabisa ufahamu na uelewa wetu juu ya Mungu.
Ndiyo ukweli,umakini tu
 
Labda nikuulize huyo Mungu wewe ulimjua tu mwenyewe uwepo wake( kama ulivyojua kunyonya titi la mama) au uwepo wa anayeitwa Mungu ulijua kupitia watu?
Mungu hata usipoenda kanisani au msikitini utajua tu yupo...Mungu anaongea na sisi muda wote..ni vile tunsjitoa ufahamu...Ndo maana huhitaji mtu akuambie hiki ni kibaya, kuna sauti ndani iko wazi sana...
Hata babu zetu kabla ya ukristu au uislam walijua kuna nguvu ipo ndo maana wakawa wanaenda kutambika kwenye miti, mapango, wanaomba mvua n.k
 
Back
Top Bottom