Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Unathibitisha vipi mungu wako Ndo kakuumba na siyo mungu odin, au brahma the creator, au zeus, au orisha au loa au vodun au sango au nkisi au alusi.

Ni nani aliyesema kajiumba halafu ajiwekee ukomo? Hayo ni maneno yako na si yangu

Thibitisha mungu yupo?
Maswala Ya Rohoni Unataka Nikuthibitishie Kwa Mwili!? (WEWE NAJUA UNATAKA ISHARA NA HAUTA ONA ISHARA ISIPOKUWA ISHARA YA YONA)

NA KAMA HUAMINI MUNGU MKUU YAHWEH NDIE ALIE UMBA VYOTE umewajuaje hao miungu ulio wataja odin, brahma, zeus NIJIBU HILI maana Wewe huamini maswala ya MUNGU UWEPO WAKE ?



Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
YANI MAISHA YAKO TU UKO CHINI YA SERIKALI INAKUTAWALA AFU USEME MUNGU HAYUPO MTAWALA WA VYOTE UNAAKILI KWELI

NYUMBANI KWAKO TU WEWE BABA NDIO MKUU KWA WATOTO WAKO NA MKEO UKISEMA NENO WANALITII AFU USEME MUNGU HAYUPO SASA HUJIULIZI WEWE HUO UONGOZI UMEUPATA WAPI!?.

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Maswala Ya Rohoni Unataka Nikuthibitishie Kwa Mwili!? (WEWE NAJUA UNATAKA ISHARA NA HAUTA ONA ISHARA ISIPOKUWA ISHARA YA YONA)

NA KAMA HUAMINI MUNGU MKUU YAHWEH NDIE ALIE UMBA VYOTE umewajuaje hao miungu ulio wataja odin, brahma, zeus NIJIBU HILI maana Wewe huamini maswala ya MUNGU UWEPO WAKE ?



Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app


Halafu jaribu kujibu jinsi ya mtu anavyouliza hakuna sehemu nimesema nahitaji ishara na unahakikisha kabisa eti unajua nataka ishara. Unaweza nionyesha sehemu niliyosema nataka ishara?
Nimesema thibitisha mungu yupo na si ishara?
 
Kuna vitu vingine inabidi ufikilie kwa akili ya ubinaadamu siyo lazima uende shule ukasoma, nafasi ya Mungu kwa binadamu ni kila kitu, yeye alikuwepo, yupo, atakuwepo daima.


Pole sana ndugu yangu, lakini ujuaji wetu huu wote mwisho wake ni kaburini, halafu Mungu mwenyewe kaweka pazia, kiasi kwamba hatuna nafasi ya kuludi tena kuja kusahihisha makosa yetu
Mungu yupi?
 
Halafu jaribu kujibu jinsi ya mtu anavyouliza hakuna sehemu nimesema nahitaji ishara na unahakikisha kabisa eti unajua nataka ishara. Unaweza nionyesha sehemu niliyosema nataka ishara?
Nimesema thibitisha mungu yupo na si ishara?
KWANI HUYU ZEUS ULIE MTAJA NI NANI TUANZIE HAPO KWANZA!?

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Kuna vitu vingine inabidi ufikilie kwa akili ya ubinaadamu siyo lazima uende shule ukasoma, nafasi ya Mungu kwa binadamu ni kila kitu, yeye alikuwepo, yupo, atakuwepo daima.


Pole sana ndugu yangu, lakini ujuaji wetu huu wote mwisho wake ni kaburini, halafu Mungu mwenyewe kaweka pazia, kiasi kwamba hatuna nafasi ya kuludi tena kuja kusahihisha makosa yetu
Wewe unamjua Mungu kwa upande upi na yeye ni nani na ana umbo gani kimuonekano?????Ushawahi kutoka nje ya mwili wako?????? Ushawahi kuutazama ulimwengu either kichawi au kinajimu?????? Au unamjua mungu kupitia vitabu vya simulizi za kiyahudi na kiarabu?????? Angalia maswali yangu vizuri afu nijibu ndugu yangu
 
Kwanini unasema walokole duniani hawazidi milioni kumi ikiwa kila mahali duniani kuna makanisa mengi ya kilokole.
Walokole ni usharika wa kiroho,sio makanisa...Mm mwenyewe napambana niwe mlokole na ninajua thawabu za walokole kwenye ulimwengu wa nje ya mwili.Wapo wachache duniani sababu huo ulokole ni imani zaidi,hivyo ni vigumu kusadikika kwa watu walio wengi.Makanisa na dini ni vitu vya matendo vinavyoonekana bali imani haionekani bali inasadikika tu moyoni.
 
kumbuka kisa cha mnajimu na sauli,sauli alitaka kumpandisha samweli na kweli samweli alikuja ijapokuwa alishakufa na akamkemea na kumtabiria kifo chake so wanajimu wanauwezo wa kutambua yaliyo ya Mungu.
Lakini pia mamajusi(wanajimu)wa mashariki walitambua kuzaliwa kwa Yesu kupitia nyota.
13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13

14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14

15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
1 Samweli 28:15

16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?
1 Samweli 28:16

17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.
1 Samweli 28:17

18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.
1 Samweli 28:18

19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.
1 Samweli 28:19
Kweli mkuu
 
Unathibitisha vipi mungu wako Ndo kakuumba na siyo mungu odin, au brahma the creator, au zeus, au orisha au loa au vodun au sango au nkisi au alusi.

Ni nani aliyesema kajiumba halafu ajiwekee ukomo? Hayo ni maneno yako na si yangu

Thibitisha mungu yupo?
HUNA HOJA SI HAPA Wewe Umetaja hiyo miungu sasa Uongo Upi Tena [emoji23] MKUU HAUPO SAWA MPOKEE YESU

MAANA MASUALA YA ROHONI WEWE NI MTUPU unamjua huyo zyeusi wako [emoji23][emoji28]

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
NAENDELEA....!!!
Duniani ukipatizama kwa ulimwengu wa kinajimu unaona dunia mbili.Kuna dunia inayoonekana na dunia isiyoonekana.Kwenye dunia inayoonekana kila Mtu anaijua ila kwenye dunia isiyoonekana ni wachache wanaijua.
Mzee matata aliponiambia nichague himaya,basi nikaanza kumdadisi yeye yupo himaya ipi na akaniambia yafuatayo
MAMBO MATATU MAKUU
MOJA: Kuna mkuu wa ulimwengu akimaanisha mfumo wote wa sayari zinazojulikana na zisizojulikana.Na kuna mkuu wa wakuu nje ya mfumo wa ulimwengu.Mpaka sasa wanajimu wameshindwa kumchambua mkuu wa wakuu sababu yupo mbali ya mfumo huu wa nyota.Na himaya zipo mbili za mkuu wa mfumo wa ulimwengu na mkuu wa wakuu.Akasema wale watu warefu wanapoenda nje ya mfumo wa sayari za ulimwengu waga wanaenda kuripoti kwa huyo mkuu wa wakuu.
MBILI:Binadamu kiasili wamefanana kiumbo na aliyewatengeneza kuanzia sura na mpangilio wa mwili kasoro tu vimo na akili.Lakini binadamu ni zao la mawazo ya kiumbe mwenye nguvu na akili kuliko binadamu,hivyo basi binadamu hawakutokea kwa bahati mbaya.Ndio maana wale watu warefu wana muonekano kama binadamu kwa asilimia 90%.Sasa aliyewatengeneza either ni mkuu wa ulimwengu au mkuu wa wakuu nje ya mfumo wa ulimwengu.
TATU:Kuna ukweli na uongo na kuna uzuri na ubaya na kuna kujua na kutokujua na kuna kupatia na kukosea.Yote haya yanaheshimika sana katika unajimu.
Mzee matata akaniambia kama wewe shida yako ni kuwajua wale watu warefu basi nakushauri ujiunge na himaya yao.Unadhani kwanini mimi nawakimbia??? Jibu ni jepesi sipo katika himaya yao na hawanitambui ndio maana hawaji kwangu.Wewe unataka kuwajua ila ili uwajue zaidi lazima ujiunge katika himaya yao.Na ukijiunga katika himaya yao basi ujue watakua hawaonekani bali utaishi kwa imani""Wale walokole wanaishi kwa imani"""na sisi wanajimu tunaishi kwa kuona.Hiyo ndiyo tofauti yetu kwenye ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida.
Akaendelea kusema himaya ya wale watu warefu wa anga za mbali ina nguvu sana kuliko himaya za watu warefu wa baharini au kwenye sayari ya Pluto,Jupter na Uranus.Hata vitabu nilivyokupa uvisome kuhusu wale watu warefu kila kitabu kina nguvu yake.Kitabu cha walokole kina nguvu na kitabu cha wanajimu kina nguvu.Lakini usiniulize swali lolote kwa sasa wewe endelea na utafiti wako na mimi nitakua nakusaidia pale unapokwama kimawazo na kielimu,na suala la kukufundisha kupaa lifute maana wazee wamenikatalia hivyo hakuna tena hicho kipengele tujifunze mengine.Akaniambia tujifunze mambi yafuatayo hapa chini
MOSI:Walokole ni akina nani kiroho
PILI:Wachawi ni akina nani kiroho
TATU:Wanajimu na waganga ni watu gani kiroho
NNE:Wale watu warefu na jamii zote mbili ni viumbe gani kiroho
TANO:Hii tunaita dini ni nini kiroho
SITA:Mungu ni nini kiroho na nguvu ya imani ni nini kiroho
SABA:Kifo ni nini kiroho
NANE:Siasa na utawala wa binadamu ni nini kiroho
TISA:Elimu ni nini kiroho
KUMI:Nini hitimisho la haya yoote.
Basi mzee wangu Matata akasema tutajifunza moja baada ya lingine
NB :Nilijua dunia hii ipo tofauti na wengi mnavyoiona kwa nje.Asilimia tisini ya vitu vinavyoonekana havipo kama vinavyoonekana kwa nje.Na katika ulimwengu wa roho binadamu wote ni sawa hakuna mbantu au mchina au mhindi au mzungu au mwarabu na nk.....!!!Wote ni sawa
NITAENDELEA...........!!!!!
 
Napata shaka kama ulimuona huyo MUNGU wa walokole...

Mbona umetumia Mnajimu? Maana Mnajimu huyo ni Mkuu wa giza...

Kumuona Mungu sio kwa kutumia mtu na nguvu za kibinadamu.

Bali ni kwa kumpokea Bwana kuwa mwokozi wa maisha yako, kuomba, kufunga, kusali...

Na hii ndio maana wapo ambao wanaenda kanisani kila siku ila hawaoni mambo ya Rohoni...

Wanajiita wakristo lakini YESU hawajui...
1 Samweli 28:8-17 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.
Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?
Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili.
Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.

Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli.

Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.

Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.

Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.

Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?
Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.
 
Na huyu mkuu wa jamii za baharini kwanini anakiburi mpaka sasa,wakati Jehova na mwanaye Yesu kristo wameshamuandikia adhabu na hukumu kali na angalia anajua na kutambua pia yakwamba Jehova ambaye ni mkuu wa anga za juu sana ananguvu na anatisha sana kuliko yeye? Au ana kiburi cha ujinga, na upumbavu au ameamua kujitoa muhanga huyu mkuu wa jamii za baharini?
 
INAENDELEA...........!!!!!
WALOKOLE : Watu wanawaita binadamu wenzao wa madhehebu ya kipentekoste kua walokole sababu wanasali kwa kukulia.Lakini katika ulimwengu wa kiroho walokole ni watu wa viduara vya miale ya moto vichwani mwao.Ni watu wabaya na waharibu mipango ya wanajimu,watu wa ngome za vimbunga vya moto na washirika wao ni watu warefu wa moto na kelele zao(Maombi) ni moto.Kuimba kwao ni moto na wanaripoti moja kwa moja kwa mkuu wao ambae ni moto mkuu nje ya mfumo wa sayari ya dunia.Lakini kwa muonekano wa kibinadamu ni wanyonge na kipato cha wastani au kusema ni watu wa maisha ya kawaida kwa asilimia kubwa sababu hawajishughulishi 100%na ubinadamu ,wapo kiroho zaidi.Wakiamka wanasali,wakitembea wanasali,wakilala wanasali,wakifanya kazi zao wanasali na ni watu wa ajabu sana kwenye ulimwengu wa kiroho.Kinachowatofautisha na binadamu wengine ni kwamba wao kimoyomoyo wanamshukuru Mungu wao hata kwenye shida.Basi wanapomshukuru Mungu wao hasa nyakati za shida bila kunungunika katika ulimwengu wa roho wanakua kama binadamu wenye ngozi za moto, wanazungukwa na wale watu warefu wenye panga za moto.
Lakini hatari zaidi ni pale wanapomlilia mungu wao aliye kule nje ya mfumo wa ulimwengu na sayarï (Vilio vyao ni kama radu za umeme zinapaa kumwendea mungu wao) .Wale watu warefu wanashuka kwa wingi na kuwazunguka na kuwalinda dhidi ya wabaya wao na wale watu warefu wa jamii ya baharinii.Kiroho walokole wanaitwa ""Wana wa mwangaza""sababu ya vile viduara vya moto vichwani mwao.
Mzee Matata akaniambia katika ulimwengu wa roho basi hao walokole hawashikiki.
WACHAWI :Binadamu hawa wanaoitwa wachawi kiroho wanaitwa""Wasumbufu""ni watu wanaopenda kusumbua wenzao kwa kila hali.Wanaroga na kuharibu nyota za watu,wanajihusisha na elimu ya giza na hawamtambui mkuu wa walokole sababu ameulaani uchawi.Kwa muonekano wa nje wachawi ni binadamu kama binadamu wengine na wana vipato vya ngazi zote,kuanzia umasikini mpaka utajiri.Kwenye ulimwengu wa kiroho ni washirika wa ile jamii ya watu warefu wanaotoka baharini.Na wakitembea basi wanatembea na wale watu warefu wa kutoka baharini.Kwenye ulimwengu wa kiroho hawana mwanga wa kuakisi jua,na hawana nguvu kama walokole sababu wamejaa damu za watu.Wao huua ili wapate nguvu na wana mengi mabaya kwa muonekano wa kibinadamu.Pia waoga sana wanapowaona walokole au wale watu warefu wa kuakisi mwanga wa jua.Wana mkuu wao na mungu wao tofauti kabisa na mungu wa walokole.Wao wana moto ila sio mkali kama moto wa walokole maana walokole wakianza kusali tu basi ule moto wao unazima.Na ndio maana hwapatani kabisa na walokole katika ulimwengu wa kiroho.Wana nguvu ila sio kama za walokole,sababu nguvu za wachawi sio za asili bali makafara lakini walokole nguvu zao ni za asili tena ya moto.Hapo kwa kidogo tu nimechambua jamii hizi mbili katika ulimwengu wa kiroho
NITAENDELEA........!!!!
 
Back
Top Bottom