Mungu Yuko wapi?

Hakufa?

Daktari aliyesaini cheti chake cha kifo alidanganya?

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza aliyesaini kwa niaba ga Serikali ya Tanzania hati ya kuwaruhusu madaktari kuziona mtambo wa Oxygen naye alishiriki uongo?

Binti wa Msuya aliyekuwa naye huko Uingereza aliridhia baba yake kusingiziwa kifo?

CDF wa kipindi hicho, Davis Mwamunyange ambaye ndiye aliyemsainia kibali cha kwenda kutibiwa Uingereza, angekubali Jeshi kudanganywa?

Maandalizi ya mazishi yaliyokuwa yakifanywa na JWTZ, kabla ya baadaye taarifa kutolewa kuwa marehemu kafufuka, nayo yalikuwa maigizo?

Kifo chake kilitangazwa na Serikali, lakini suala la yeye kwenda Mbinguni na Jehanamu, ni ushuhuda wake binafsi.
 
BASI Sawa mkuu...
 
No...siamini superstition yoyote that includes the bible na maujinga yote ya dini mauchawi sijui nyota zote ni fikra za watu wazamani walioshindwa kuelewa dunia
Kama huamini kuwa Kuna uchawi, unastahili kupewa pole. Isije ikawa umeshalogwa! Kitendo cha kutilia mashaka juu ya uwepo wa Mungu si jambo la kawaida.

Unasemaje kuhusiana na matukio ambayo yameshawahi kutokea maeneo kadhaa hapa Tanzania, ambayo yapo beyond Science explanation?

Humu Jamii Forum, kuna nyuzi zenye taarifa ya vifo vyenye utata, mfano, mtu kufa na kuzikwa na baada ya muda akaonekana akiwa hai, na Polisi walipofukua kaburi wakakuta gogo badala ya maiti.

Hayo matukio unayaelezeaje? Yashatokea Mwanza, Kigoma, Simiyu, n.k., na kote huko, Polisi walithibitisha.
 
Biblia ni Jibu la kila Swali katika maisha yako;Hivyo basi soma Biblia.
 
Kuamini juu ya uwepo wa Mungu ni tofauti na kumwamini Mungu.

Kumwamini ndiko kunakomfanya mtu awe na matendo yanayoshabihiana na imani yake.

Hata Shetani na wachawi wanaamini kuwa Mungu yupo, lakini wamechagua kutokumwamini, hivyo matendo yao yanapingana na matakwa ya Mungu.

Mtu anaweza kuamini juu ya uwepo wa Mungu na bado akatenda kinyume na Mungu, lakini yeyote anayemwamini Mungu hata matendo yake yataakisi hivyo.
 
Hakufa Sasa unalazimisha au...which one is more likely the law of nature zimekuwa suspended kwa ajili yake peke ake au wamekosea kumdiagnose, doctors ain't perfect so they make mistakes. Nimekuuliza if kufufuka is real na hao unaosema wamefufuka, mbona Kuna story tofauti kuhusu hio mbingu na motoni, tumsikilize nani tumwache nani...nijibu bac naona unakazia sijui Nani kaona kafa nijibu swali.. why different stories abt heaven n hell
 
Mungu yupi Sasa wapi 3000
 
Sijui hao uliowasikiliza, ila mimi niliutoa huo mfano Msuya kwa vile ni mtu anayefahamika.

Ubishi hautasaidia mkuu. Mbingu ipo, na jehanamu ipo pia. Bora ufahamu hilo mpema na ukafanya uamuzi sahihi kungali muda unaruhusu.

Hakuna kukata rufaa Jehanamu.
 
Hahaha ndo mnatishiana hivyo...nijibu kibaolojia.. Nini kitachoungua baada ya Mimi Kufa. Kama ni roho, Ina ngozi Ina nerves na pain receptors Ina misuli why niogope siwezi skia maumivu coz pain inahusisha ubongo na spinal cord ambayo Sina mda huo. If ni mwili, unatoka wapi, unajiphotocopy...in short hii concept ni ya mababu na kwa elimu ya saa hivi inafeli in logic na reason ndo maana mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa na kuwaza ataungua baada ya kufa ni vitisho vya ajabu kisa watu wajinga bac
 
Mwenye Enzi Yote.
Kila dini Ina Mungu wa hivi, wako ndo anajulikana zaidi... Either Yahweh au Allah wote wametengenezwa na jamii zao husika na wanasheria na historia kutokana na jamii zao na kipindi chao.
 
Hii dunia hata kwa akili za kawaida tu, ina chanzo. Na hiko chanzo ndio tunakiita MUNGU.

Shida kubwa hapa ni dini. Haswa ukristu na Uislam. Ni sheeda.
 
Wewe n mtaalam wa Biology?

Wanasayansi wanakiri kuwa mpaka sasa, ni sehemu ndogo tu ya ubongo ndiyo ishafahamika kiufasaha. Bado sehemu kubwa haijulikani, tafiti zinaendelea.

Hata miaka ya nyuma, iliaminika kuwa ubongo ndiyo akili, toafauti na inavyofahamika sasa, kuwa ubongo ni kama hardware na akili ni software.

Wewe unajifahamu vizuri? Unafikiri huyo anayeonekana kwa macho ya nje ndiye wewe halisi? Noo!!!

Mwili wako ni jengo la roho yako. Wewe halisi ni roho, na una nafsi. Ndani ya nafsi ndiko kulimo na akili. Hata wataalamu wa Elimu Viumbe na Elimu nafsi wanalifahamu hiloe. Au unafikiri neno SUBCONSCIOUS MIND limetoka wapi?

Mtu anapokufa, haimaanishi kuwa anapoteza uwezo wa kujitambua. Kinachotokea ni yeye kutokuwa na uwezo wa kuwasiliana na ulimwengu wa asili. Anapokufa, anatoka kwenye mwili wake na kuelekea panapomstahili.

Akiwa ameshatoka kwenye mwili wake, anakuwa timamu katika mambo yote, ikiwa ni pamoja na kuhisi maumivu endapo mwili wake wa kiroho utaumizwa.

Usijifariji kuwa endapo utaishia Jehanamu hutaweza kusikia maumivu. Si kweli. Jehanamu ni mateso na vilio visivyo na mfano.

Pakimbie.
 
Hayo maumivu ya moto unayesiaje bila kuwa na ubongo, ngozi, spinal cord na nerve cells. Unajua dawa ya kuuwa ganzi inafanyaje katika mwili. Sasa ndo ukishaelewa medicine, ukijua maumivu yanasababishwa na Nini...utaacha kuamini story za watu wa kale ambao hawakujua chochote kuhusu mwili wa binadamu...eti moyo ndo unafikra na ndo una roho jamani jamani.. biology form 2 rudini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…