Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Sasa kwa nini Haruni kuhani wa Mungu atume mbuzi huko jangwani kwa ajili ya azazel?
Ile ilikuwa ni sehemu ya ibada ya toba ya kitaifa iliyokuwa inafanyika mara moja kwa mwaka.

Mbuzi yule aliwakilisha deposit ya uovu wa wana wa Israel ambao ulikuwa unawekwa juu ya mbuzi na mbuzi kupelekwa jangwani na mtu mmoja atakaye kuwa appointed

Baada ya mbuzi kufikishwa jangwani alikuwa anaachwa atange tange majangwani huko, na alikuwa hachinjwi.

Zoezi hilo pia liliambatana na kumtoa kondoo mmoja, ambaye yeye alichinjwa kwa ajili ya kufanya upatanisho wa nafsi na damu ilimwagwa madhabahuni.

Sasa kuelewa hili inabidi fahamu mambo ya msingi manne

1.Nini tofauti ya uovu na dhambi, pia tofauti ya uovu na makosa, pia tofauti ya uovu(iniquities) na maovu(evils), na uhusiano wake na huyu mbuzi wa Azazel

2. Adhabu iliyokuwa na toba ndani yake ambayo Israel aliipitia jangwani kwa miaka 40 kwa kutanga tanga majangwani, na uhusiano wake na huyu mbuzi wa Azazel

3.Kanuni ya kiroho ya nafsi moja kuhamisha uovu wake kwenda nafsi nyingine, kwa nafsi moja kulipia(kudhamini), jambo ambalo mbuzi huyu alifanya na pia Yesu alifanya

4.Madai ya wafalme wa kuzimu na haki walizo nazo juu ya mwanadamu atendaye dhambi, na uhusiano wake na huyu mbuzi wa Azazel

Ningefafanua kwa mapana na ningejibu swali lako la msingi, ila tusivuruge uzi wa ndugu yetu, una mambo mengi ya kujifunza

Pia ni vyema ukajifunza misimu ya toba za kiroho zilozowekwa kwa wana wa Israel na mahusiano yake na Mahakama za Kiroho.
 
Nataka kufanya uchunguzi na mimi niwaone tu inatoshaaa hebu niambie njia za kufanya hivyo
Pia nasubiri muendelezo
Zipo njia nyingi

Ila kama huna nguvu za huyu Mungu wa walokole, utaishia kufungua portals ambazo zitawapa access hao wanao kaa baharini kuingia moja kwa moja kwenye maisha yako

Madhara utakayoyapata ni aidha uwe mchawi aliyeshindikana

Au uanzishe dini mpya

Wote walioanzisha dini hizi ambazo ni nje ya Ukristo, walikuwa na ambitions za kuufahamu ulimwengu wa roho

Wakafungua portals(malango) ambayo Mungu kwa hekima yake aliamua kuyafunga

Matokeo yake maroho yakawavamia, yakawapa mafundisho ya mashetani yaliyochanganywa na ya Kimungu ndani yake, wakaishia kuunda dini tunazozijua leo.

So si vyema sana kutafuta kuona for the sake of kuona tu, ni heri uenende kwa imani bila kuona otherwise utawasha moto usioweza kuuzima
 
Nataka niuwashe huo moto
 
Ulichosema ni sahii kabisa
 
Upo sahii ndugu,,,unapoanza kufanya utafiti wa mambo ya kiroho basi unaishia kua either mchawi au kujiunga na imani tata
 
Umefafanua vyema mambo ya kiroho
 
NINGEKUA NA UWEZO WA KUWAKUSANYA WALOKOLE WOTE NA KUWAWEKA SEHEMU MOJA NA NIWAAMBIE KAULI MOJA.BASI NINGEWAAMBIA HIVI""""""Haijalishi mnapitia hali gani kimwili ila kiroho nyinyi ni watawala na wamliki......kinachotakiwa kwenu ni imani tu
 
Utafiti mzuri sana ila Kuna maeno unayachangany na yapo tofauti sana 1 Mungu au MUNGU ( bible inasema jina lake linatakiwa liamze na elufi KUBWA ayo zote ziwe kubwa)-na mungu au miungu mingine
Ni makosa ya kiuandishi tu,katika kuandika na kuelezea na sio jambo dogo kuelezea vitu vya kiroho kuna vikwazo kiroho na kimwili.I hope you understand spiritually
 
Sasa kwa nini Haruni kuhani wa Mungu atume mbuzi huko jangwani kwa ajili ya azazel?
Hilo kwa kweli sijui mkuu na sipendi nidanganye ila nachojua ni kua huyo Azazel amefungwa kwenye shimo jangwani toka enzi za mtu aitwaye Enoko muajemi wa mespotamia ambaye wanajimu wanajiuliza alikua binadamu au mwana wa kiungu.Na sababu ya Azazel kufungwa ni kwamba aliwashawishi wana wa kiungu wazae na wanadamu kwa kutumia uchawi na unajimu wa elimu ya anga.Na wakawafundisha binadamu elimu ya kiungu ambayo ni unajimu na uganga hasi.Hivyo mmliki wa wamiliki namaanisha Mkuu wa wakuu akamfunga yeye pamoja na wenzie na akavipoteza taratibu kizazi baada ya kizazi,vizazi vyao wote (AZAZEL NA WENZIE) walivyozaa na wanadamu
 
Huyo Azazel ni nani?
 
Shukrani[emoji1374]
 
Hapa kutakuwa na jambo moja la msingi sana kuthibitisha zao mbili tofauti katika wanadamu. Yaani uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka ambalo naamini halina ubishi.
Linalobishaniwa kwa hizi zao mbili ni wapi ulipoingilia.
Je uliingilia kwa Eva(Hawa) au wana wao baada ya kuongezeka?
Na je kuna tofauti gani kati na Nefili na mijitu?
Au Nefili ndio hao hao majitu.

Mwanzo 6:4
[4]Nao Wanefili
walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, and they bare children to them, the same became mighty men which were of old, men of renown.
 
Hamna mtu yamewahi kumkuta zaidi ya kulishana matango pori tu na kuamini without questioning. Story zote ushirikina ni hearsay na unapaswa kuamini tu kama nyumbu bila kutumia akili.
hatuwezi shindana ni mpaka ukutane na hio kadhia ndio utatia akili umezaliwa maisha bora sio kila shida utaifahamu kaa kwa kutulia kwa kua hujalazimishwa kuamini.
 
Siwezi kuunganisha link mkuu ila uzi wa ushuhuda wangu upo humu. Naomba uangalie profile yangu kuna sehemu ya kuona nyuzi na activities zangu huku JF utauona.
uzi wako unaitwaje mkuu niusearch heading tuu nitajie ntashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…