Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Nikili tu ya kuwa Huu uzi umenifanya nikue kiimani
Maana umenikumbusha mambo mengi sana sana tangu nikiwa mtoto mpaka kijana.
Kuna wakati nilipokuwa nimetekwa kupelekwa mererani kutolewa kafara,
Kuna mambo ya ajabu niliona yakishuka angani kwa macho yangu, kuna siku nikipata muda nitaweka, wakati huo nikiwa mtoto wa miaka 8.
Sio tu hili, nilipishana na makundi ya wanyama hatari kama Nyati, majoka makubwa ambayo yalikuwa yanauwezo wa kunimeza kwa dakika 0, simba, chui, lkn hawakuweza kunidhuru, nilikuwa najiona nipo kwenye kundi la watu wenye moto mkali ambao pumzi zao zinawasukuma na kuwapumbaza wale wanyama. Rohoni nilikuwa nina amani kubwa mnoo japo kuwa nipo katikati ya hatari.

Kupitia andiko hili sasa nimejua mengi
Asante mwandishi[emoji91][emoji91][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Usisite kutuletea huo ushuhuda kiongozi
 
Mkuu vipi kuhusu kusikiliza nyimbo za gospel kitu Gani Hua kinatokea MTU anapokua anaimba au kusikiliza wimbo wa gospel Uwe wa kuabudu au kusifu....binafsi Hua najikuta nabubujikwa sanyingine nanena Kwa lugha Yan nkiomba huku nimefungulia gospel Hua Naona maombi nakua spiritual zaid tofaut nkiomba bila kufungulia gospel
Yaani ,kiroho KULIA NDIO KUIMBA NYIMBO NZURI ROHONI,
SASA KWA KUWA UNAIMBA KWA BUBUJIKO ,BASI HAPO UKO KIROHO UNAKUWA UMEUGUSA MOYO WA MUNGU ,ENDAPO UTAABUDU HIZO NYIMBO KATIKA ROHO NA ILE KWELI YAKE.
 
Wokovu unahubiriwa na akina nani?
Si Walokole ndo wanahubiri?
Ujue kuokoka sio tu kutubu na kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi, hiyo ni step ya kwanza ya Imani, step ya pili ni kumpokea Roho Mtakatifu, step ya tatu ni kuishi maisha Matakatifu Ili uendane na Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu atakuwa mwalimu wako mzuri sana , na ukitia bidii na nidhamu, utaenda in a high dimension, kuishi kama Mwana wa Mmiliki alivoishi hapa duniani..
Shida ipo hakuna Mungu wa walokole kuna Mungu wa wote ili ukubali yupo ndio unamkubali awe kwenye maisha yako
 
Hadithi njoo utamu kolea ... Utafiti wa miaka 22 ulianza ukiwa na miaka mingapi ?
 
Hapo Ili maanisha vingine,

Yaani , yesu alikuja kuusulubu mwili ,ambao mwili huo umebeba dhambi za watu ,adhabu ya Dhambi za watu alizibeba Mwenyewe Katika mwili wake,

Na mwili ndio huyo nyoka, maana mwili hivi Leo ndio mjaribu wetu,
naomba unifafanulie zaidi kuhusu hizo picha
 
Hao watu wasio binadamu hawajiweki katika race ya kizungu tu.Wanaweza kua race yoyote ile.Siri za Mungu wa walokole na siri za yule mwana wa mmiliki hakuna anaezijua hata kurudi kwake ni fumbo.Kuhusu watu wasio binadamu ni wale watu warefu wasioakisi mwanga ambao wana vita na mwana wa umliki wapo wengi tu duniani katika race tofauti tofauti.Na pia wale watu warefu wanaowalinda walokole wapo wengi tu katika maumbo ya kibinadamu wakitimiza majukumu yao ya kuwalinda walokole ambao katika ulimwengu wa roho wanaitwa wana wa Mungu mkuu mwenye nembo ya kungaa kuliko jua angani inayosomeka kwa lugha za kibinadamu kama ALFA NA OMEGA.
uh! Mkuu msaada tafadhar, unaposema "nembo ya kung'aa kuliko jua inayosome kwa lugha ya kibinadamu ALFA NA OMEGA" unamaana gani?
 
Shida ipo hakuna Mungu wa walokole kuna Mungu wa wote ili ukubali yupo ndio unamkubali awe kwenye maisha yako
Nakuomba, ukafuatilie kwanza , ASILI NA HISTORIA YAKE ,Hilo Neno walokole,

Halafu ,ndio uje Tena kutupinga Tena,na kaushaidi kama ulivyofanya mwanzo Kupitia Google,
 
Mkuu vipi kuhusu kusikiliza nyimbo za gospel kitu Gani Hua kinatokea MTU anapokua anaimba au kusikiliza wimbo wa gospel Uwe wa kuabudu au kusifu....binafsi Hua najikuta nabubujikwa sanyingine nanena Kwa lugha Yan nkiomba huku nimefungulia gospel Hua Naona maombi nakua spiritual zaid tofaut nkiomba bila kufungulia gospel
Kuna nyimbo mnaziita injili,,hizi nyimbo asili yake ni kwa wale watu warefu wenye mabawa na wanaziimba masaa ishirini na nne.Nyimbo zoote za injili na kusifu walizitunga wao!!Unapoziimba kabla ya kusali ni kama unawaita waje msali pamoja.
 
Kilinikutaga pia Mimi nlikua namsaidia Sana Kwa Upendo Mungu alikuja kunifunilia Ni watu wa Aina Gani...ili nibidi nisitishe msaada Kwa Hao watu Ila Kwa wengine misaada kama kawaida
Saidia wote ili uwe na alama ya upendo,,,,inakaa moyoni mwako kwa umbo la tunda na imezungushiwa taji..Kiroho inakutambulisha wewe kama mlokole wa kweli..UPENDO BILA KUJALI AU MAWAA AU MAJIVUNO AU KUTEGEMEA KURUDISHIWA FADHILA..NDIO SIFA KUU KIROHO YA WALOKOLE
 
Mungu wa watu yukoje?
Elezea kwa Maandiko matakatifu ndo tutaelewana.

Sio kwa maneno matupu.
MUNGU aliyeumba mbingu na nchi, Mtakatifu wa Watakatifu haabudiwi na kila mtu. Ndo maana alijiita " Mungu wa Israeli" mara nyingi katika agano la Kale na wakati pale Middle east kulikuweko na Wafilisti, Wayebusi, Wagibeon, Waamaleki, Waamori, Wamoabu , Waamoni. Unajua kwanini hakujiita "Mungu wa Wafilisti "? Je Wafilisti sio watu? Ni kwasababu walikataa kumuabudu wakaamua kumuabudu Dagon kama Mungu wao.
Swali zuri ila mimi namshuudia Mungu wa jamii ya watu wanaojiita walokole kama anavyotambulika kwenye ulimwengu wa kiroho.Na kuna binadamu weeengi hawamwamini huyu Mungu ila wachawi na wanajimu na wahesabu namba za jua la mashariki na waganga na walw watu warefu wasioakisi mwanga wa jua wanamuogopa sana huyu Mungu wa walokole.Na hao walokole wamesambaa dunia nzima na wana alama zao kiroho..Ndio namuelezea Mungu wao na mtoto wake aitwae Mwana wa mmiliki na Roho yake iitwayo roho kuu ya nafsi hai..Huwezi kuelewakiurahisi mpaka uwe unaujua ulimwengu wa nje ya mwili kwa kina.
 
Unajua unatakiwa muda wakuelekezwa hakuna Mungu wa walokole ila kuna mungu wawatu
Yupo na wanajimu na wachawi na waganga wanamjua kwa jina la Mmiliki na ana roho tatu ndani ya roho moja ndani ya nafsi tatu.Ambazo ni mwana wa mmiliki na Roho kuu yenye kutoa pumzi ya uhai au oksjeni
 
Je inachukua muda gani kwa Mmiliki kujibu maombi ya Walokole?
Je ukiomba utajiri kwa Mwana wa Mmiliki, anaweza kukupa?
 
Mungu amewaumba watu wote ila sio Mungu anayetumikiwa na wote.

Mungu wa walokole ndo Mungu wa Utakatifu wa hali ya juu na anaabudiwa na walokole tu, hakuna dini nyingine inayomuabudu Mungu kama huyo.

Mungu wa Walokole ni wa tofauti na miungu mingine, kila dini Ina mungu wake, na hawafanani kabisa. Kama huishi maisha ya Utakatifu na kumuamini Bwana Yesu, basi humtumikii Mungu wa walokole, eidha unamtumikia mungu mwingine eidha kwa kujua ama kutojua.
Mkuu upo sahii,,Mungu wa walokole Ndio mungu anaeogopeka sana kwenye ulimwengu wa kiroho,,,,NIMESHUHUDIA KWA MACHO YANGU
 
Je inachukua muda gani kwa Mmiliki kujibu maombi ya Walokole?
Je ukiomba utajiri kwa Mwana wa Mmiliki, anaweza kukupa?
Sekunde hiyo hiyo...Tatizo walokole hawana uwezo wa kuona majibu yao kwa sababu wapo mwilini..Kabla hujayaona kimwili,,tayari umeshajibiwa..NDIO MAANA NGUZO KUU YA WALOKOLE NI IMANI NA KUAMINI
 
Back
Top Bottom