Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
ACHA KUMSINGIZIA MUNGU MAMBO YA KISHETANI.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama wewe unaongozwa na shetani Basi usifikirie kuwa watu wote tunaongozwa na kumtegemea shetani,ACHA KUMSINGIZIA MUNGU MAMBO YA KISHETANI.
Mbona la kuongozwa na shetani lipo wazi kabisa mpaka unaanza msingizia Mungu mambo ya Kishetani. Damu yake mtalipa tu.Kama wewe unaongozwa na shetani Basi usifikirie kuwa watu wote tunaongozwa na kumtegemea shetani,
Nashukuru kwa mchango wako na nimeusoma wote na kila mstari na neno kwa neno. napenda niseme kuwa mh Rais anatambua kuwa yeye Ni mwanadamu, anatambua kuwa yeye siyo Mungu mtu Wala malaika ndio sababu hajawahi kuzuia mtu kumkosoa,ndio sababu unaona namna watu walivyo huru kuzungumza juu yake kulingana na mitizamo yao,Rais wetu siku zote Kama ilivyo kwa yeyote inapaswa akosolewe kwa heshima,adabu na staha, siyo kumtukana Wala kumdhalilisha Wala kumshushia heshima Wala kumshambulia kwa maneno makali na lugha isiyo ya heshima. Hakuna anayeweza kukubali kudhalilishwa . Tunahitaji kuona Rais wetu akikosolewa kwa heshima adabu na staha Kama ambavyo Mimi na wewe tungependa kutendewa hivyo.Labda nikukumbushe mpendwa, kuwekwa na Mungu haimanishi kuwa huwezi kufanya maovu, au huwezi kusemwa vibaya kama unakosea, shida ya watanzania tunamuona Rais kama ni mtu ambaye hawezi kukosea, tunamuona Kama Mungu, hii ndo shida, yule ni mwanadamu Kama wewe, tena hata elimu wapo walio chini yake wanamzidi kwa mbali, ile ni nafasi ya uongozi mpendwa! Wala sio nafasi ya utendaji, hata wewe unaweza kukaa pale nchi ikaenda bila shida yoyote ndo maana huyu kiongozi alipojua kuwa ile ni nafasi ya upendeleo na ni nafasi moja, haya ndio aliyoyafanya mbele za Mungu
1 Wafalme 3:6
Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.
1 Wafalme 3:7
Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
1 Wafalme 3:8
Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.
1 Wafalme 3:9
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?
1 Wafalme 3:10
Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili.
1 Wafalme 3:11
Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;
1 Wafalme 3:12
basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
1 Wafalme 3:13
Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.
Kwa hiyo unaweza ukawa Rais hata kama huo urais umetoka kwa Mungu yawezekana kabisa ukafanya yaliyo mabaya machoni pa Mungu, maanake kukosolewa haimanishi kwamba kuna watu wanataka kumtoa urais hapana, maanake yeye ni mwanadamu hawezi kukamilika kwa kila eneo, na kiongozi mzuri anawasikiliza watu. Lakini ukijihesabia haki , huko ni kutaka kujilinganisha na Mungu maana yeye ndiye hakosei!!!! Hii ni mifano michache ya watu waliowekwa na Mungu lakini mwisho wao haukuwa mzuri
1: suleimani
1 Wafalme 11:6
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
2:NADABU
1 Wafalme 15:26
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya baba yake, na kosa lake alilowakosesha Israeli.
3:BAASHA
1 Wafalme 15:34
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.
4:SAULI
1 Samweli 15:22
Naye Samweli akasema, <br>je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu <br>Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? <br>Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, <br>Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
5: OMRI
1 Wafalme 16:25
Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akatenda maovu kuliko wote waliomtangulia;
6:AHABU
1 Wafalme 16:30
Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kuliko wote waliomtangulia.
7:MANASE
2 Wafalme 21:2
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Ipo mifano mingi mpendwa, kwa hiyo kuwekwa na Mungu, sio kigezo cha uongozi Bora!! Kikubwa anapokosea akubali, wananchi wanapolalamika, awasikilize, na kumuomba Mungu ampe hekima ya kuongoza, na kumpa unyenyekevu, akijua kuwa yeye sio Bora kuliko watu milioni 60+
Na nyie wapambe sio kila kitu kumtukuza mtu, sababu ya fedha au vyeo, msije mkawa mashahidi wa uongo, na kushiriki dhambi za wengine!! Wale mlio karibu na Mh rais mnatakiwa kuwa wa kweli na kumshauri ipasavyo kama alivyo fanya samweli, lakini nyie ndo mnawapoteza hawa viongozi wetu kwa sababu ya njaa zenu!! Ole wenu!
1 Samweli 13:13
Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya BWANA, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana BWANA angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele.
1 Samweli 13:14
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.
Damu ya Nani au umevurugwa na huelewi unachoandika hapaMbona la kuongozwa na shetani lipo wazi kabisa mpaka unaanza msingizia Mungu mambo ya Kishetani. Damu yake mtalipa tu.
Ulikuwepo wakati anampa?0742-676627
Ulisahau kuweka namba ya simu na mtaa unaoishi pale Uporoto.
Akithibitisha ni tag.Thibitisha kwanza uwepo wa Mungu. Cc Kiranga
Asante sana kwa kutamani kuelewa..Nataka uthibitisho mamlaka aliyo nayo Rais yametoka kwa Mungu.
Nataka pia ufafanuzi jinsi gani unafahamu mamlaka ya Rais au kiongozi fulani yanatoka au hayatoki kwa Mungu. Vigezo gani unatumia?
Anampa nini wakati alisahau kumuwekea namba, soma vizuri au nawe ni msafwa kiswahili kimekupiga chenga.Ulikuwepo wakati anampa?
Kwahiyo 2025 sio lazima kumpigia kura kwakuwa aliishachaguliwa na Mungu?Ndugu zangu Uongozi unatoka Kwa Mwenyezi Mungu anayetufahamu sisi Tungali katika Matumbo ya Mama zetu, Yeye Ndiye Anayejuwa hatima yetu, yeye ndiye mtoa Riziki, Neema na Baraka, yeye ndiye kiongozi mkuu wa viongozi wote hapa chini ya jua. Ndiye mtoa Maarifa na Njia kwa wale wamchao na kufuata njia zake.
Rais Samia yupo hapo ,Amefika hapo kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimuandikia kufika hapo. Mama Samia Hajafika hapo kwa uweza wa Mwanadamu, hajafika hapo kwa ujanja wake, kwa Akili zake, kwa Dini yake,kwa kabila lake, kwa jinsia yake, kwa nguvu zake, kwa mipango ya kiuanadamu, kwa Fedha zake, kwa ukarimu wake, upole wake, ucheshi wake, sura yake, Mwendo wake, Sauti yake, Umbo lake, kimo chake, Maono yake, mikakati na mbinu zake, familia yake na Elimu yake.
Mama Samia Amefika Hapo kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa mipango ya Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa kuwa ndivyo ambavyo Mwenyezi Mungu alimwandikia hivyo, Kwa kuwa ndivyo Mwenyezi Mungu alipanga iwe Hivyo, Ndivyo Ambavyo alitaka agano litimie katika ulimwengu wa kiroho wa uumbaji wa Mama Samia Tangia Akiwa Tumboni mwa mama yake
Mbele za Mwenyezi Mungu kila Jambo na wakati wake na majira yake, huu ulikuwa Ni wakati wa Mama Samia, Haya Ni majira ambayo MWENYEZI MUNGU alipanga iwe Hivyo kwa Rais Samia kuinuliwa kiuongozi kuongoza nchi yetu, siyo sisi wanadamu, siyo sisi tuliyo waamuzi. Ni Mungu Ndiye Aliyempaka Rais Samia Mafuta ya Uongozi, Ni Mungu Ndiye aliyempa kibali Cha kufika Hapo. Ni Mungu Ndiye aliyemcholea Ramani yake na njia yake kufika hapo, Ni Mungu Ndiye aliyemshika mkono kumfikisha hapo, Ni Mungu Ndiye Aliyemvusha katika mabonde na milima, katika majaribu na mitihani, ni Mungu Ndiye aliye mpitisha njia ambayo wengine hawakupitishwa, Ni Mungu Ndiye aliyemlinda na kumpigania kufika hapo.
kwote alikopita na kufanya na watu kazi ilikuwa ni mipango ya Mungu katika Kumwandaa na kumfundisha namna ya kuishi na watu wa aina zote, hao watu na hayo maeneo ya kikazi ilikuwa Ni madaraja tu ya kumvusha, lakini Mipango ya Mungu ilikuwa ni kumuinua Hadi hapa Alipo kwa Sasa nafasi ya mwisho kiuongozi na kicheo. Hivyo Hakuna wakumshushaa Mama Huyu Mzalendo wa kweli.
Sasa wewe Mwanadamu Ni Nani mbele za Mwenyezi Mungu? Ni Nani aliyewahi kuongoza kwa akili zake akafanikiwa? Ni Nani awezaye kushindana na Mwenyezi Mungu? Ni Nani kwa Fedha zake Amewahi kununua Urais wa nchi hii? Ni Nani kwa kusuka makundi ya kumshambulia na kumhujumu Rais wake amewahi kufanikiwa kupata Urais wa nchi hii? Ni Nani huyo? Yupo wapi? Wangapi walikuwa na mapesa na marafiki wenye mapesa waliojaribu kununua Urais lakini hawajawahi kufanikiwa? Wangapi wamewahi kuutamani Urais lakini bado wanausikia kwenye Redio? Nani alitegemea Odinga atafika Hadi Leo hii bila kuapishwa kuwa Rais ? Vipi Hillary Clinton? Nani alitegemea mfungwa Nelson Mandela atakuja kupata heshima ya ulimwengu?
Ndugu zangu Amini Amini Nawaambieni kuwa Kama Haikupangwa Na Mwenyezi Mungu Wewe uwe kiongozi Au Rais Basi Tambua kuwa Hata Ufanyeje utaishia kusononeka tu Moyoni Mwako pale utakapoona miaka inayoyoma huku hakuna Dalili za wewe kutimiza Ndoto Zako.
Rais Samia huwezi Ukamchafua na kumpaka matope kwa watanzania na ukafanikiwa,kwa sababu watanzania tunamkubali Sana Rais Samia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kulitumikia Taifa hili, Amekuwa mkweli na muwazi Sana katika kuongoza Taifa letu, kwa kila changamoto tuipitiayo amekuwa mkweli kueleza mikakati ya kukabiliana nayo
Rai Yangu kwa Wana CCM wenzangu na Wazalendo Wa Taifa Hili Tusikubali kuchonganishwa na wenye maslahi Binafsi,Tusikubali watugawe Wala kutupandikiza mbegu za chuki, Marais wote Watano waliopita na kumtangulia Rais wetu mpendwa na kipenzi cha watanzania mama shupavu.
Rais Samia walikuwaa Ni wanaccm na waliotekeleza ilani ya ccm, Hivyo asitokee mtu wakutuletea mbegu za wale na sisi. CCM Ni moja ,Wana CCM Ni wamoja Na Chama Ni kimoja chini ya mama yetu jasiri, Hodari, shupavu, mchapa kazi, mcha Mungu, Mzalendo Na mwenye Dhamira ya Dhati na Taifa hili Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Ni Samia mpaka 2030Kwahiyo 2025 sio lazima kumpigia kura kwakuwa aliishachaguliwa na Mungu?
Kweli wewe unafanana na jina lako maana hata kusoma tu kwako ni shida. Naamini hata kuelewa huwezi kuelewa chochote kileHii itakuwa ndo Id ya Nape.
Kwahiyo hatupigj kura?Ni Samia mpaka 2030
Tutampigia kura za Ndio kwa kuwa huyu ndiye aliyeinuliwa kuja kutuongoza Hadi 2030Kwahiyo hatupigj kura?
Ahahahahah! Kwanini Mungu asimfanye tu kuwa Rais bila ya sisi kupiga kura?Tutampigia kura za Ndio kwa kuwa huyu ndiye aliyeinuliwa kuja kutuongoza Hadi 2030
Kila kitu lazima kitimie nakupigia mchakato wa kidunia na Sheria zake, kwanini hujiulizi ilikuwaje Mungu akaruhusu shetani aje Duniani kututesa wakati alikuwa na uwezo wa kumwangamiza huko huko aliko.Ahahahahah! Kwanini Mungu asimfanye tu kuwa Rais bila ya sisi kupiga kura?