Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Huna adabu na umekosa maadili na kujawa na Roho ya kishetani, Ungekuwa Timamu kichwani ungejuwa maneno unayopaswa kuyatumia katika kuwasilisha hoja yako,Naona wewe Ni mgonjwa unayetakiwa kupatiwa matibabu ya haraka sana
Huyo si mgonjwa wala hana roho ya kishetani, ila anakushangaa namna unavyokuwa limbukeni maana hata wanaomsifia mh. Rais hawawezi kuja na approach za kipumbavu Kama za kwako.
 
Rais Samia Ni kiongozi shupavu na madhubuti Sana, ndio maana unaona nchi ikiwa Tulivu na Amani, Ndio sababu unaona kila kero Inayojitokeza mbele yetu ikikabiliwa kishupavu na serikali yetu, ndio sababu unaona namna tulivyo fanikiwa katika secta nyingi ndani ya muda mfupi wa uongozi wake mama Samia
Sekta zipi zilizofanikiwa, ni dhahiri shahiri mengi unayoandika humu hujayafanyia upembuzi yakinifu acha mihemko, ibua hoja zenye tija kwa masirahi ya taifa ikiwa wewe ni mzalendo kumiliki no ya voda kisiwe kigezo cha wewe kuzidi kuwa mvivu kifikra.
 
Sio kumpigia nani, hata matokeo ya kituo chetu yaliwekwa pembeni, na mawakala wakasainishwa karatasi za matokeo ambayo hayakuwepo. Na ukigowa unakamatwa na polisi na kubambikiwa kesi. Na ushahidi upo lakini hakuna pa kwenda kushitaki.
Sasa ikiwa wewe ni mzalendo wa kweli ulishindwa nini kwenda mahala panapohusika hii inaonesha ni kwa jinsi gani hujui maana ya uzalendo, chukua kamsi ya kiswahili sanifu utafute maana ya neno mzalendo, acha mihemko Lucas
 
CCM ndio chama pekee barani Afrika na Dunia nzima kwa ujumla kilichobaki kinaheshimika miongoni mwa vyama vichache vilivyopo vya umri wake, hii Ni kutokana na namna kinachogusa maisha ya watu na kuwa karibu zaidi na watu kwa kuwasikiliza na kuwatatulia kero wananchi
Try knowledge, Sobber and Great decision, you look like a someone who promised negatively, We created to solve problems not to create problem.
 
Sasa ikiwa wewe ni mzalendo wa kweli ulishindwa nini kwenda mahala panapohusika hii inaonesha ni kwa jinsi gani hujui maana ya uzalendo, chukua kamsi ya kiswahili sanifu utafute maana ya neno mzalendo, acha mihemko Lucas
Sasa hapa ulikuwa unamjibu nani
 
Ndugu zangu Uongozi unatoka Kwa Mwenyezi Mungu anayetufahamu sisi Tungali katika Matumbo ya Mama zetu, Yeye Ndiye Anayejuwa hatima yetu, yeye ndiye mtoa Riziki, Neema na Baraka, yeye ndiye kiongozi mkuu wa viongozi wote hapa chini ya jua. Ndiye mtoa Maarifa na Njia kwa wale wamchao na kufuata njia zake.

Rais Samia yupo hapo ,Amefika hapo kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimuandikia kufika hapo. Mama Samia Hajafika hapo kwa uweza wa Mwanadamu, hajafika hapo kwa ujanja wake, kwa Akili zake, kwa Dini yake,kwa kabila lake, kwa jinsia yake, kwa nguvu zake, kwa mipango ya kiuanadamu, kwa Fedha zake, kwa ukarimu wake, upole wake, ucheshi wake, sura yake, Mwendo wake, Sauti yake, Umbo lake, kimo chake, Maono yake, mikakati na mbinu zake, familia yake na Elimu yake.

Mama Samia Amefika Hapo kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa mipango ya Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa kuwa ndivyo ambavyo Mwenyezi Mungu alimwandikia hivyo, Kwa kuwa ndivyo Mwenyezi Mungu alipanga iwe Hivyo, Ndivyo Ambavyo alitaka agano litimie katika ulimwengu wa kiroho wa uumbaji wa Mama Samia Tangia Akiwa Tumboni mwa mama yake

Mbele za Mwenyezi Mungu kila Jambo na wakati wake na majira yake, huu ulikuwa Ni wakati wa Mama Samia, Haya Ni majira ambayo MWENYEZI MUNGU alipanga iwe Hivyo kwa Rais Samia kuinuliwa kiuongozi kuongoza nchi yetu, siyo sisi wanadamu, siyo sisi tuliyo waamuzi. Ni Mungu Ndiye Aliyempaka Rais Samia Mafuta ya Uongozi, Ni Mungu Ndiye aliyempa kibali Cha kufika Hapo. Ni Mungu Ndiye aliyemcholea Ramani yake na njia yake kufika hapo, Ni Mungu Ndiye aliyemshika mkono kumfikisha hapo, Ni Mungu Ndiye Aliyemvusha katika mabonde na milima, katika majaribu na mitihani, ni Mungu Ndiye aliye mpitisha njia ambayo wengine hawakupitishwa, Ni Mungu Ndiye aliyemlinda na kumpigania kufika hapo.

kwote alikopita na kufanya na watu kazi ilikuwa ni mipango ya Mungu katika Kumwandaa na kumfundisha namna ya kuishi na watu wa aina zote, hao watu na hayo maeneo ya kikazi ilikuwa Ni madaraja tu ya kumvusha, lakini Mipango ya Mungu ilikuwa ni kumuinua Hadi hapa Alipo kwa Sasa nafasi ya mwisho kiuongozi na kicheo. Hivyo Hakuna wakumshushaa Mama Huyu Mzalendo wa kweli.

Sasa wewe Mwanadamu Ni Nani mbele za Mwenyezi Mungu? Ni Nani aliyewahi kuongoza kwa akili zake akafanikiwa? Ni Nani awezaye kushindana na Mwenyezi Mungu? Ni Nani kwa Fedha zake Amewahi kununua Urais wa nchi hii? Ni Nani kwa kusuka makundi ya kumshambulia na kumhujumu Rais wake amewahi kufanikiwa kupata Urais wa nchi hii? Ni Nani huyo? Yupo wapi? Wangapi walikuwa na mapesa na marafiki wenye mapesa waliojaribu kununua Urais lakini hawajawahi kufanikiwa? Wangapi wamewahi kuutamani Urais lakini bado wanausikia kwenye Redio? Nani alitegemea Odinga atafika Hadi Leo hii bila kuapishwa kuwa Rais ? Vipi Hillary Clinton? Nani alitegemea mfungwa Nelson Mandela atakuja kupata heshima ya ulimwengu?

Ndugu zangu Amini Amini Nawaambieni kuwa Kama Haikupangwa Na Mwenyezi Mungu Wewe uwe kiongozi Au Rais Basi Tambua kuwa Hata Ufanyeje utaishia kusononeka tu Moyoni Mwako pale utakapoona miaka inayoyoma huku hakuna Dalili za wewe kutimiza Ndoto Zako.

Rais Samia huwezi Ukamchafua na kumpaka matope kwa watanzania na ukafanikiwa,kwa sababu watanzania tunamkubali Sana Rais Samia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kulitumikia Taifa hili, Amekuwa mkweli na muwazi Sana katika kuongoza Taifa letu, kwa kila changamoto tuipitiayo amekuwa mkweli kueleza mikakati ya kukabiliana nayo

Rai Yangu kwa Wana CCM wenzangu na Wazalendo Wa Taifa Hili Tusikubali kuchonganishwa na wenye maslahi Binafsi,Tusikubali watugawe Wala kutupandikiza mbegu za chuki, Marais wote Watano waliopita na kumtangulia Rais wetu mpendwa na kipenzi cha watanzania mama shupavu.

Rais Samia walikuwaa Ni wanaccm na waliotekeleza ilani ya ccm, Hivyo asitokee mtu wakutuletea mbegu za wale na sisi. CCM Ni moja ,Wana CCM Ni wamoja Na Chama Ni kimoja chini ya mama yetu jasiri, Hodari, shupavu, mchapa kazi, mcha Mungu, Mzalendo Na mwenye Dhamira ya Dhati na Taifa hili Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Hakuna cha Mungu,ni uchawi tu ndio maana uwezi sikia neno Mungu katika utuba zake au salamu yake
 
Hakuna cha Mungu,ni uchawi tu ndio maana uwezi sikia neno Mungu katika utuba zake au salamu yake
Rais Samia Ni Rais mcha Mungu na mwenye Hofu ya Mwenyezi Mungu, Kama wewe hujawahi kumsikia Basi usitufanye sote Ni viziwi Kama wewe, Rais wetu Ni kiongozi Mwenye kumtangulia Mungu kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom