Mungu na shetani kushirikiana kumtesa Ayubu ni ushahidi tosha kama Mungu na Shetani ni Marafiki. ndio maana Mungu hamuui shetani mpaka leo

Mungu na shetani kushirikiana kumtesa Ayubu ni ushahidi tosha kama Mungu na Shetani ni Marafiki. ndio maana Mungu hamuui shetani mpaka leo

Wakati Mungu anamwambia yote hayo shetani Nani alimuona?

What am saying is tatizo lipo kwako mtoa mada
Neno la Mungu biblia ndio limeandika hiyo stori.

Mwandishi wa biblia ambalo tunafundishwa kwamba ni neno la Mungu ndio ameweka hayo maneno.

Je unataka kusema kitabu cha Neno la Mungu kimeandika uongo ?
 
Kuna mdau mmoja aliwahi kusema kwamba bibilia ni one side story. Kwamba shetani hakupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kufurushwa huko juu mbinguni kuja hapa duniani.
Akaongeza. Kwamba ugomvi wa Mungu na Shetani sisi unatuhusu nini?

Wangemalizana huko huko. Sio amlete huku duniani.
 

Yesu Amponya Mtu Mwenye Pepo​

5 Wakafika upande wa pili wa ziwa wakaingia katika jimbo la Wagerasi. 2 Yesu alipotoka kwenye mashua, mtu mmoja mwenye pepo mchafu alitoka makaburini akaja kukutana naye. 3 Mtu huyu aliishi makaburini wala hakuna aliyeweza kumfunga hata kwa minyororo , 4 kwa maana mara nyingi alipofungwa kwa minyororo mikononi na vyuma miguuni, aliivunjavunja na hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Usiku na mchana alikaa makaburini na milimani aki piga makelele na kujikatakata kwa mawe.

6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia akapiga magoti mbele yake, 7 akapiga kelele kwa nguvu akasema, “Unataka nini kwangu, Yesu, Mwana wa Mungu Mkuu? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!” 8 Alisema hivi kwa kuwa Yesu alikuwa akimwambia, “Mtoke huyu mtu! Wewe pepo mchafu!”

9 Yesu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jina langu ni jeshi, kwa maana tupo wengi.” 10 Akamwomba sana Yesu asiwapeleke nje ya jimbo lile. 11 Hapo hapo lilikuwapo kundi la nguruwe likilisha kando ya mlima. 12 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Turuhusu tukawaingie wale nguruwe.” 13 Basi akawaruhusu. Wakamtoka yule mtu wakaenda wakawaingia wale nguruwe na kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likatimka kasi kwenye mteremko ule, wakazama ziwani, wakafa.

14 Wale waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotokea. Watu wakatoka kwenda kujionea mambo hayo.

15 Wakaja kwa Yesu, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akiwa ameketi, amevaa nguo na pia akiwa na akili timamu. Wakaogopa. 16 Wale walioyaona mambo haya waliwaeleza wengine yaliyomto kea yule aliyekuwa na pepo na lile kundi la nguruwe. 17 Basi watu wakaanza kumwomba Yesu aondoke katika wilaya yao.
 
Mungu aliruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Ayubu katika Biblia. Hadithi inaanza na Ayubu, mtu mwema na tajiri, ambaye anamcha Mungu kwa uaminifu.

Shetani anapinga uaminifu wa Ayubu, na kumwambia Mungu kwamba Ayubu anamcha Mungu kwa sababy ya mali tu ila sio kutoka moyoni. ( imagine shetani na Mungu wanapiga story kirafiki ila kanisani tunaambiwa ni maadui wakubwa)

Baada ya mabishano hayo kati ya Mungu na shetani kwenye sto
ri

Mungu anamruhusu Shetani kumjaribu Ayubu kwa kumuharibia Ayubu maisha na kupoteza mali, kupoteza afya kwa kupata magonjwa yeye na familia yake


soma Biblia Ayubu 2 kuanzia mstari wa kwanza mpaka wa 13 unaonesha majadiliano ya Mungu na Shetani​

1 Tena kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za Bwana.
2 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
3 Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.
4 Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
5 Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
6 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake.
7 Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.
8 Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni.
9 Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe.
10 Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
11 Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikilia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo.
12 Basi walipovua macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni.
13 Kisha wakaketi nchi pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lo lote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.
Mungu wetu ni mungu wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom