Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,921
- 4,683
Wanajimu na wachawi ni fani mbili tofauti.kumbuka kisa cha mnajimu na sauli,sauli alitaka kumpandisha samweli na kweli samweli alikuja ijapokuwa alishakufa na akamkemea na kumtabiria kifo chake so wanajimu wanauwezo wa kutambua yaliyo ya Mungu.
Lakini pia mamajusi(wanajimu)wa mashariki walitambua kuzaliwa kwa Yesu kupitia nyota.
13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13
14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14
15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
1 Samweli 28:15
16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?
1 Samweli 28:16
17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.
1 Samweli 28:17
18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.
1 Samweli 28:18
19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.
1 Samweli 28:19
Wanajimu ni wasoma nyota na matukio ya hizo nyota katika ulimwengu wa kiroho bila nia ya kudhuru.
Ambapo wachawi ni walozi(fitini) kwa kujigeuza pepo na kuunganishwa katika ulimwengu wa roho nia yao ikiwa ni kudhuru.
Zamani wakati wa agano la damu za ndama na mbuzi, nafsi zilizofunikwa maovu kwa dhabihu hizi zilipokufa zilienda mahali pa daraja la juu kule kuzimu palipoitwa paradiso.
Shetani kwa huo wakati alikuwa na access ya kuzifikia hizi nafsi na uwezo wa kuzileta huku duniani kutumia wachawi kwa kazi mahsusi. Ndicho kitu mwanamke huyu mchawi wa Endori alichofanya kwa Samweli.
Lakini baada ya dhabihu ya damu ya Yesu kutolewa watakatifu waliokufa chini ya hii kafara walihamishwa kutoka pale mahali pa juu pa kuzimu na kupelekwa uweponi mwa Mungu(mbinguni?).
Hapo walipo kwa sasa shetani hana access napo hivyo mchawi hawezi tena kuiita nafsi ya mtakatifu duniani.
Ukiona mzimu wa aliyekufa katika kipindi cha agano jipya uliletwa duniani na kuwa na ijara kwa walio hai ni kudhihirisha nafsi ya huyo mtu ilipotea na yupo kuzimu ambako wachawi na waabudu mizimu wana access.
Hii ndiyo maana ya shetani kunyang'anywa funguo na Yesu aliposhuka kuzimu na kuzihubiria zile nafsi zilizopotea wakati wa kungoja.
Mathayo 27:50-53
[50]Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
Jesus, when he had cried again with a loud voice, yielded up the ghost.
[51]Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
And, behold, the veil of the temple was rent in twain from the top to the bottom; and the earth did quake, and the rocks rent;
[52]makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
And the graves were opened; and many bodies of the saints which slept arose,
[53]nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
And came out of the graves after his resurrection, and went into the holy city, and appeared unto many.