Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Imani, Imani, Imani.

Naona imetajwa Sana ,kwenye mada,

Mimi nimepokea ,ujumbe wa kivuvio wa ki Mungu ,

Ninaita uvuvio ,sababu haya nayo yahandika ,sikupanga na hata Mimi sikuyajua ,

Nimeshangaa ,maana hata Mimi najifunza pia Kwa nilichokiandika hapa mwenyewe, nimeandika kitu ambacho hata Mimi nilikuwa najiuliza,

Kuwa baraka zinatokaje rohoni kuja mwilini

Kiufupi ,
Rohoni ni Imani
Mwilini ni matendo

Rohoni ni Ulimwengu wa Imani
Mwilini ni ulimwengu wa matendo,
,
Ni kama Duniani yaani mwilini tumekuja kutenda Mapenzi ya Mungu ,matakwa yake sio yetu ,

Details;-

Unapozungumzia Imani ,unazungumzia matendo,

Maana ni pacha,Imani na matendo vinamuungano,

Hivyo,

Unaposema walokole wanalindwa Kwa Imani, hio kiroho maana Imani HAIONEKANIKI ni ya kirohoni, Sasa Kwa lugha nyingine tunasema ,Katika mwili wanalindwa Kwa matendo,



Kiroho= Ili ulindwe kiroho inategemea Imani ,maana Imani ni ya Rohoni na ndio Nguvu ya Ulinzi rohoni ni Imani,

Kimwili=Ili ulindwe mwilini Ulimwengu wa nyama unaoonekana ,maana na huku mwilini tuna mahadui ,wakimwili ,Tena Kuna wengine wametika rohoni na kutufuata hata mwilini yaani Ulimwengu wetu wa Mwili ndio hao majini ,Sasa Nguvu ya Ulinzi huku mwilini ni matendo. Maana matendo ni ya huku mwilini na ndio Kinga Yako huku mwilini ,

Yaani

Ili uwe na ulinzi Roho ulinzi huo unaitegemea uwepo wa Imani,ambayo nayo Imani ya Rohoni inaitegemea Matendo ya huku mwilini Ili iwe hai,

Maana Imani ni ya kiroho eneo lake linakaa rohoni na ndio mazingira yake ,na makazi yake Imani ni rohoni ,Ila yenyewe matendo mazingira yake na makazi yake ni mwilini ,

Sasa Ili kule rohoni imani ana mtegemea matendo wa huku mwilini kama nguvu ya uhai wake kule rohoni ,

Ili Huyo Imani awepo kule rohoni ,awe na uhai,

Ni Kwa wewe kutenda matendo huku mwilini kule rohoni Imani anakuwa hai ,

Maana OKSIJENI YA UHAI WA IMANI HUKO ROHONI NI MATENDO YA HUKU MWILINI,MAANA IMANI KULE ROHONI HANA UHAI WALA UJANJA KAMA HUKU MWILINI HAKUNA MATENDO BASI KULE ROHONI NDIO UNA MUHUWA IMANI NA KUMKATIA HEWA YAKE YA ROHONI NI MATENDO YA HUKU MWILINI NDICHO IMANI ANACHOBKITEGEMEA, BILA HEWA YAKE AMBAYO NDIO MATENDO HUKU MWILINI KULE ROHONI IMANI ANAKUFA,

NA OKSIJENI YA UHAI WA MATENDO HUKU MWILINI INATEGEMEA UHAI WA KULE ROHONI YAANI KUWA NA IMANI ROHONI ,
MATENDO HUKU KATIKA MWILI SIKITU YATAKUWA SAWA NA MAHITI YAANI HAYAHESABIKI NA MATENDO HAYO YATAKUWA HAYANA UHAI KAMA HAYANA UHAI YAANI KAMA HAYAENDANI NA IMANI TULIOONGOZWA KUIFUATA, UKIKOSA IMANI ROHONI,MATENDO HAYO NI MFU HUKU MWILINI ,

MFANO UNAPAMBANA KATIKA MWILI KUWA MWANASAYANSI MKUBWA KUJA NA TEKNOLOJIA KUBWA HALAFU ,IMANI YA KUWA HIVO HUNA YAANI,MAANA IMANI KULE ROHONI IMEKUFA ROHONI HIVYO HUKU MWILINI MBIO ZOTE ZA KUFANYA MAKUBWA ZINAPATA UPINZANI WA KIROHO MAANA ULINZI WA HILO UNALO LIPAMBANIA HUKU MWILINI ,
LIMEKOSA ULINZI WA KULE ROHONI,
JAPO HUO NI MFANO TU WAKIMWILI ,

SASA ILI UFANIKISHE AU UFANIKIWE ,LAZIMA UWE NA IMANI AMBAYO ITAISAPOTI IMANI YAKO HUKO ROHONI YA KUJA KUFANIKIWA HUKU MWILINI ILI MATENDO YAKO YA HUKU MWILINI YALINDWE, MAANA ROHONI UNA UZIMA WA HAYO MATENDO UNAYO YAFANYA KATIKA MWILI AMBAO NGUVU YA UZIMA WA MATENDO HAYO NI ILE IMANI,

IMANI YAKO INATAKIWA ISAPOTIWE NA IMANI KUU

AMBAYO NDIO UZIMA WA IMANI ULIONAYO,

YAANI , NENO LA MUNGU INA NGUVU YA KUZALISHA IMANI. MAANA CHANZO CHA IMANI YETU NI NENO LA MUNGU.

Kiroho= Uhai wa Imani ni matendo,Ili Imani ihendelee kuwepo rohoni ,Ili huko Rohoni uendelehe kulindwa ,Huyo Imani anamtegemea matendo huku Katika mwili,Sasa kule rohoni ndio unalindwa,


Mwilini= Ili ulindwe mwilini ,Ina tegemea Matendo, maana matendo yanaonekana hivyo matendo Yako mwilini , na utachotenda kitategemea na ufahamu wa Imani inakuelekeza ufanye Nini ,Ili nayo hayo matendo huku mwilini yasife ,ukakosa ulinzi na kibali Cha Mungu ,


Uhai wa matendo mwilini inategemea uhai wa Imani rohoni ,na uhai wa Imani rohoni unategemea uhai wa matendo mwilini , na

Uhai wa ulinzi rohoni unategemea Imani Yako rohoni,na uhai wa ulinzi mwilini unategemea na matendo Yako mwilini,Ili ulinzi uwepo,




Sasa ,

Kwenye Upande wa Baraka,

Nimepokea mafunuo hapa ni hivi


Imani =roho

Matendo=mwili


Imani= Kugundia Teknolojia kubwa,hio unaipokea rohoni ,Sasa Ili hio Imani ije mwilini,

Inaitegemea Matendo ya Mwilini ya kiugunduzi wa Teknolojia mpya,


Matendo= Matendo ya utafiti wa kiugunduzi wa Teknolojia mpya,
(
Mfano,Unapokea Wazo LA kiugunduzi ,litalokushugulisha kulitafiti)

Unajishugurisha na Kazi za utafiti wa kiugunduzi wa Teknolojia mpya,

Career:TECHNOLOGY DEVELOPER,

FOCUS: IWE "RESEARCH AND DEVELOPMENT SCIENTIST OR TECHNOLOGIST "



Sasa ,baraka ya Mungu ,ni sawa na kibari Cha Mungu ,Katika utafiti huo MUNGU ANAACHILIA WAZO JIPYA LA KIUTAFITI AMBALO SIO TU JITIADA ZAKO ,
Au Anatanguliza Wazo ambalo utalishughulikia KIUTAFITI,

MAANA HAKUNA ANAESEMA LINIJIE WAZO FURANI ,WAZO LOLOTE JIPYA LINAKUJA SIO KWA MAAMUZI YA MTU ,


,WAZO PIA NI ROHO NDIO MAANA MTU ACHAGUI WAZO ,ILA WAZO HUJA LENYEWE TU,


NA MUNGU KWA KUWA NI ROHO HUJIBU KIROHO HIVYO NJIA NZURI YA BARAKA HIZO LINAPITA KWENYE WAZO,


IMANI= ROHONI; UNAPOKEA, WAZO AU MAWAZO YA KITAJIRI

MATENDO= MWILINI; MATENDO YANAYOHUSU KUUTAFITA UTAJIRI,MATENDO YA KUTENDEA WAZO LILE LA KITAJIRI,


UKIISHI KIMwiLI ,UTAISHI KUTESTI KILA WAZO ,ILA UKIISHI KIROHO UTAPOKEA WAZO TOKA KWA MUNGU NA YAKUPASAYO KUFANYA KATIKA MWILI YAANI MATENDO MWILINI.



NGOJA NIIDHIE HAPO ,

Tukumbuke,
Chanzo Cha kuumba Imani zetu ni Neno lake ,
Woow nimeipenda hii
 
HALI INAYOCHANGIA UWE NA NGUVU ZA MUNGU

1 Wathesalonike 5:17,19,21

[17]ombeni bila kukoma;
[19]Msimzimishe Roho;
[21]jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;

Unahitaji kuhakikisha kiroho na kimwili unakuwa na nyuvu za Mungu (moto wa Mungu)
Ushindi wako utapatikana kutokana na kiwango kile ulicho nacho rohoni cha NGUVU ZA MUNGU.

NA HAYA YANATAKIWA KUZINGATIWA KWAKO

[emoji2389] NENO LA MUNGU.....hakikisha unalo neno la Mungu la kutosha ndani yako....kumbuka neno lilikuwako tangia mwanzo na ndiye mwanzo....na huo MWANZO ndiko kuna chimbuko(MUNGU) la Mwanadamu
ambalo sasa hili sisi tuweze kuwa mahala hapo tunahitaji kuwa na NENO LA MUNGU
Yohana 1:1-12

[emoji2390] MAOMBI....Omba kila wakati ulio nao
Andaa mazingira mazuri yanayokuruhusu kuomba na sio kwa mizaa au mazoea. Hakikisha hakuna kinachokufunga au kukuzuia kuomba.
Maombi ni silaha lakini ni mpaka pawepo ma muunganiko mzuri wa wewe na Mungu.

Usiache kuomba...omba mpaka uone....usichoke kuomba hata kama huoni kupenya usichoke kuomba
OMBA BILA KUKOMA

[emoji2391] JITENGE NA KILA LILILO BAYA
Dhambi inakuondolea utukufu na kibali cha kuwa na Mungu. Dhambi inaondoa nguvu za Mungu maana kama Mungu hatokuwepo kwako basi nguvu zake hautokuwa nazo.....mkimbie shetani na uyakatae mambo yake yote.

[emoji2392] USIMZIME ROHO MTAKATIFU
Tumepewa ROHO MTAKATIFU atusaidie kwa kila jambo kwahiyo kila utakalolifanya ambalo halimfanyi Roho Mtakatifu awepo kwako basi unayaondoa mapenzi ya Mungu juu yako.

MFANYE ROHO KUWA RAFIKI YAKO ILI UWEZE KUSAIDIKA KWA KILA JAMBO LAKO LOLOTE.

VYOTE HIVYO VINALETA NGUVU ZA MUNGU.
NA MUNGU WA AKUBARIKI SANA KTK JINA LA YESU KRISTO.
Ubarikiwe
 
MUNGU MKUU WA WALOKOLE ANASEMA YEYE NI MWENYE HAKI TUBUNI HAPENDI UNAFIKI NA KUJIHESABIA HAKI NA KUKATAA WOKOVU....
NILIJARIBU KUMKIMBIA BAADA YA KUANDIKA MAKALA HII NA KURUDIA MAISHA YA KIDUNIA SABABU NILIOGOPA KUBEBA JUKUMU HILI ZITO ILA AMENIAMBIA JUKUMU LANGU NI MOJA TU KUWAELEZEA WATU UKUU WAKE NIPENDE NISIPENDE...!!!
NILIKUA KAMA YONA AMENIAMBIA ILA USIKU WA LEO UMEBADILISHA MAISHA YANGU...SABABU MZEE WANGU MMOJA ALIWEKA NADHIRI KWAKE......NA YEYE HAVUNJI AHADI.
MUNGU MKUU WA WALOKOLE AKIKUCHAGUA BASI UJUE AMEKUCHAGUA HUWEZI KUMKIMBIA AU KUJIFICHA...
TUTUBU MAANA BAADA YA KIFO NI HUKUMU.......
MM BINAFSI NIMETUBU NA AMENIAMBIA NIJISAMEHE MIMI KWANZA AFU NA YEYE ATANISAMEHE.....
TUTUBU NA TUISHI CHINI YA NEEMA ZAKE.
 
MUNGU MKUU WA WALOKOLE ANASEMA YEYE NI MWENYE HAKI TUBUNI HAPENDI UNAFIKI NA KUJIHESABIA HAKI NA KUKATAA WOKOVU....
NILIJARIBU KUMKIMBIA BAADA YA KUANDIKA MAKALA HII NA KURUDIA MAISHA YA KIDUNIA SABABU NILIOGOPA KUBEBA JUKUMU HILI ZITO ILA AMENIAMBIA JUKUMU LANGU NI MOJA TU KUWAELEZEA WATU UKUU WAKE NIPENDE NISIPENDE...!!!
NILIKUA KAMA YONA AMENIAMBIA ILA USIKU WA LEO UMEBADILISHA MAISHA YANGU...SABABU MZEE WANGU MMOJA ALIWEKA NADHIRI KWAKE......NA YEYE HAVUNJI AHADI.
MUNGU MKUU WA WALOKOLE AKIKUCHAGUA BASI UJUE AMEKUCHAGUA HUWEZI KUMKIMBIA AU KUJIFICHA...
TUTUBU MAANA BAADA YA KIFO NI HUKUMU.......
MM BINAFSI NIMETUBU NA AMENIAMBIA NIJISAMEHE MIMI KWANZA AFU NA YEYE ATANISAMEHE.....
TUTUBU NA TUISHI CHINI YA NEEMA ZAKE.
Tunamshukuru Mungu Kwa ajili yako....karibu Tena zizini
 
Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.

Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.

Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.

Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.

Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.

Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".

Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.

Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.

Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.

Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?

Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?

Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?

Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?

Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.

Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.

Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.

ITAENDELEA
Hata mie naanza kutambua hilo maana Kanisa langu Katoliki hapa limeanza nalo kuwatoa mapepo watu na kuwaponya wagonjwa nje ya mahospitali eti kwa nguvu ya Mungu. Pia hata tafsiri ya majina sasa imeelekezwa kilokole.
 
Dah uzi huu bhaana eti mungu wa walokole dah[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wanajimu wote waongo tu na hata hao waloloke nao waongo tu labda dini ya wachawi
 
Back
Top Bottom