Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Labda nikukumbushe mpendwa, kuwekwa na Mungu haimanishi kuwa huwezi kufanya maovu, au huwezi kusemwa vibaya kama unakosea, shida ya watanzania tunamuona Rais kama ni mtu ambaye hawezi kukosea, tunamuona Kama Mungu, hii ndo shida, yule ni mwanadamu Kama wewe, tena hata elimu wapo walio chini yake wanamzidi kwa mbali, ile ni nafasi ya uongozi mpendwa! Wala sio nafasi ya utendaji, hata wewe unaweza kukaa pale nchi ikaenda bila shida yoyote ndo maana huyu kiongozi alipojua kuwa ile ni nafasi ya upendeleo na ni nafasi moja, haya ndio aliyoyafanya mbele za Mungu
1 Wafalme 3:6
Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.

1 Wafalme 3:7
Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.

1 Wafalme 3:8
Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.

1 Wafalme 3:9
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

1 Wafalme 3:10
Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili.

1 Wafalme 3:11
Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;

1 Wafalme 3:12
basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

1 Wafalme 3:13
Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.
Kwa hiyo unaweza ukawa Rais hata kama huo urais umetoka kwa Mungu yawezekana kabisa ukafanya yaliyo mabaya machoni pa Mungu, maanake kukosolewa haimanishi kwamba kuna watu wanataka kumtoa urais hapana, maanake yeye ni mwanadamu hawezi kukamilika kwa kila eneo, na kiongozi mzuri anawasikiliza watu. Lakini ukijihesabia haki , huko ni kutaka kujilinganisha na Mungu maana yeye ndiye hakosei!!!! Hii ni mifano michache ya watu waliowekwa na Mungu lakini mwisho wao haukuwa mzuri
1: suleimani
1 Wafalme 11:6
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
2:NADABU
1 Wafalme 15:26
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya baba yake, na kosa lake alilowakosesha Israeli.
3:BAASHA
1 Wafalme 15:34
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.
4:SAULI
1 Samweli 15:22
Naye Samweli akasema,
je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
5: OMRI
1 Wafalme 16:25
Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akatenda maovu kuliko wote waliomtangulia;
6:AHABU
1 Wafalme 16:30
Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kuliko wote waliomtangulia.
7:MANASE
2 Wafalme 21:2
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.

Ipo mifano mingi mpendwa, kwa hiyo kuwekwa na Mungu, sio kigezo cha uongozi Bora!! Kikubwa anapokosea akubali, wananchi wanapolalamika, awasikilize, na kumuomba Mungu ampe hekima ya kuongoza, na kumpa unyenyekevu, akijua kuwa yeye sio Bora kuliko watu milioni 60+

Na nyie wapambe sio kila kitu kumtukuza mtu, sababu ya fedha au vyeo, msije mkawa mashahidi wa uongo, na kushiriki dhambi za wengine!! Wale mlio karibu na Mh rais mnatakiwa kuwa wa kweli na kumshauri ipasavyo kama alivyo fanya samweli, lakini nyie ndo mnawapoteza hawa viongozi wetu kwa sababu ya njaa zenu!! Ole wenu!
1 Samweli 13:13
Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya BWANA, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana BWANA angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele.

1 Samweli 13:14
Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.

Labda nikukumbushe mpendwa, kuwekwa na Mungu haimanishi kuwa huwezi kufanya maovu, au huwezi kusemwa vibaya kama unakosea, shida ya watanzania tunamuona Rais kama ni mtu ambaye hawezi kukosea, tunamuona Kama Mungu, hii ndo shida, yule ni mwanadamu Kama wewe, tena hata elimu wapo walio chini yake wanamzidi kwa mbali, ile ni nafasi ya uongozi mpendwa! Wala sio nafasi ya utendaji, hata wewe unaweza kukaa pale nchi ikaenda bila shida yoyote ndo maana huyu kiongozi alipojua kuwa ile ni nafasi ya upendeleo na ni nafasi moja, haya ndio aliyoyafanya mbele za Mungu
1 Wafalme 3:6
Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.

1 Wafalme 3:7
Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.

1 Wafalme 3:8
Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.

1 Wafalme 3:9
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

1 Wafalme 3:10
Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili.

1 Wafalme 3:11
Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;

1 Wafalme 3:12
basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

1 Wafalme 3:13
Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.
Kwa hiyo unaweza ukawa Rais hata kama huo urais umetoka kwa Mungu yawezekana kabisa ukafanya yaliyo mabaya machoni pa Mungu, maanake kukosolewa haimanishi kwamba kuna watu wanataka kumtoa urais hapana, maanake yeye ni mwanadamu hawezi kukamilika kwa kila eneo, na kiongozi mzuri anawasikiliza watu. Lakini ukijihesabia haki , huko ni kutaka kujilinganisha na Mungu maana yeye ndiye hakosei!!!! Hii ni mifano michache ya watu waliowekwa na Mungu lakini mwisho wao haukuwa mzuri
1: suleimani
1 Wafalme 11:6
Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
2:NADABU
1 Wafalme 15:26
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya baba yake, na kosa lake alilowakosesha Israeli.
3:BAASHA
1 Wafalme 15:34
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.
4:SAULI
1 Samweli 15:22
Naye Samweli akasema,
je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
5: OMRI
1 Wafalme 16:25
Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akatenda maovu kuliko wote waliomtangulia;
6:AHABU
1 Wafalme 16:30
Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kuliko wote waliomtangulia.
7:MANASE
2 Wafalme 21:2
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.

Ipo mifano mingi mpendwa, kwa hiyo kuwekwa na Mungu, sio kigezo cha uongozi Bora!! Kikubwa anapokosea akubali, wananchi wanapolalamika, awasikilize, na kumuomba Mungu ampe hekima ya kuongoza, na kumpa unyenyekevu, akijua kuwa yeye sio Bora kuliko watu milioni 60+

Na nyie wapambe sio kila kitu kumtukuza mtu, sababu ya fedha au vyeo, msije mkawa mashahidi wa uongo, na kushiriki dhambi za wengine!! Wale mlio karibu na Mh rais mnatakiwa kuwa wa kweli na kumshauri ipasavyo kama alivyo fanya samweli, lakini nyie ndo mnawapoteza hawa viongozi wetu kwa sababu ya njaa zenu!! Ole wenu!

Nashukuru kwa mchango wako na nimeusoma wote na kila mstari na neno kwa neno. napenda niseme kuwa mh Rais anatambua kuwa yeye Ni mwanadamu, anatambua kuwa yeye siyo Mungu mtu Wala malaika ndio sababu hajawahi kuzuia mtu kumkosoa,ndio sababu unaona namna watu walivyo huru kuzungumza juu yake kulingana na mitizamo yao,Rais wetu siku zote Kama ilivyo kwa yeyote inapaswa akosolewe kwa heshima,adabu na staha, siyo kumtukana Wala kumdhalilisha Wala kumshushia heshima Wala kumshambulia kwa maneno makali na lugha isiyo ya heshima. Hakuna anayeweza kukubali kudhalilishwa . Tunahitaji kuona Rais wetu akikosolewa kwa heshima adabu na staha Kama ambavyo Mimi na wewe tungependa kutendewa hivyo.

Ikumbukwe kuwa unaweza ukamkosoa mtu bila matusi Wala kumdhalilisha na ujumbe wako ukafika bila shida yoyote Ile,hivyo Tujenge na kujijengea utamaduni wa kukosoana kwa heshima na staha, tujifunze kuvumiliana pale tunapotofautiana kimtizamo,hiyo ndio demokrasia yenyewe na ukomavu wenyewe

Thibitisha kwanza uwepo wa Mungu. Cc Kiranga
Akithibitisha ni tag.

Mungu hayupo.

Dhana ya Mungu kuwepo ni chaka la kuficha uzembe wa kufikiri tu.

Yani, sehemu ambayo unatakiwa kufikiri zaidi ili kutoa majibu ya kina na yenye mantiki, ukiwa huwezi au hutaki kufikiri zaidi, na unataka kutoa jibu jepesi, hapo ndipo unachomeka habari ya Mungu.

Ndiyo maana jamii za watu wavivu wa kufikiri na zisizo na elimu zinapenda sana kutumia habari za Mungu, na jamii zilizoendelea kielimu umuhimu wa Mungu unapungua sana.

Nataka uthibitisho mamlaka aliyo nayo Rais yametoka kwa Mungu.

Nataka pia ufafanuzi jinsi gani unafahamu mamlaka ya Rais au kiongozi fulani yanatoka au hayatoki kwa Mungu. Vigezo gani unatumia?
Asante sana kwa kutamani kuelewa..

Nami sasa nimekuelewa..

HAYA NDIYO MAELEZO YANGU

QN. No. 1: Je, mamlaka za wanadamu (kiroho & kimwili) zinatoka kwa Mungu muumba?

JIBU: BIG YES [Warumi 13 yote]

Kwenye maelezo yangu ya awali nilisema "kwa mujibu wa Biblia yaani Neno la Mingu"....

Na kwa hiyo justification itatoka kwenye maandiko matakatifu yaani Biblia ninayoifahamu mimi. Huko kwenye korani ya kiislamu sitaingia kwa sababu sijui lolote unless wajitokeze wanaojua watie neno..

Kwahiyo, it's undisputed truth that;

1. Kila mwenye mamlaka ya kutiisha watu au kutoa haki na hukumu kwa watu; mfano maaskofu na wachungaji makanisani, mashekhe huko misikitini, wazazi (baba na mama kwa watoto wao), hakimu wa mahakama, ma - Rais au wafalme wa nchi/mataifa, mwalimu wa shule nk nk basi hao wote wanafanya kazi hiyo kwa niaba ya Mungu..

SOMA BIBLIA YAKO kitabu cha WARUMI sura ya 13 yote utapata maelezo ya kina juu ya mamlaka za watu in relatioship to God..

Hii ndiyo tafsiri ya mantiki inayosemwa na mtume Paulo kwa Warumi na sisi leo juu ya mamlaka za watu ili kutiisha na kuhukumu watu kwa niaba ya Mungu...

Kumbuka, Mungu NI WA HAKI na anamtaka kila aliyempa (aliyekasimiwa) mamlaka ya Kimungu kusimamia/kuongoza watu wake afanye hivyo kwa haki sawasawa na ambavyo yeye mwenyewe angefanya kama angekuwa na mwili wa ki - binadamu kama sisi jinsi tulivyo..!

QN. No. 2: Je, waliokasimiwa mamlaka ya ki - Mungu kutiisha na kuhukumu watu kwa haki wanaweza kunyang'anywa na Mungu? Na katika mazingira au kwa sababu zipi? Na kwa namna gani..?

JIBU:

A: YES,
Wanaweza kupokonywa mamlaka hayo

B: Katika mazingira ya kukiuka taratibu na kanuni zake: Kutiisha kila mtu, kuhukumu kila mtu kwa haki

C: Kwa namna gani?

Mungu anaweza kumpokonya na kumnyang'anya yeyote mwenye kutenda kwa mamlaka yake kwa namna na njia yoyote anayopenda yeye..

√ Yaweza kuwa kwa njia ya kifo mfano Mfalme Sauli wa Israel kwenye Biblia na wengine wengi waliofuata baada yake...

√ Kwa njia ya adhabu ya kimwili na kutengwa kwa muda hadi ujirekebisha

Mfano; Mfalme Nebudneza alinyang'anywa ufalme wake na kupata adhabu ya kuishi porini kwa miaka 7 na wanyama mpaka alipogundua kosa lake na kutubu. Alirejeshwa madarakani..

Itaendelea......

Kwahiyo 2025 sio lazima kumpigia kura kwakuwa aliishachaguliwa na Mungu?

Ahahahahah! Kwanini Mungu asimfanye tu kuwa Rais bila ya sisi kupiga kura?
Kila kitu lazima kitimie nakupigia mchakato wa kidunia na Sheria zake, kwanini hujiulizi ilikuwaje Mungu akaruhusu shetani aje Duniani kututesa wakati alikuwa na uwezo wa kumwangamiza huko huko aliko.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…