Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Mungu hata usipoenda kanisani au msikitini utajua tu yupo...Mungu anaongea na sisi muda wote..ni vile tunsjitoa ufahamu...Ndo maana huhitaji mtu akuambie hiki ni kibaya, kuna sauti ndani iko wazi sana...
Hata babu zetu kabla ya ukristu au uislam walijua kuna nguvu ipo ndo maana wakawa wanaenda kutambika kwenye miti, mapango, wanaomba mvua n.k
Issue sio kwenda kanisani au msikitini bali tunajua uwepo wa Mungu kupitia watu kwa bila kujali watu hao wa dini au sio wanadini.
 
Kaka..., au basi!
Mungu ni asili, yeye ndiyo chanzo cha vyote vinavyoonekana na visivyo onekana.
Ili Mungu akure maarifa, hana haja ya kukuandikia kiatabu.

Jiulize maarifa makubwa waliyonayo wanyama mbalimbali, wameyasoma kwenye kitabu gani kitakatifu?

Mungu yupo, hasomi, haandiki, wala hana dini. Dini ni mpango wa mwanadamu. Dini imejaa vitisho, Mungu hana haja ya kumtisha mtu.

Dini zimeenezwa kwa kufanya mauaji makubwa. Mungu wetu anachukia mauaji.

Dini ni mpango halisi wa shetani, kuwadanganya watu, wajione wanamfuata Mungu kumbe wako maili nyingi sana na mpango wa Mungu kwa mwanadamu.

Kama dini haiwezi kukupeleka Kariakoo, itawezaje kukupelela mbinguni?

Ukiweza kumpenda jirani yako kama nafsi yako mwenyewe wewe utakuwa bora kuliko mtu anayesali kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Upendo ndio kusudi la mwanadamu kuwepo duniani. Tukipendana kwa dhati, dunia ndio Paradiso yenyewe
 
Hivi ulisha wahi kujiuliza viumbe vilivyomo mwilini mwako huwa vinakutambua ww km nani??.Unaweza kuta navyo vinakuita Mungu ama vinakutambua kama muumbaji maana km vikisikia kiu,njaa,kulala,kutoa uchafu,kustarehe ww lazima huku nje upate shida,mfano ni lazima ule ulale unywe maji ili tu viumbe walioko ndani yako wapate mahitaji yao waishi.Ww mtu ukiacha kufanya hivyo viumbe walioko ndabi yako wanaanza kufa na ww pia mtu lazima ufe tunaishi kwa kutegemeana.
Jambo fikirishi..na sisi inaweza tukawa tunaishi ndani ya kiumbe kikubwa ndo maana na sisi hiki kiumbe dunia kisipo tupa mazao ama mvua ama hewa safi kwa wakati lazima sisi viumbe ndani yake tunakufa.
Wazo langu mm ni kwamba inawezeka Mungu ..ama huyo mwenye vyote yuko nje ya uishi wetu sisi viumbe wadogo na hana mda kabisa na sisi km sisi tusivo na mda na viumbe wa mwilini mwetu.maana hakuna anaejua kua vinasali sala tano ama jumapili.Chanzo cha vyote anacho jali ni kwamba tupo kuendeleza uwepo wetu..Inawezekana pia kuna viumbe wakubwa zaidi yetu hao sasa ndo hua wanamuomba huyo Mwenye vyote.
Critical thinking
 
Naona swali la msingi unalikwepa kila ukijaribu kuulizwa.

Swali:
Mungu na Concept mzima ya Mungu imeletwa na kuelezewa na hizo Dini na sisi wote tumejua kuna Mungu kupitia hizo Dini, kwa kifupi God issues is religious things, sasa wewe hapa unasema unaamini kuna Mungu ila huamini Dini hizo zilizokuletea Cocept ya huyo Mungu mbona kama haingii akilini.

Muelezee huyo mungu anayemuamini wewe ambae si wadini yeyote, umemjulia wapi, ameamrisha nini, kupitia nini umepata hayo maamrisho au miongozo yake na nini ESSENCES ya hio miongozo wa huyo mungu unayemuamini wewe....na inakuwaje huyo mungu awe na miongozo fulani bila kuwa na mfumo unayesimamia hio miongozo ambapo pale juu mfumo huo unaitwa Dini.

nadhani ungeeleza mambo haya kwa kina tukuelewe.
Mungu anajulikana kabla hizi dini za kutoka mashariki ya kati hazijatufikia. Kila jamii na kabila walikuwa na Mungu wao. Bahati mbaya hawa wanakuja walipokuja wakawadanganya mababu na mabibi zetu kwamba wao wanaabudu na kuamini mizimu
 
Mungu yupo maana Dunia haiwezi kujitengeneza yenyewe na viumbe vyake na kila kiumbe kina sababu yake...
Ila uwepo wa Mungu yapo Mataifa makubwa na baadhi ya watu wanafanya fursa ndio maana wengine wanabaki kutokuamini...
Hoja yako inamaanisha kwamba kila kilichopo kimetengenezwa na kilichokuwepo kabla. Ndio maana unasema Mungu yupo kwasababu dunia haiwezi kujitengeneza yenyewe. Je, huyo Mungu ilikuwaje akatokea? Alitoka wapi na lini? Je huyo Mungu alitokea mwenyewe bila kuwa na chanzo?
 
Mungu ni asili, yeye ndiyo chanzo cha vyote vinavyoonekana na visivyo onekana.
Ili Mungu akure maarifa, hana haja ya kukuandikia kiatabu.

Jiulize maarifa makubwa waliyonayo wanyama mbalimbali, wameyasoma kwenye kitabu gani kitakatifu?

Mungu yupo, hasomi, haandiki, wala hana dini. Dini ni mpango wa mwanadamu. Dini imejaa vitisho, Mungu hana haja ya kumtisha mtu.

Dini zimeenezwa kwa kufanya mauaji makubwa. Mungu wetu anachukia mauaji.

Dini ni mpango halisi wa shetani, kuwadanganya watu, wajione wanamfuata Mungu kumbe wako maili nyingi sana na mpango wa Mungu kwa mwanadamu.

Kama dini haiwezi kukupeleka Kariakoo, itawezaje kukupelela mbinguni?

Ukiweza kumpenda jirani yako kama nafsi yako mwenyewe wewe utakuwa bora kuliko mtu anayesali kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Upendo ndio kusudi la mwanadamu kuwepo duniani. Tukipendana kwa dhati, dunia ndio Paradiso yenyewe.
Freedom of speech.Anyway kuna kitu hujakifahamu bado about human nature to his/her Creature.Ukiwa mkubwa utaelewa.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom