Mungu ni mwema kaniokoa na Kifo japo nipo kitandani hospitalini muda huu

Nakuombea mifupa yako, mishipa yako, misuli yako na maeneo mengine yote uliyoumia au kuvunjika, yapone mara moja katika Jina la Yesu Kristo. Aidha, Mungu akupe amani ipitayo ufahamu wa kibinadamu na ulale usingizi mnono kuanzia sasa.

Mwili wako wote utakapoimarika kumbuka kumpa Mungu utukufu, heshima, sifa na shukrani za pekee!
 
Mkuu cathetar haikuumi sana?, maana kwa wanaume inakuwaga mtihani naona.
 
Polenl sana mkuu utapona tu,nakumbuka mwaka 2019 June maeneo ya Bunju karibu na Petrol Africa nikiwa kwenye bajaj,dereva wa bajaj alimkwepa boda boda aliyeingia Road ghafla,hali ilisababisha bajaj kupinduka na abaria wote kunilalia.Niliumia kifua na kuvunjika mfupa wa bega, pia dereva alivunjika mguu.

Tulikimbizwa hospital kwa huduma ya kwanza nikachomwa sindano ya maumivu ya diclopa...aisee nilivimba macho baada ya sindano nikawa sioni huku maumivu ya mfupa wa bega nguo zimechanika...dah Mungu ni mwema

Baadaye nilienda Rabininsia baada ya x-ray ikabainika nimevunjika mfupa wa bega huku goti ilmechubuka.Hadi muda huu ni usiku sijatoa taarifa kwa ndugu wala mke kwasababu wife alikuwa ana mimba ya miezi 8.

Baada ya matibabu,nikanunua t shirt nikavalishwa kwasababu shati lilichanika nikanunua na miwani kwasababu macho yalikuwa yamevimba nikaelekea nyumbani ....aisee wife na watoto walishtuka sana kuniona na lile dude la kussapoti mkono,suruali imechanika na macho yamevimba. Nashkuru Mungu nilipona baada ya miezi 2...Mungu ni mwema.

Ajali isikie tu,ni sekunde chache tu zinabadili maisha ya mtu.Tuongeze umakini

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Pole sana kiongozi

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
pole sana bro, Mungu atakujaalia utapona [emoji120][emoji2536]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…