Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Mkuu naona tayari ushavuta afutatu yako ila mwambieni mama yenu yeye na serikali yake ya maccm wafanyekazi aache kumtumiatumia hovyo jina la Mungu kama excuse pia kuwatumia nyinyi waimba mapambio kumpambapamba huku mitandaoni haitamsaidia kitu
 
Mkuu naona tayari ushavuta afutatu yako ila mwambieni mama yenu yeye na serikali yake ya maccm wafanyekazi aache kumtumiatumia hovyo jina la Mungu kama excuse pia kuwatumia nyinyi waimba mapambio kumpambapamba huku mitandaoni haitamsaidia kitu
Nahisi Lucas mwashambwa ni Dkt Mwigulu Nchemba
 
Mwenyezi Mungu Ndiye aliyemuinua Rais Samia kufika hapo Alipo fika na ndio anayeendelea kumpa maarifa ya kiuongozi
Sawa ila

Huyohuyo Mungu atamshusha Siku si nyingi
Maana amekiuka maagizo ya Mungu

Kumbuka Yona alivyoghulikiwa.
So tulia tuu mdaa si mrefu
 
Sawa ila

Huyohuyo Mungu atamshusha Siku si nyingi
Maana amekiuka maagizo ya Mungu

Kumbuka Yona alivyoghulikiwa.
So tulia tuu mdaa si mrefu
Rais Mama Samia kipenzi Cha watanzania anawatumikia watanzania kwa upendo mkubwa Sana pasipo ubaguzi Wala chuki na mtu
 
Wewe una utahira kutwa kucha uko jf kuabudu na kumtukuza binadamu mwenzio hata kama unalipwa
Nina akili Timamu mkuu ndio maana unaona nikitumia busara na hekima kuwajibu watu aina yako wanaotukana badala ya kujenga hoja
 
Mkuu unanikbusha Malaria Sugu alivyokuwa anamtetea Dkt Kikwete hahahahaha pole sana. Nime dislike comments zako kwa sababu wewe ni mtu mbaya sana mnafiki mkubwa ambaye hauitakii CCM mema na Rais Wetu Samia.
Nina mapenzi mema na chama changu,uzalendo na nchi yangu na kumuunga mkono mh Rais wangu kwa kazi kubwa na yakutukuka anayoifanya katika kuijenga nchi hii
 
Rais Mama Samia kipenzi Cha watanzania anawatumikia watanzania kwa upendo mkubwa Sana pasipo ubaguzi Wala chuki na mtu
Huyu Mungu ni mwaminifu

Nakuambia

Mbona zanzibar maji yapo

Mafuta bei chee afu mikopo tugawane

Sio

Mmasubiri tuu
Naomba ya wazalendo yatajibu.
 
Ndugu zangu Uongozi unatoka Kwa Mwenyezi Mungu anayetufahamu sisi Tungali katika Matumbo ya Mama zetu, Yeye Ndiye Anayejuwa hatima yetu, yeye ndiye mtoa Riziki, Neema na Baraka, yeye ndiye kiongozi mkuu wa viongozi wote hapa chini ya jua. Ndiye mtoa Maarifa na Njia kwa wale wamchao na kufuata njia zake.

Rais Samia yupo hapo ,Amefika hapo kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimuandikia kufika hapo. Mama Samia Hajafika hapo kwa uweza wa Mwanadamu, hajafika hapo kwa ujanja wake, kwa Akili zake, kwa Dini yake,kwa kabila lake, kwa jinsia yake, kwa nguvu zake, kwa mipango ya kiuanadamu, kwa Fedha zake, kwa ukarimu wake, upole wake, ucheshi wake, sura yake, Mwendo wake, Sauti yake, Umbo lake, kimo chake, Maono yake, mikakati na mbinu zake, familia yake na Elimu yake.

Mama Samia Amefika Hapo kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa mipango ya Mwenyezi Mungu, Amefika Hapo kwa kuwa ndivyo ambavyo Mwenyezi Mungu alimwandikia hivyo, Kwa kuwa ndivyo Mwenyezi Mungu alipanga iwe Hivyo, Ndivyo Ambavyo alitaka agano litimie katika ulimwengu wa kiroho wa uumbaji wa Mama Samia Tangia Akiwa Tumboni mwa mama yake

Mbele za Mwenyezi Mungu kila Jambo na wakati wake na majira yake, huu ulikuwa Ni wakati wa Mama Samia, Haya Ni majira ambayo MWENYEZI MUNGU alipanga iwe Hivyo kwa Rais Samia kuinuliwa kiuongozi kuongoza nchi yetu, siyo sisi wanadamu, siyo sisi tuliyo waamuzi. Ni Mungu Ndiye Aliyempaka Rais Samia Mafuta ya Uongozi, Ni Mungu Ndiye aliyempa kibali Cha kufika Hapo. Ni Mungu Ndiye aliyemcholea Ramani yake na njia yake kufika hapo, Ni Mungu Ndiye aliyemshika mkono kumfikisha hapo, Ni Mungu Ndiye Aliyemvusha katika mabonde na milima, katika majaribu na mitihani, ni Mungu Ndiye aliye mpitisha njia ambayo wengine hawakupitishwa, Ni Mungu Ndiye aliyemlinda na kumpigania kufika hapo.

kwote alikopita na kufanya na watu kazi ilikuwa ni mipango ya Mungu katika Kumwandaa na kumfundisha namna ya kuishi na watu wa aina zote, hao watu na hayo maeneo ya kikazi ilikuwa Ni madaraja tu ya kumvusha, lakini Mipango ya Mungu ilikuwa ni kumuinua Hadi hapa Alipo kwa Sasa nafasi ya mwisho kiuongozi na kicheo. Hivyo Hakuna wakumshushaa Mama Huyu Mzalendo wa kweli.

Sasa wewe Mwanadamu Ni Nani mbele za Mwenyezi Mungu? Ni Nani aliyewahi kuongoza kwa akili zake akafanikiwa? Ni Nani awezaye kushindana na Mwenyezi Mungu? Ni Nani kwa Fedha zake Amewahi kununua Urais wa nchi hii? Ni Nani kwa kusuka makundi ya kumshambulia na kumhujumu Rais wake amewahi kufanikiwa kupata Urais wa nchi hii? Ni Nani huyo? Yupo wapi? Wangapi walikuwa na mapesa na marafiki wenye mapesa waliojaribu kununua Urais lakini hawajawahi kufanikiwa? Wangapi wamewahi kuutamani Urais lakini bado wanausikia kwenye Redio? Nani alitegemea Odinga atafika Hadi Leo hii bila kuapishwa kuwa Rais ? Vipi Hillary Clinton? Nani alitegemea mfungwa Nelson Mandela atakuja kupata heshima ya ulimwengu?

Ndugu zangu Amini Amini Nawaambieni kuwa Kama Haikupangwa Na Mwenyezi Mungu Wewe uwe kiongozi Au Rais Basi Tambua kuwa Hata Ufanyeje utaishia kusononeka tu Moyoni Mwako pale utakapoona miaka inayoyoma huku hakuna Dalili za wewe kutimiza Ndoto Zako.

Rais Samia huwezi Ukamchafua na kumpaka matope kwa watanzania na ukafanikiwa,kwa sababu watanzania tunamkubali Sana Rais Samia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kulitumikia Taifa hili, Amekuwa mkweli na muwazi Sana katika kuongoza Taifa letu, kwa kila changamoto tuipitiayo amekuwa mkweli kueleza mikakati ya kukabiliana nayo

Rai Yangu kwa Wana CCM wenzangu na Wazalendo Wa Taifa Hili Tusikubali kuchonganishwa na wenye maslahi Binafsi,Tusikubali watugawe Wala kutupandikiza mbegu za chuki, Marais wote Watano waliopita na kumtangulia Rais wetu mpendwa na kipenzi cha watanzania mama shupavu.

Rais Samia walikuwaa Ni wanaccm na waliotekeleza ilani ya ccm, Hivyo asitokee mtu wakutuletea mbegu za wale na sisi. CCM Ni moja ,Wana CCM Ni wamoja Na Chama Ni kimoja chini ya mama yetu jasiri, Hodari, shupavu, mchapa kazi, mcha Mungu, Mzalendo Na mwenye Dhamira ya Dhati na Taifa hili Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Umasikini ni uhaba wa mawazo
 
Acheni kumsingizia Mungu kwenye mambo yenu. Urais ni kazi kama kazi zingine. Hakuna jipya kwenye hicho cheo.

Tunachokitaka kama kapata nafasi aongoze nchi ipate maendeleo kwasababu hatakaa hapo milele. Haya mambo yakumpamba kila saa inaonyesha jinsi asivyotosha kwenye hiyo nafasi.

Uongozi ni kazi sio mapambio kwenye hakuna.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Acheni kumsingizia Mungu kwenye mambo yenu.Urais ni kazi kama kazi zingine.Hakuna jipya kwenye hicho cheo.Tunachokitaka kama kapata nafasi aongoze nchi ipate maendeleo kwasababu hatakaa hapo milele.Haya mambo yakumpamba kila saa inaonyesha jinsi asivyotosha kwenye hiyo nafasi.Uongozi ni kazi sio mapambio kwenye hakuna.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kazi hiyo ndio anayoifanya mh Rais kwa nguvu zake zote katika kuwatumikia watanzania, Anatimiza kusudi la Mwenyezi Mungu aliyemuumba na kumuinua kufika hapo alipofika kiuongozi ili awatumikie na kuwasaidia watu kuinuka kimaisha
 
Watakuja kujipinga wenyewe

Tena wale wale waliowapinga waliomtangulia

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais Samia Suluhu Hasan
Hakika Mwenyezi Mungu ambariki Sana mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
 
Mungu ameukataa huu utawala wa kidhalimu. Amemkataa huyu bibi ambaye ni shetani kwenye umbo la binadamu. Tanzania mpya na salama ni hakika, hakuna atakayezuia.

Hawa mafisadi na walanguzi mnaowaona punde hamtowaona tena, asema Bwana. Mwivi na aibe sana na mzalendo ashikilie hapohapo. Soon kila kisicho mpango wa Allah kitang'olewa.
 
Mungu ameukataa huu utawala wa kidhalimu. Amemkataa huyu bibi ambaye ni shetani kwenye umbo la binadamu. Tanzania mpya na salama ni hakika, hakuna atakayezuia. Hawa mafisadi na walanguzi mnaowaona punde hamtowaona tena, asema Bwana. Mwivi na aibe sana na mzalendo ashikilie hapohapo. Soon kila kisicho mpango wa Allah kitang'olewa.
Huna adabu na umekosa maadili na kujawa na Roho ya kishetani, Ungekuwa Timamu kichwani ungejuwa maneno unayopaswa kuyatumia katika kuwasilisha hoja yako.

Naona wewe Ni mgonjwa unayetakiwa kupatiwa matibabu ya haraka sana
 
Back
Top Bottom