Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Ile ilikuwa ni sehemu ya ibada ya toba ya kitaifa iliyokuwa inafanyika mara moja kwa mwaka.Sasa kwa nini Haruni kuhani wa Mungu atume mbuzi huko jangwani kwa ajili ya azazel?
Mbuzi yule aliwakilisha deposit ya uovu wa wana wa Israel ambao ulikuwa unawekwa juu ya mbuzi na mbuzi kupelekwa jangwani na mtu mmoja atakaye kuwa appointed
Baada ya mbuzi kufikishwa jangwani alikuwa anaachwa atange tange majangwani huko, na alikuwa hachinjwi.
Zoezi hilo pia liliambatana na kumtoa kondoo mmoja, ambaye yeye alichinjwa kwa ajili ya kufanya upatanisho wa nafsi na damu ilimwagwa madhabahuni.
Sasa kuelewa hili inabidi fahamu mambo ya msingi manne
1.Nini tofauti ya uovu na dhambi, pia tofauti ya uovu na makosa, pia tofauti ya uovu(iniquities) na maovu(evils), na uhusiano wake na huyu mbuzi wa Azazel
2. Adhabu iliyokuwa na toba ndani yake ambayo Israel aliipitia jangwani kwa miaka 40 kwa kutanga tanga majangwani, na uhusiano wake na huyu mbuzi wa Azazel
3.Kanuni ya kiroho ya nafsi moja kuhamisha uovu wake kwenda nafsi nyingine, kwa nafsi moja kulipia(kudhamini), jambo ambalo mbuzi huyu alifanya na pia Yesu alifanya
4.Madai ya wafalme wa kuzimu na haki walizo nazo juu ya mwanadamu atendaye dhambi, na uhusiano wake na huyu mbuzi wa Azazel
Ningefafanua kwa mapana na ningejibu swali lako la msingi, ila tusivuruge uzi wa ndugu yetu, una mambo mengi ya kujifunza
Pia ni vyema ukajifunza misimu ya toba za kiroho zilozowekwa kwa wana wa Israel na mahusiano yake na Mahakama za Kiroho.