Mungu na dini ni vitu viwili tofauti. Mungu hasomi wala haandiki

Mungu yupo maana Dunia haiwezi kujitengeneza yenyewe na viumbe vyake na kila kiumbe kina sababu yake...
Ila uwepo wa Mungu yapo Mataifa makubwa na baadhi ya watu wanafanya fursa ndio maana wengine wanabaki kutokuamini...
 
Wakati mwingine ukisha andika uwe unasoma uliyoyaandika kabla ya kuyaleta hapa
 
Uko sahihi.Mungu hajaumba dini.Jinsi unavyomuona mtoto mdogo alivyo ndivyo jinsi ambavyo binadamu tumeumbwa kabla yakufundishwa dini.Mtoto mdogo ana kila kitu ambacho Mungu amemuumba nacho,kinachokuja kuongezeka kwake nivyakibinadamu,dini,pesa,chuki,ndoa na ujinga.hayo anakutana nayo ukubwani.lakini upendo,uzazi,karama,kipaji,thaman ya uhai anazaliwa navyo kwasababu viko ndani yake toka kuumbwa nahivyo utavipata kwa viumbe vyote hai ambavyo havijui Dini ni nini.
 
Upo sahihi kabisa
Dini ni mradi kama zilivyo project nyingine na hutumika kwa malengo mbalimbali kama kutawala akili za watu, kutisha na kuwaletea watu hofu pamoja na kuwagawanya watu ili iwe rahisi kuwamudu na kuwaswaga kama ngombe, mbuzi au kondoo.

Halikadhalika dini zote ni matawi ya Serikali duniani kuhakikisha waumini wanafuata na kutii Sheria na kuheshimu mamlaka.
 
Eti kuna moto wa milele ameuandaa Mungu huyo Mungu gani anampango wa kuwafanya mishikaki watoto zake wapenzi
Ukifanya dhambi/maovu au ukimkosea binadamu mwenzako nature itakuadhibu hapa hapa duniani wala hakuna moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…