Mungu na shetani kushirikiana kumtesa Ayubu ni ushahidi tosha kama Mungu na Shetani ni Marafiki. ndio maana Mungu hamuui shetani mpaka leo

Shetani alikua anaitwa shetty😀
 
Hatari
 
Haya tueleweshe sasa hilo andiko lilikua na maana gani?
 
Tunafundishwa kwamba Mungu ni Mtakatifu sana na kamwe kiumbe chenye dhambi hakiwezi kujihudhurisha mbele yake. Vipi tena shetani aliye baba wa ubaya wote na mwanzilishi wa dhambi aweze kwenda mbele ya Mungu na kupiga naye stori kama vile ni washikaji?

Mimi ni Mkristo lakini hata Wanatheolojia wengi wanakiri kuwa hili fundisho lina utata. Nasubiri ufafanuzi wako wa kina bila kejeli, matusi wala dhihaka 🙏🏿
 
Mbona umechelewa kujua km hao ni marafiki mkuu… ni vile wanatuona km Matraco yao 😹😹😹
Acha dada yangu
Acha kufuata mkumbo wa hawa vijana wa humu ndani

MUNGU anakupenda sana
YESU ni mwema sana
 
Wakati anamjaribu ayubu alikuwa haitwi shetani, haya hebu tuambie alikuwa anaitwa nani tujue.

Naomba jibu langu haraka.
 
Hizo ni hadithi za kufikirika za kutungwa na watu tu, hakuna Mungu wala Shetani.

Hizo ni hadithi za watu tena zenye makosa mengi ya kimantiki, zilizobadilishwabadilishwa mara nyingi na waandishi wake.

Ni hekaya na ngano za Wayahudi, mmepigwa ukoloni wa kiutamaduni kuaminishwa Mungu aliyetungwa na Wayahudi
 
Kufuru kubwa. Tubu ndugu before It s too late.
 
Wakati Mungu anamwambia yote hayo shetani Nani alimuona?

What am saying is tatizo lipo kwako mtoa mada
 
Kwani wewe huwezi kuongea na adui yako? Bila shaka inawezekana, shetani anasubiri hukumu ya Mungu.
 
Shetani sio kwamba anapiga storu na Mungu, Shetani siku zote anatushitaki kwa Mungu, ndio maana ilibidi Yesu aje afe athibitishe kuwa kwenye Hali ya ubinadamu ukimtegemea Mungu unamshinda Shetani,

Shetani muda wote anatushawishi kutenda mabaya ili kwa Sheria za asili Mungu anatakiwa atuadhibu maana mshahara wa dhambi ni mauti ,na hakuna ondoleo la Dhambi bila Damu kumwagika,but Yesu anatutetea maana alimwaga Damu yake ,ila kwa sharti la kumuamini Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi ,

Shetani anatajwa katika Biblia kama mshataki wa waaminio. Hapa kuna aya zinazothibitisha hilo:


  1. Ufunuo 12:10
    "Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, Sasa kumekuwa wokovu na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana mshitaki wa ndugu zetu, aliyewashtaki mbele za Mungu wetu mchana na usiku, ametupwa chini."
  2. Ayubu 1:6-11
    (Hapa Shetani anamshitaki Ayubu mbele za Mungu, akidai kuwa anamcha Mungu kwa sababu tu ya baraka alizopewa.)
    "Siku moja hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao... BWANA akamwambia Shetani, Je! Umeona mtumishi wangu Ayubu? Kwani hapana aliye kama yeye duniani... Shetani akajibu, Je! Ayubu anamcha Mungu bure?"
  3. Zekaria 3:1-2
    "Kisha akanionyesha Yehoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kumshtaki. BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akuukemee, Ee Shetani!"

Aya hizi zinathibitisha kuwa Shetani anafanya kazi ya kumshtaki mtu mbele za Mungu, akijaribu kuwashushia waaminio hukumu.
 
@iblis bin shetani njoo utoe ufafanuzi Ile tour Yako Kwa ayubu😊
 
Habari hiyo inapatikaba katika kitabu cha Ayubu, je, Ayubu ndiye aliyeiandika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…