Mti ndio uzaao matunda na hivyo kila mti huzaa kwa jinsi yake.
Ukikata matawi ya mti na kuacha shina lake basi mti huo utamea tena matawi yatakayozaa matunda ya asili ya mti wenyewe.
Kuzaliwa upya katika kiroho ni kungolewa shida katika asili yake na kupandikizwa katika asili ya shina jingine ambalo ni roho wa Kristo.
Matunda yatakuwa yapatanayo na toba kwa mhusika.
Ukiona matunda bado ni ya asili katika mwili basi hilo ni jawabu tosha kuwa nafsi hiyo haijawahi kumbolewa kutoka katika utumwa wa dhambi japo inaweza kujinenea yenyewe vinginevyo.
Aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi.
Hatendi dhambi kwa sababu sii asili yake kufanya hayo. Na kama kutakuwepo na makosa maana yapo jua halita kuchwa bila kutengeneza.
Dini ina kawaida ya mazoea ya maungamo yasiyomaanisha maana anaeungama hajawahi kuzaliwa upya kwa roho wa Mungu bali ana yale maarifa(ujuzi) na hata nafunuo makuu kumhusu Mungu kiakili.
Maandiko yanakiri kuwa wana ujuzi tu na sii roho wa kristo
Waebrania 10:26
[26]Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
For if we sin wilfully after that we have received the knowledge of the truth, there remaineth no more sacrifice for sins,
Hata hivyo wanauzungumziwa katika waebrania sita ni watheologia(dini) na sii mtu aliyezaliwa upya katika ufalme wa Mungu.
Waebrania 6:4-6
[4]Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
For it is impossible for those who were once enlightened, and have tasted of the heavenly gift, and were made partakers of the Holy Ghost,
[5]na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
And have tasted the good word of God, and the powers of the world to come,
[6]wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
If they shall fall away, to renew them again unto repentance; seeing they crucify to themselves the Son of God afresh, and put him to an open shame.
Aliyezaliwa upya katika ufalme maandiko yanakiri kwake kutowezekana kwa nguvu ya aina yeyote kumpokonya mikononi mwa Yesu ila mmoja tu yaani Yuda ili andiko litimie.
Yohana 17:12
[12]Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
While I was with them in the world, I kept them in thy name: those that thou gavest me I have kept, and none of them is lost, but the son of perdition; that the scripture might be fulfilled.
Hivyo kusoma misa(sala) bila kumaanisha toba kibinafsi kwa kughairi mabaya na keuzo la dhati ni sawa na kupayuka kufanywako na mshika dini yeyote.
Sent using
Jamii Forums mobile app