Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mwanzo ulipokua unasema walokole walokole sikuelewa, niakajua unaongelea makanisa ya kilokole.
Lakini kadri uzi unavyoenda nikaelewa kua watu wanatangatanga na makanisa bure tu, MUNGU yupo popote..

Wakati niko primary nilikua na imani kwelikweli, nikikumbuka enzi zile nilikua tofauto kiimani na watoto wenzangu. Nilikuwa nikimuomba MUNGU kitu kinakua.
Nakumbuka kuna siku nilipoteza kitabu cha hesabu na tulikua tunakaribia kufunga shule, na ticha alisema kama umepoteza kitabu itabidi ulipe na mimi kumwambia mshua naogopa. Basi kuna siku nilisali sana, nililia na MUNGU mno, ajabu kesho yake nilikuta kitabu kwenye begi langu wakati kilipotea kitambo sana.

Kiukweli kipindi kile nilikua na imani sana, nikisali inakua, tena vilevile au zaidi ya kile kwa njia tofauti.
Kwasasa nshakua kijana wa hovyo ila maisha ya wokovu yana raha sana aisee. Ukianza wokovu tangu utoto wako bila kupuliziwa moshi akilini alooo utapata raha maisha yako yote, utakua na stress ila MUNGU atakushangaza.
Mitihani mingi shule nimepass kimiujiza tu baada ya kusali sana.

One day Yes nitarudi kwa miguu yote miwili kwa Muumba.
Rudi ndugu yangu, Mungu anakupenda
 
Mwambie arudishe bandari ya Dar es Salaam, walokole wanawalalamikia Waarabu wa Unguja wameiuza bandari kwa Waarabu wenzao wa Dubai.
Sijui kwanini unaingiza mambo ya bandari hapa anyway pole Sana
 
Kuna uzi fulani hivi kuna mdau alielezea vizuri kuhusu Mungu.alifafanua vema kuwa haijalishi dini yako nanukuu unapouweka mwili wako mbali na manungunik visasi kuwa na moyo wa upend ni rahsi sana kuwasilian na Mungu
Mwanadamu ni mfano wa Mungu, Si sura ya mwili Bali roho yako.. Ukitaka kujua hilo, angalia kama Kuna mwanadamu a napenda mambo mabaya.. Na kujitapa kwa hayo.. Jibu nin Hapana, maana hata wezi. Wachawi, walawiti wote wanampenda waonekane wema.. Maana hiyo ndio asili ya Mungu, yeye ni Mtakatifu, Haki Na mwema. Ndio maana anasema, Hakuna Amani kwa watendao Mabaya, bse jinsi tumeubwa ni nafsi za Utakatifu, hivyo nafsi zetu zinapata Amani tukitenda Mema,... Ndio maana wale wote wanaojidai kuwa Mkristo kafiri, huwa naelewa Nafsi zao zimetawaliwa na Yule Mwovu, sibishani nao Bali nawaombea... Maana uasili wao ni ya Mungu, ila shetani kawadanganya. Na neno lina Sema, kila atendae Mema/Haki ni wa Mungu.. Ndio maana ni rahisi kuconnect na Mungu tukitenda Mema🙏🙏
 
Nikaote jua badala ya kuota ndoto?

Mie naota Dirham saa hizi wewe unanletea mambo ya jua?

Unanshangaza.
Kama nakuona unavyoumia ukiwaona watu wa Mungu wanapeana habari njema kwa staha na bila kugusa dini nyingine.Nakushauri ubadili methodology ya kueneza dini yako bila kashfa na maneno ya shombo kwa wasio wa imani yako ili wauige mfano wako wasilimu.
Hebu anzisha uzi wewe na wenzio kwa lengo la kuwavuta watu kwenye dini yako.Naamini watu wanaimisconceive.
 
Kama nakuona unavyoumia ukiwaona watu wa Mungu wanapeana habari njema kwa staha na bila kugusa dini nyingine.Nakushauri ubadili methodology ya kueneza dini yako bila kashfa na maneno ya shombo kwa wasio wa imani yako ili wauige mfano wako wasilimu.
Hebu anzisha uzi wewe na wenzio kwa lengo la kuwavuta watu kwenye dini yako.Naamini watu wanaimisconceive.
Dini nyingine ndiyo ipi? Kuna neno lipi la Mungu linaloongelewa hapa, Mungu yupi? Biblia inasema Mungu wa dunia shetani, ndiyo huyo anaongelewa, au yupi?
 
Dini nyingine ndiyo ipi? Kuna neno lipi la Mungu linaloongelewa hapa, Mungu yupi? Biblia inasema Mungu wa dunia shetani, ndiyo huyo anaongelewa, au yupi?
Kuna tofauti ulichokiandika hapa na kwenye Biblia" Biblia inasema mungu wa dunia hii"sio Mungu wa dunia hii" angalia capital M na R pale unaposoma Biblia itakusaidia.Utakuta Roho na roho ,Mungu na mungu.Uliza kwa Bible Scholars ujue tofauti .
 
Hizi tusome tu kama riwaya lakini ni chai! Hadithi yake haiko compatible na mafundisho ya Ukristo.

Ila hadithi ni tamu!
 
Walokole waanatumia biblia moja...ila katika mapokeo yao ya neno yamewekwa ndani ya mioyo yao na wanayaishi

Labda nikupe mfano hapo kwa Lutheran...

Mimi ni mlutheran hadi kipaimara nimesoma ila sasa nimeokoka ni mlokole...ishu sio dhehebu...

Siwezi kuzungumzia suala la hao Manabii na mafuta wanayotumia maana ni wapakwa mafuta ya Bwana...

Ila ninaouwezo wa kupima Roho zao nikajua huyu ni wa Bwana na huyu sio...
Ulivyokuwa Mlutheri hukuwa umeokoka? Kuacha dhambi kupitia toba ni kazi ya kila siku kwenye safari ya Wokovu! Ubatizo ndio wokovu wa kweli maana unakupa funguo ambayo huwezi kuipata nje yake.

Huko kwenye wokovu hakuna dhambi? Au wewe hutendi dhambi?

Lutheran ndio baba wa ulokole, umeanzia huko lakini bado mnaenda kuutafuta kwingine na kuishia kuwa watumwa wa watu waliojivika kuwa na nguvu za Mungu ambazo wanaweza kuziachilia wanavyotaka.
 
Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.

Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.

Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.

Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.

Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.

Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".

Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.

Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.

Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.

Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?

Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?

Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?

Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?

Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.

Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.

Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.

ITAENDELEA
Aliyeanzisha uzi huu amekimbia hii inatia mashaka juu ya uadilifu na uaminifu wake!
 
Dini nyingine ndiyo ipi? Kuna neno lipi la Mungu linaloongelewa hapa, Mungu yupi? Biblia inasema Mungu wa dunia shetani, ndiyo huyo anaongelewa, au yupi?
Maswali ya vijiwe vya kahawa.Ngoja nichague kukupuuza!
 
Kwanini walokole wana nguvu?

Jibu: Walokole wamemkaribisha YESU akae ndani yao, wanamuamini kwa Kila wafanyalo, hii inafanya sasa Mlokole awe ananguvu maana anayemtu anamsaidia ambaye ni Roho Mtakatifu

Kwanini sio wanaosali makanisa kama Lutheran na Catholics?

Jibu: Wanaosali makanisa hayo ulivyotaja pia wapo waliookoka nao wanazo nguvu, ila wengi wao hawana nguvu hizo, ni kwakuwa wao wanaishi kwa Sheria za kanisa na mazoea...
Umejibu vyema sana
 
Maswali ya vijiwe vya kahawa.Ngoja nichague kukupuuza!
Kabisa kabisa, teknolojia imehamishia vijiwe vya kahawa kiganjani.

Ni heri upuuze ili nami nibaki na wasiyo puuza. Naamini unaondoka huku hoja imekuingia vizuri na haijibiki kiwepesi.

Ni vyema tunashindana kwa hoja, mmoja akiona hayawezi anaondoka kwa heshima kabisa kama ulivyoamua, tunaagana, tukikutana kijiwe cha kahawa cha kiganjani, tunaongea hoja zingine. Kwa furaha na amani.

Naakutakia kila la heri.
 
Back
Top Bottom